Siungi mkono kubadili analogue kwenda digital. Toa maoni yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siungi mkono kubadili analogue kwenda digital. Toa maoni yako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tuko, Apr 5, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kumekuwa na mchakato huu wa TCRA kutaka kusitisha matumizi ya mfumo wa 'kawaida' tunaotumia sasa kwenda mfumo wa digital.
  Japo kuna faida kitaalamu lakini ni wazi kuwa wananchi na wasambaza ving'amuzi wenyewe hawajawa tayari. Wakati madish yanauzwa nchi nzima, ving'amuzi bado haviuzwi nchi nzima. Wakati wapo mafundi wa kufunga na kurekebisha madish nchi nzima, mafundi wa ving'amuzi wanapatikana katika baadhi ya miji tu, tena ni wachache

  Hadi sasa na kwa muda mrefu baadae mwaka huu, wapo watanzania kwa maelfu wanaonunua TV sets na kwa kuwa hawana access na ving'amuzi, wananunua madish. Kama TCRA hawaamini waende kwenye maduka ya madish leo, waone mass ya watu wananunua madish

  Nadhani inahitajika walau miaka miwili tena, angalau hata kampuni za ving'amuzi zijiimarishe.

  Je mwanaJF una maoni gani?
   
 2. zagalo

  zagalo Senior Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  madish yataendelea kufanya kazi. Na ving'amuzi ni kama antena tu haitaji utalaam sana kuunganisha. Na mwisho hata usipounga mkono, ndo ishakua.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Hii transfer toka analogia kwenda digitali, sio choice au option, ni lazima!. Kama simu zilivyohama toka toka analojia kwenda digitali, did we had a choice?.

  Tuko kwenye dunia ya Utandawazi, hivi ni chice sisi Watanzania tuingie kwenye utandawazi?.

  No it was not our choice, huu ni uamuzi wa wenyewe, sisi tunaishia kupangiwa tuu na ITU.
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ok,Ok,Ok,,,
  Nakubali kuwa lazima tutabadilika. Nisichounga mkono ni kufungwa kwa analogue December 2012. Tunahitaji mda zaidi. At Zagalo, kwa sasa ndio tunatumia both madish na ving'amuzi, but by 2013 madish yatakuwa obsolete...
   
 5. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hebu nikuulize unaelimu gani kwanza may be?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Unaonyesha hujaelewa vema mabadiliko haya!
  Hapo kwenye red si kweli, madish hayatakuwa absolete!
  Badiliko la kutoka analojia kwenda digitali haliyahusu madishi...labda kwa lugha nyapesi, madish ni sehemu ya teknolojia ya digitali.
  Mfumo wa digitali uta'affect terrestrial antennas, yaani hii minara ya aridhini, lakini madishi yenyewe yanapokea signal moja kwa moja toka kwenye sattelite hivyo hayataathirika.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  mimi tatizo langu sio muda wala mabadiliko!

  kichefuchefu changu ni kuwa hii digital ni ya wazungu, sio yetu.....wahandisi wetu hawana uwezo wa kuifanya digital iwe yetu..eventually electronics and telecommunication engineers wetu wanabadilika na kuwa REPAIR MAN!!

  kazi ipo, tunapelekwa pelekwa tu
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  mKUU,
  Sasa kuna geni gani hapo?
  Leo hii ndio unaanza kusikitikia na kuona hili kama tatizo?
  Kwani ni teknolojia ipi yoyote ya kidunia ambayo ni yetu Watanzania...au zile mashine za kukamua mafuta ya alizeti na Juisi ya Miwa zinazotengenezwa na wahandisi wa Coet pale Mlimani, na wajasiriamali wa SIDO?
   
 9. PRISCUS JR

  PRISCUS JR JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mfumo huu ni mzuri ila ni unyonyaji mpya uliokurupukiwa na TCRA, ntarudi baadae nifafanue wizi huo.
   
 10. S

  Saskatchewan Senior Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Siku zote sisi masikini ndo waathirika wakubwa na haya mabadiliko ya teknolojia! Kununua televisheni peke yake ilikuwa kazi, kununua king'amuzi na kukilipia kila mwezi itawezekana kweli! Sidhani kama sisi maskini tutamudu gharama. Kwa wale wenye uwezo wenyewe haitakuwa tatizo sana! Inabidi turudi miaka ya tisini kununua mikanda ya filamu na kuangalia sababu tv channels za bure hazitakuwepo. Umaskini mbaya sana!
   
