Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Mkuu Godbless J Lema Mbona wewe ulimuita waziri Mkuu Pinda MWONGO kama SHETANI? Bwege na shetani lipi kubwa?

Hata mimi siungi mkono, ila adhabu aliyopewa huyu kijana ni kubwa kuliko! Hatukuwa na namna zaidi ya kumuwezesha ili amalizane na tatizo hilo.

Hata hivyo hii sheria ya mtandao ni kandamizi mno halafu inakata upande mmoja.
 
Ukiwa mwanasiasa kuwa na ujasiri wa kupokea yote na kuvumilia yote ndio sifa kuu ya viongozi shupavu, hakuna anaeunga mkono dhihaka dhidi ya rais au binadamu yeyote, lakni kinachopingwa ni adhabu na muamsho dhidi ya sheria mbovu ya mawasiliano ya mtandao...
hats wew jua kuwa hatukuungi mkono wew tunaunga mkono unachokisimamia, siku ukijichanganya tunakubwaga tu Kama wenzako..
Mmechanganyikiwa
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali , lakini kwa hakika kabisa siungi mkono Rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu . Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
Lema sasa naona umeanza kuwa mtu mzima na muelewa sana! Na kupongeza kwa kulitambua hilo na ninajua huu ujumbe umewafikia wale walio mchangia kwania ya kumbeza Rais!

Hongera sana kumbe na wewe una chembe ya busara na hekima! Lakini huu ujumbe ili bidi uwafikie wale wabunge na vijana wachadema walio changishana wazi wazi kwa kejeli ili kumuunga mkono yule kijana mpumbavu!

Hakika umeanza kuwa mkubwa na umekuwa kabisa hongera sana!
 
Mkuu GODBLESS J Mbona wewe ulimuita waziri Mkuu Pinda MWONGO kama SHETANI? Bwege na shetani lipi kubwa?
Hata mimi siungi mkono, ila adhabu aliyopewa huyu kijana ni kubwa kuliko! Hatukuwa na namna zaidi ya kumuwezesha.
Hata hivyo hii sheria ya mtandao ni kandamizi mno halafu inakata upande mmoja.
Tangu ujiunge na Team Mamvi hakika unaongea pumba sana. Umeshaiga mambo ya BAVICHA
 
Lema sasa naona umeanza kuwa mtu mzima na muelewa sana! Na kupongeza kwa kulitambua hilo na ninajua huu ujumbe umewafikia wale walio mchangia kwania ya kumbeza Rais!

Hongera sana kumbe na wewe una chembe ya busara na hekima! Lakini huu ujumbe ili bidi uwafikie wale wabunge na vijana wachadema walio changishana wazi wazi kwa kejeli ili kumuunga mkono yule kijana ********!

Hakika umeanza kuwa mkubwa na umekuwa kabisa hongera sana!
Kwa mara ya kwanza na mimi nimemuunga mkono leo
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Adhabu aliyopewa si kwa sababu ya kosa alilolifanya.

Ni kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
 
Asante Lema,

Lakini mbona kama alichangiwa 4.5m za faini na viongozi wa chama chako mkoa, au mlimchangia baadae mkamwambia lakini kijana umekosea au ulinyamaza kimya.
Swali la maingi sana. Inawezekana wameanza kufarakana huko kwenye kumchangia huyo kijana
 
Swali la maingi sana. Inawezekana wameanza kufarakana huko kwenye kumchangia huyo kijana
Ni wazi kwa post hii ya Lema hajapendezwa na kile kitendo tena kuchanga hadharani ndio kumeonesha kejeli zaidi na kuyaunga mkono matusi dhidi ya Rais...!

Hakika Lema kanitoa machozi kwa uzalendo alio onesha!

Lema amepingana nao wazi wazi wala hajajificha!
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
Lema umechemka tena mbona ulikaa kimya mkapa alipowaita sumaye na Lowasa wapumbavu. Kwangu mimi upumbavu ni tusi kubwa kuliko bwege. Sheria lazima zifuatwe na watanzania wote akiwemo rais na mawaziri. Kiukweli sikushangai labda unaitafuta gear ya kurudi bungeni maana katika watu ambao hawaaminiki ukawa ni wewe umetokana sana Lowasa wa watu baada hata haya huna ukajifanya unapiga kampeni ninyi wanafiki wa cdm na ccm Hukurupuki yenu Mungu anaijua kwa kuwqfanyq watanzania kama mizoga ama wana utindia ubongo kwa uovu wao
 
Ndiyo, kwani ye ana damu ya hudhurungi?

After all, mi na walipa kodi wengine tunamlipa mshahara na kumtunza.
Kama hii ni hoja yako vasi kulikuwa hakuna umuhimu wa Rais kuwa na ulinzi kama anaopata kwa gharama ya walipa kodi.

Tatizo unaongelea nadharia. Mimi ninaongelea uhalisia.

Rais wa nchi ni tofauti na mwananchi mwingine nchini.

Heshima kwa Rais lazima ilindwe lakini vilevile ni lazima na Rais ajiheshimu.
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Unawezaje kujilinganisha na rais wakati hata ujumbe wa mtaa huna,lazima utambue heshima anayopewa rais ni taasisi si kama mtu binafsi
 
Adhabu aliyopewa si kwa sababu ya kosa alilolifanya.

Ni kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Adhabu ile hipo kisheria kabisa haijatokana na matakwa ya judge..sheria ya mtandao.
 
Ni wazi kwa post hii ya Lema hajapendezwa na kile kitendo tena kuchanga hadharani ndio kumeonesha kejeli zaidi na kuyaunga mkono matusi dhidi ya Rais...!

Hakika Lema kanitoa machozi kwa uzalendo alio onesha!

Lema amepingana nao wazi wazi wala hajajificha!
Mambo ya Orlando haya!
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.

Walipokuwa wanawasilisha michango walikuwa wanakabidhi na kadi zao za chama mpaka useme amechangiwa na wanachama?
 
We sema hayo usidhani jamaa ndio atakuwa muungwaana kwa wapinzani.

Zitto alisifiwa lakini angalia kinachompata leo.
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
Hakika leo nimekuona ni mwanasiasa mahiri na uliyeiva haswa
 
Back
Top Bottom