Siungi mkono kubadili analogue kwenda digital. Toa maoni yako

Kumbe jambo hili la digitali halijaeleweka na wengi...timu yetu ya elimu kwa jamii inabidi iweke mikakati mizito zaidi pale Morogoro itakapokutana soon mwezi huu!
jAMANI, STATIONS AMBAZO ZINAONEKANA free to Air sasa hivi, bado zitaendelea kuonekana free hata kwa kingamuzi...
Ni mtu yule anayetaka complications za MICHEZO, SINEMA NA MIZIKI YA KILEO ndiye atalazimika kulipia vituo hivyo, yaani ni kama ilivyo sasa!
Gharama atakayoingia mtu ni ndogo tu ya kawaida ya Tshs 59,000 tu, ambapo ni sawa na kumiliki simu ya tochi, ambapo pia kila Mtanzania ana uwezo huo kwa sasa.
Kama kuna maswali ulizeni!

Una hakika hizi receiver zinaonesha local channels free ?

Chukua mfano staaTymz imepungukiwa na baadhi ya channels za locals ambazo zinapatikana bure!

Fafanua hayo kwanzo ili uturidhishe na hii transition ya digital huenda tukaipokea vyema

-
 
Duh.. Mkuu sasa hapa ndo nazidi kuchanganyikiwa, but usichoke kunielimisha. Unaposema madish yataendelea kutumika, najiuliza mambo yafuatayo
a. Kulikuwa na haja gani ya kuleta na kuongelea ving'amuzi?
b. DSTV wana dish, ving'amuzi hawana dish, kuna tofauti gani kati ya technologia inayotumika na DSTV ukilinganisha na hii inayotumika na alina Star times?
c. Kuna watu wanaongelea kurekodi vipindi, kuwa na channels nyingi katika frequency moja, ina maana haya yote yanawezekana katika technologia ya dish?
Ntashukuru ukinijibu hayo machache...
Mkuu,
Nitakujibu kifupi!
(a)Kwa uelewa wangu, Dish ni teknolojia kama ya kati(middle) kati ya hii ya minara na digital. kama umetumia dish utagundua kuwa kuna wakati linapoteza signal au kuanza ku'scratch na hatimaye kutokamata kabisa!..Setting ya Free to Air Dish inataka manual keenness sana, na kila baada ya muda utalazimika kumwita fundi aje kureset ili uendelee kukamata stations!...Teknolojia ya vingamuzi bila shaka unaijua, iko makini, haina scratches, picha zake ni makini kabisa.
(b)Dish la Dstv linasetiwa kwa kuelekeza kwenye Sattelite, na hivyo shida zake ni kama hapo juu(a)..Mkuu, kingamuzi unajua mambo yake...ni kipini tu kinagandishwa hata kwenye friji chumbani...basi mkubwa unakula ma'National Geographic, eTV, KBC, na madude yaliyosoma!
(c)Kwenye disha la Free to Air hakuna uwezekano huo.
 
Pia inarahisisha utawala.
 
mKUU,
Sasa kuna geni gani hapo?
Leo hii ndio unaanza kusikitikia na kuona hili kama tatizo?
Kwani ni teknolojia ipi yoyote ya kidunia ambayo ni yetu Watanzania...au zile mashine za kukamua mafuta ya alizeti na Juisi ya Miwa zinazotengenezwa na wahandisi wa Coet pale Mlimani, na wajasiriamali wa SIDO?

sijaanza kusikitika leo mkuu!
 
