Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Hizi dhana za kuwatukuza viongozi na kuwaona na super beings ndo maaana wanatuibia kila siku . Uongozi ni dhamana tu haumu elevate mtu kuwa above other human beings. Kwenye nchi kama North Korea, China, Rwanda etc huko ndio kuna tamaduni kama hizo za kidikteta Kiongozi anakuwa Mungu wa pili sababu inaeleweka inaongozwa kwenye hiyo misingi ya kidikteta.Sasa nchi yetu ni ya kidemokrasia,,,huu utukufu wa viongozi tunaokuza gafla kwenye Awamu ya tano unatuweka kwenye same periscope na nchi kama Rwanda na North Korea
Kikubwa nilichomwambia The boss, ni kuwa jambo jema tu ndilo huigwa bila kuangalia linatoka nchi gani, na jambo baya halipaswi kuiga hata lifanywe na nchi iliyoendelea. Maneno ya kuudhi, matusi hata umuelekezee mtu wa kawaida asie kiongozi hatoridhika, basi hatakuwa nguvu ya kukufanya chochote, yote kwa yote mimi na wewe hatuwezi jifananisha na hadhi ya viongozi, iwe viongozi wa dini, Siasa na nyanja nyingine.
 
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Mwaka 2013 kundi la kigaidi la ISIS lilipoanza kufanya matukio na baada ya kuona serikali ya marekani inachelewa kuchukua hatua za kijeshi, jamaa mmoja ambae ni mmoja wa malegend wa republican party alimwita Obama "black brained leader" na hakuna prosecution yoyote aliyofanyiwa.
 
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Na tena huyo huyo ndiye anayewaita wananchi wake vi.la.za
 
Kila jamii ina utamaduni wake, kwetu utamaduni wa kutamka tusi ilikuwa unaruhusiwa kwa sharti la kulipoza tusi kabla kutamka kwa kusema
ASHAKUM SI MATUSI
Anyway napita tuu
1466268429836.jpg
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Unapo muheshim mwenzio naw utaheshimiwa, usipo muheshim mtu usidhani kama nawe utakuwa salama kupata heshima.
 
Mwaka 2013 kundi la kigaidi la ISIS lilipoanza kufanya matukio na baada ya kuona serikali ya marekani inachelewa kuchukua hatua za kijeshi, jamaa mmoja ambae ni mmoja wa malegend wa republican party alimwita Obama "black brained leader" na hakuna prosecution yoyote aliyofanyiwa.
sasa Tanzania ni Marekani?
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Daaah!!! Nimeanza kukuunga mkono ulipotoa ushauri kwa Waziri wa Viwanda juu ya kuhamisha General Tyre. Nadhani uendelee kumkumbusha na umpe eneo la kiwanda la wazi. Hiyo ndo siasa ila vijana wengi wa mitandaoni wameshika matusi kama sehemu ya kushindania siasa.

Hoja zina nguvu kuliko tusi maana si wote wanaopenda kejeli na matusi katika ukweli.

Ushauri mzuri sana huu.
 
mitume wanatukanwa mbona haishangazi,huwezi jua sababu za ye kutumia neno hilo ndo maana ye hajakamatwa lile la vilaza
 
Tangu nmeanza kukufatilia post zako na hotuba zako leo ninadiriki kusema kuwa UMEPEVUKA kisiasa,Big up Mbunge wa Arusha
Rudisha to the other side.
Ambaye bado ni nchanga naona umemuanika mwenyewe.
 
Sisi na Rwanda tunaanza kufanana
Si ndipo alipowahi kuchukua formula ya mkoa unakuja kuendeshea nchi yako.
Huu ni ujuha wa hali ya juu, hamna kitu kibaya kama kujidai unajua kila kitu ktk kuongoza nchi
 
Watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba alichokisema Lema ni sahihi kabisa hakuna mtu anayeunga mkono mtu kumtukana Raisi au mtu mwingine .Alichokifanya huyo Kijana Isaac siyo sahihi kabisa watu wengi wanamchangia kwa sababu kumsaidia kuepuka ile adhabu kufungwa miaka 3 jela. Mtukufu hataki hata kukoselewa kabisa hata hoja
 
Mh Lema nimejaribu kufuatilia hotuba zako na michango yako kwenye kwenye bunge hili jipya,unaonekana umekomaa kisiasa kwa kiasi kikubwa tofauti na bunge lililopita.Hongera sana Mh Lema upinzani sio uadui bali ni kutoa mawazo mbadala yatakayo iwezesha serikali kutimiza wajibu wake ipasavyo.
 
Nahisi huyu sio lema atakuwa n lizaboni kwa kutumia jina lengine
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Hukumu si ilishatolewa na mhusika kupatikana na hatia? Anatiwa moyo namna gani tena hadi kuwa makosa..?

Umesahau wakati unaonewa Ubunge wako watu walijitolea hadi uhai wao? (Kama Lema kweli)

Kwamba ukihukumiwa unatakiwa utelekezwe na usisaidiwe kutekeleza hukumu?
 
Back
Top Bottom