Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Tumuite msaliti Lema na ikiwezekana tuandamane basi kama unaona kakosea,mambo mengine hayahitaji akili nyingi kuona hili sawa au la

Yeah kama ambavyo haikuhitaji akili nyingi kuona kuwa kilichopo hapa ni udikteta tu na si jingine.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nakumbuka mwaka juzi kuns cartoonist alimchora Zuma with his genitalia hanging. Hakuns walichomfanya huyu cartoonist zaidi ya basdji ya watu kulalamika tu. Walichobshstika kufaulu watu wa serikali ni kuiomba mahakama iamroshe ile katuni isowekwe tena public. Lakini cartoonist hakufanywa chochote kws sababu ya umuhimu mkubwa wa fredom of speech kwa SA. Ingekuwa kwetu sijui ingekuwaje!

Umeona eeh...
 
Tumuite msaliti Lema na ikiwezekana tuandamane basi kama unaona kakosea,mambo mengine hayahitaji akili nyingi kuona hili sawa au la
Kweli kabisa pengine Lema ni msaliti!
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
ni kweli kabisa kiongozi nakuunga mkono.
Lakini pia ungetumia nafasi hii pia kuuleza umma pia hata kiongozi mkubwa awe mstaafu au operational na wao pia wawe makini na kutoa maneno ya kuudhi wengine kama "wapumbavu na malofa", "vi..lz", "nonsense". Tangu democrasia imeshamiri duniani Karne 19 viongozi walitoka kuwa wasiogusika wala kukosoleka. Sasa wako wazi kwa criticism, na pia walitoka kutoka kuwa Watawala wa watu hadi kuwa Watumishi wa watu yaani watu hao wasipokutaka utatoka kwa utaratibu wa kidemocrasia.
Misingi hii ya kidemocrasia imesababisha nchi nyingi kubadili hata sheria zao ziaccommodate mawazo pinzani,kukosolewa,

Sasa hivi hata ukitaka kuandika unajikuta unafanya editing mara mia angalau usijikute umeingia kwenye kitu wanaita "seditious intention" kosa ambalo nchi nyingi imeliondoa kutokana na kunyima uhuru na lack of clarity ya kosa lenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
KIJANA ALIKOSEA KWELI AJIFUNZE KUJENGA HOJA ZA KISIASA

KWA UPANDE WA PILI ANGESAMEHEWA INGELETA PICHA YENYE KUVUTIA ZAIDI KULIKO IYO ADHABU YA KUWAFANYA WAOGOPE KUMZUNGUMZIA RAISI KWA MAMBO AMBAYO ANAKOSEA

.....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara "

Godbless Lema (Mp)
Huo ni ukomavu wa kisiasa. Ikumbukwe mtu anayekuzidi umri au madaraka ni kufuru kumtusi.
 
Mean while kuna wanaopeta mtaani baada ya kuwaita wenzao wapambafu na malofa na wengine wakaita wengine viladha.
 
Yeah kama ambavyo haikuhitaji akili nyingi kuona kuwa kilichopa hapa ni udikteta tu na si jingine.
Hamna udikteta wowote ukweli ni kwamba kijana hana adabu tena hakustahili faini kabisa ilitakiwa akiliwe kiboga ndio angejifunza kuwa na adabu
 
Watu wengi hatuungi mkono lugha ya matusi iwe ni kwa rais wa nchi au mtu mwingine yeyote.Ni mawazo yangu kwamba watu wengi waliomchangia yule kijana walifanya hivyo sio kwa kuunga mkono ule utovu wa nidhamu aliofanya kwa rais bali walifanya hivyo kuonyesha jinsi wasivyokubaliana na sheria yenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kabisa Mkuu hii yote ni kutaka kuwatia hofu tu Watanzania tuwe na woga wa hali ya juu kuikosoa hii Serikali ambayo kwa maoni yangu imeanza vibaya sana.

Chukulia mfano wa yale aliyoyasema Mchungaji Gwajima, mimi sijaona neno baya lolote alilolisema Gwajima kiasi cha kusakwa kwa nguvu kubwa sana utadhani ametamka kwamba anataka kuipindua Serikali.

Polisi wawafuatilie wahalifu mbali mbali nchini wakiwemo wezi, wapokea rushwa, majangili, wauza unga ambao uhalifu wao nchini unaifanya Tanzania ikose maendeleo ya kweli. Watu wanaotoa kauli kama ya Gwajima hawastahili kabisa kusakwa hata kwa sekunde moja na hivyo kupoteza nguvu kubwa ya polisi na masaa yao chungu nzima.


Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
 
Kwa hiyo Lema ni msaliti aa mabadiliko?
Lini wapinzani wa Bongo wamewahi kulipwa kwa siasa za kistaarabu?Huyu Lema kesho na keshokutwa anaweza kupigwa virungu kama sio mabomu ya machozi na nyie wafuasi wa CCM mnaomsifia leo hii ndio mtakuwa wa kwanza kumkejeli na kumdhihaki na hata huyo anaemtetea leo hii nae hatamsaidia kwa lolote.
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.

Duuh, wewe nadhani hujamwelewa Lema!

Hebu rudia tena kumsoma, labda umejiwahi tu kuandika na kupost!!
 
Tunako elekea kwa tabia hizi kuna watu humu hata kuwatusi wazazi wao wataona ni sawa tu!

Kupinga hoja za mtu si lazima utoe matusi kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe! Zitto anapost mara 20 kwa siku ili kufikisha ujumbe lakini hatoi matusi?!

Chukulia Raisi angekuwa babako afu mtu anamtusi Bwege haki ya nani ningekuwa ni mimi ndiyo mtoto wa Raisi ningeanza na huyu jamaa hata kabla ya mahakama!
 
Back
Top Bottom