Mkuu PJ ni kweli halijaeleweka kwa wananchi wa kawaida. Wasiwasi wangu ni kuwa complications zake hazijaeleweka hata kwa mamlaka husika ikiwemo TCRA. Naomba unifafanulie mambo yafuatayo
a. Hadi wakati huu ninapoandika hapa, kuna maeneo chungu nzima ya nchi yetu ambapo hivi ving'amuzi havipo. Ni kwa nini?
b. Kwa yale maeneo ambayo kwa sasa hamna dealers wa ving'amuzi, wananchi wananunua TVs za kawaida, kukata shauku yao ya mahitaji ya TV. Je, ni halali imlazimu mtu leo kununua technologia iliyopo maeneo yake, kisha miezi saba baadae unamwambia imepitwa na wakati? Je, haikuwa muafaka kwa serikali kusubiri hadi dealers wa ving'amuzi watakapoenea nchi nzima ndipo waanze kuahmasisha wateja kuhamia huko?
c. Nilimsikia mtaalamu fulani akisema matangazo ya digital yanasambazwa kupitia mkongo wa taifa. Hiyo inamaanisha nini kwa maeneo ambayo mkongo haujafika kwa sasa?

d. Mkuu hii nchi sio Dar na labda Arusha peke yake. Kuunganishiwa king'amuzi cha Ting hapa moro ni Tsh 320,000, Zuku zaidi la laki 2 na hizi ni bei za mawakala wanaotambuliwa...
Ntashukuru ukinijibu baadae...
Mkuu Tuko,
(a)Mkuu, labda nikushangaze kuwa sasa hvi tunapoongea, TV zilizpo nchini ziko katika 24% ya eneo la nchi, baada ya miaka yote hiyo ya kuja kwa TVs nchini:shock:...can u imagine?
Na pia nikushangaze kuwa hadi sasa muundombinu wa digitali umeshaenea nchini kwa 20%!..hivyo unatakiwa upongeze sana juhudi za kuhamia digitali, maana katika muda mfupi sana wamejenga muundombinu wa kiasi hicho!
Jiulize hadi mwisho wa December watakuwa wamefikia percent ngapi ya nchi kama si kote?

(b)Shida nyingine ya watu wengi ni kushindwa kujua kuwa TV compatible kwa mfumo wa Digitali ni ipi!..kuna wengine wanasema na kudanganya wenzao kuwa tv zote zenye tumbo au mgongo, ni za analojia...No! No
! No!
Tv karibu zote zinazouzwa sasa hivi madukani ni compatible na Digital. TV yoyote yenye zile pins mbili na kuendelea, inayoweza kuchomekwa AV cable hiyo inafaa kupokea teknoloji ya Digitali.
Zile TV za kizamani za kuchomeka waya wa kutoka kwenye Dish au antenna ya chadema , na hazina AV pins hazitafaa, sasa sijui kama kuna maduka yanauza TV za hivo kwa sasa!

(c)Mkuu,
Muundombinu huu wa digitali hakika unategemea internet, na kama ujuavyo mkongo uko kwenye kasi kubwa ya kusambaa nchini!

(d) Mkuu, suala la bei ni function ya muda, NA PIA programs zilizopo katika Smartcard/package husika!..Umesahau kuwa Line ya Mobitel enzi hizo ilikuwa ikiuzwa kwa Tshs 100K?...Sasa hivi wengi wanagawa Bure..hiyo isikupe homa ya vipindi!
mBONA Star Times wanauza kwa Tshs 59K?...
 
Una hakika hizi receiver zinaonesha local channels free ?

Chukua mfano staaTymz imepungukiwa na baadhi ya channels za locals ambazo zinapatikana bure!

Fafanua hayo kwanzo ili uturidhishe na hii transition ya digital huenda tukaipokea vyema
-
Star Times wanaonyesha TBC1 freely kama Local channel...unasemaje?
 