 11. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Naomba uliza na sisi wa huku mtimbira tusio hata na radio tutaathirika?
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kumbe jambo hili la digitali halijaeleweka na wengi...timu yetu ya elimu kwa jamii inabidi iweke mikakati mizito zaidi pale Morogoro itakapokutana soon mwezi huu!
  jAMANI, STATIONS AMBAZO ZINAONEKANA free to Air sasa hivi, bado zitaendelea kuonekana free hata kwa kingamuzi...
  Ni mtu yule anayetaka complications za MICHEZO, SINEMA NA MIZIKI YA KILEO ndiye atalazimika kulipia vituo hivyo, yaani ni kama ilivyo sasa!
  Gharama atakayoingia mtu ni ndogo tu ya kawaida ya Tshs 59,000 tu, ambapo ni sawa na kumiliki simu ya tochi, ambapo pia kila Mtanzania ana uwezo huo kwa sasa.
  Kama kuna maswali ulizeni!
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wakuu tunaweza kukaa na kukubaliana kwamba muda uongezwe! Well but others are migrating! Kama Wenzetu wakitangulia hauoni kwamba Tanzania ina hatari ya kugeuzwa Jalala la Vifaa vya Analojia? Think of it Mkuu
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mi mradi tv ionyeshe
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Hii digital migration ina faida nyingi kuliko hasara, hivi vituo vyetu vya TV vyote vinageuka production houses kwa kuprovide contents tuu!. Ule ukiritimba wa kuitegemea sijui TBC au ITV kutudengulia kurusha vipindi vyetu ndio unamalizika rasmi!.

  Mfano Chadema hawahitaji kuwa kituo cha TV kurusha matangazo yake, kinalipia tuu chaneli kwa hao multiplex providers na kwenda hewani!.

  Hata mimi na vile vipindi vyangu vya "Wiki ya Utumishi wa Umma na PPR", "Saba Saba na PPR " na " Nane Nane na PPR" sina haja ya kuwanyenyekea tena hao wenye TV zao!, nalipia chaneli nakwenda hewani!.

  Mfano kila Jumapili asubuhi karibu kila dhehebu litakuwa hewani kwenye ibada

  Chan 1 Katoliki
  Chan 2 Kakobe
  Chan 3 Rwakatare
  Chan 4 Walutheri
  Chan 5 Waangalikana
  Chan 6 Pentecoste
  Chan 7 Menonite
  Chan 8 Mzee wa Upako
  Chan 9 Mwakasege
  etc, etc

  Wigo wa chaguo la nini cha kuangalia linakuwa kubwa zaidi

  Tatizo kwangu ni moja tuu, nitalazimika kuwa na ving'amuzi vingi zaidi!, saa hizi niko na DSTV kwa ajili ya African Magic, Niko na Star Time kwa ajili ya TBC-1, Agape kwa ajili ya HBO sasa kuna Zuku hicho cha ITV na star kinakuja, hapo sijakihesabu hiki cha Easy TV cha mchina etc!.
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nonsense...
  Elimu yangu haihusiani na usumbufu wowote kama mtanzania nitakaoupata...
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Duh.. Mkuu sasa hapa ndo nazidi kuchanganyikiwa, but usichoke kunielimisha. Unaposema madish yataendelea kutumika, najiuliza mambo yafuatayo
  a. Kulikuwa na haja gani ya kuleta na kuongelea ving'amuzi?
  b. DSTV wana dish, ving'amuzi hawana dish, kuna tofauti gani kati ya technologia inayotumika na DSTV ukilinganisha na hii inayotumika na alina Star times?
  c. Kuna watu wanaongelea kurekodi vipindi, kuwa na channels nyingi katika frequency moja, ina maana haya yote yanawezekana katika technologia ya dish?

  Ntashukuru ukinijibu hayo machache...
   
 18. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mkuu PJ ni kweli halijaeleweka kwa wananchi wa kawaida. Wasiwasi wangu ni kuwa complications zake hazijaeleweka hata kwa mamlaka husika ikiwemo TCRA. Naomba unifafanulie mambo yafuatayo
  a. Hadi wakati huu ninapoandika hapa, kuna maeneo chungu nzima ya nchi yetu ambapo hivi ving'amuzi havipo. Ni kwa nini?
  b. Kwa yale maeneo ambayo kwa sasa hamna dealers wa ving'amuzi, wananchi wananunua TVs za kawaida, kukata shauku yao ya mahitaji ya TV. Je, ni halali imlazimu mtu leo kununua technologia iliyopo maeneo yake, kisha miezi saba baadae unamwambia imepitwa na wakati? Je, haikuwa muafaka kwa serikali kusubiri hadi dealers wa ving'amuzi watakapoenea nchi nzima ndipo waanze kuahmasisha wateja kuhamia huko?
  c. Nilimsikia mtaalamu fulani akisema matangazo ya digital yanasambazwa kupitia mkongo wa taifa. Hiyo inamaanisha nini kwa maeneo ambayo mkongo haujafika kwa sasa?

  d. Mkuu hii nchi sio Dar na labda Arusha peke yake. Kuunganishiwa king'amuzi cha Ting hapa moro ni Tsh 320,000, Zuku zaidi la laki 2 na hizi ni bei za mawakala wanaotambuliwa...

  Ntashukuru ukinijibu baadae...
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  @Pasco.
  Hili tatizo la vingamuzi vingi litapungua taratibu! With time teknolojia itaruhusu kuwa na kingamuzi kimoja tu, ambapo kazi yako itakuwa ni kuwa na SmartCards za makampuni mengi utakavyo, na utakaa kwenye kochi ukiwa unahama toka s/card ya Startimes kwenda ya Ting etc, bila kunyenyuka, ukitumia remote ctrl. Hilo liko just on transit, tuwe patient.
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  @Tuko, niko via mobile, na maswali yako ni marefu, nitayajibu nikiwa kwny laptop,
   
Loading...