Kumbe jambo hili la digitali halijaeleweka na wengi...timu yetu ya elimu kwa jamii inabidi iweke mikakati mizito zaidi pale Morogoro itakapokutana soon mwezi huu!
jAMANI, STATIONS AMBAZO ZINAONEKANA free to Air sasa hivi, bado zitaendelea kuonekana free hata kwa kingamuzi...
Ni mtu yule anayetaka complications za MICHEZO, SINEMA NA MIZIKI YA KILEO ndiye atalazimika kulipia vituo hivyo, yaani ni kama ilivyo sasa!
Gharama atakayoingia mtu ni ndogo tu ya kawaida ya Tshs 59,000 tu, ambapo ni sawa na kumiliki simu ya tochi, ambapo pia kila Mtanzania ana uwezo huo kwa sasa.
Kama kuna maswali ulizeni!
Nadhani ww ndo hujaelewa mkuu PJ! Kuna watu wenye ving'amuzi lakini hizo local channels zote hazionekani! Unasemaje local channels zitaonekana? Halafu umasikini uko pale pale sio watanzania wote wana uwezo wa kununua ving'amuzi sababu ww unaona unaweza ndo maana unafikiri wote wanaeza! Labda inawezekana hujui kama kuna watanzania wengi wanaoishi chini ya dola moja! Jipange
 
Mkuu umekuja na jambo zuri kujadili ingawa kwa kwetu Tanzania bado asilimia kubwa ya watu wataathirika kwa kukosa analog signal.

Kubadili Analog signal kwenda Digital ndio mahitaji ya huko mbele kwani zile channels zote ambazo hupatikana bure zitaweza kuonekana kwa uzuri zaidi na more clear.

Kama unavyofahamu kwa sasa TV sets nyingi zinakuwa na chenga na watu wanakwanda hivyohivyo mradi kuna news na angalu msomaji au picha za matukionhata kama hakuna clear view.

Digital TV signal inatumia nafasi ndogo ya kurusha matangazo (less broadcast space) hivyo kutoa mwanya kwa channels nyingi kuonekana kama alivyooanisha mmoja wa wachangiaji hapo juu, tena nyingine zitaja na muonekano wa ndani zaidi -High Definition.

Nafikiri kitakachotakiwa kwa raia wa kawaida na wale wenye uwezo ni kuanza kupanga budget ya kununua seti za televisheni ambazo ni za kisasa zaidi ambazo zingine zimeundiwa digital signal ili kupokea digital channels yaani -Freeview built in, na kuanza taratibu za kuachana na telerestial TVs.

Kuhusu serikali kupitia hao TCRA wanaangalia namna ya kupata mtambo au mitambo ya kuvuna digital channels hizo na kuzisambaza kwa wananchi kwani ni lazima pawe na kituo cha kurushia matangazo ambacho ndio central ya kila kitu.

Ila bila shaka kuingia katika ulimwengu wa digital kuna faida nyingi zikiwemo ya hiyo kupata channels lukuki, kupata features (kama zipo) za audio description na subtitlings kwa wale wasio na uwezo wa kusikia na kuona.
 
Kutoka analog sys kwenda Digital sys ya kutumia Ving'amuzi ni moja wapo ya wizi usiotumia silaha ....
 
kila jambo lina gharama yake. Mfumo wa digital una faida zake nyingi, so lets accept gharama zake,but baadae tutaona faida zake. kama wadau walivyo-comment, matumizi ya madishi ndo part ya digital so haitaathiri sana watu wa mikoani kwakua wengi tayari wanatumia madishi.wanaoathirika sana ni wakazi wa mijini ambao wamezoea kutumia antena. lakini we unataka watu wapewe miaka mingapi ya maandalizi ya kununua king'amuzi cha chini ya laki moja au dishi la laki 2?
Kumekuwa na mchakato huu wa TCRA kutaka kusitisha matumizi ya mfumo wa 'kawaida' tunaotumia sasa kwenda mfumo wa digital.
Japo kuna faida kitaalamu lakini ni wazi kuwa wananchi na wasambaza ving'amuzi wenyewe hawajawa tayari. Wakati madish yanauzwa nchi nzima, ving'amuzi bado haviuzwi nchi nzima. Wakati wapo mafundi wa kufunga na kurekebisha madish nchi nzima, mafundi wa ving'amuzi wanapatikana katika baadhi ya miji tu, tena ni wachache

Hadi sasa na kwa muda mrefu baadae mwaka huu, wapo watanzania kwa maelfu wanaonunua TV sets na kwa kuwa hawana access na ving'amuzi, wananunua madish. Kama TCRA hawaamini waende kwenye maduka ya madish leo, waone mass ya watu wananunua madish

Nadhani inahitajika walau miaka miwili tena, angalau hata kampuni za ving'amuzi zijiimarishe.

Je mwanaJF una maoni gani?
 
Hii digital migration ina faida nyingi kuliko hasara, hivi vituo vyetu vya TV vyote vinageuka production houses kwa kuprovide contents tuu!. Ule ukiritimba wa kuitegemea sijui TBC au ITV kutudengulia kurusha vipindi vyetu ndio unamalizika rasmi!.

Mfano Chadema hawahitaji kuwa kituo cha TV kurusha matangazo yake, kinalipia tuu chaneli kwa hao multiplex providers na kwenda hewani!.

Hata mimi na vile vipindi vyangu vya "Wiki ya Utumishi wa Umma na PPR", "Saba Saba na PPR " na " Nane Nane na PPR" sina haja ya kuwanyenyekea tena hao wenye TV zao!, nalipia chaneli nakwenda hewani!.

Mfano kila Jumapili asubuhi karibu kila dhehebu litakuwa hewani kwenye ibada

Chan 1 Katoliki
Chan 2 Kakobe
Chan 3 Rwakatare
Chan 4 Walutheri
Chan 5 Waangalikana
Chan 6 Pentecoste
Chan 7 Menonite
Chan 8 Mzee wa Upako
Chan 9 Mwakasege
etc, etc

Wigo wa chaguo la nini cha kuangalia linakuwa kubwa zaidi

Tatizo kwangu ni moja tuu, nitalazimika kuwa na ving'amuzi vingi zaidi!, saa hizi niko na DSTV kwa ajili ya African Magic, Niko na Star Time kwa ajili ya TBC-1, Agape kwa ajili ya HBO sasa kuna Zuku hicho cha ITV na star kinakuja, hapo sijakihesabu hiki cha Easy TV cha mchina etc!.
Wanabodi,

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA leo imetoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa digital na kueleza kuwa huna haja ya kuwa na king'amuzi zaidi ya kimoja na wenye TV za migongo wasiwe na wasiwasi tutaingia mfumo wa digitali na TV zao hizo hizo!.

Ufafanuzi huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa TCRA Bw. Innocent Mungy alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa live la TBC-1.

Bw. Mungy amesema matangazo yote yatarushwa na makampuni matatu yanayoitwa Multiplex Operators ambao ni Star Media, Agape Associates na kampuni nyingine moja, ila ili kuziona chanel za bure ambazo ni free to air kama ITV, TBC, Channel Ten, Star TV etc, sio lazima kuwa na ving'amuzi vitatu, kingamuzi kimoja tuu kinatosha na TV zote za bure zitapatikana humo!.

Ufafanuzi huu umemaliza rasmi ile simtofahamu ya wasiwasi wa watu kuzitupa TV zao za migongo au kulazimika kufunga ving'amuzi zaidi ya kimoja!.

Huyu Bw. Mungy wa TCRA, anastahili pongezi kwa kutoa ufafanuzi murua. Hongera Innocent Mungy!.

Pasco.
madish yanayoendelea kutumika ni yale ya digital tuu, kama CU-Band, au Dstv etc, yale ya kulipia, haya madishi ya kawaida yanayoitwa nyungo, mwisho wa biashara ni 31/12/2012. Kuanzia 01/01/2013 ni mwendo wa vingamuzi tuu!, kwani hujafika ulaya?, umeona madish?!. Kuanzia mwakani Tanzania ni kama ulaya!

Kwa vile mimi sio mtu wa TCRA, nakushauri, fuatilia kipindi ili kupata uhakika zaidi!.

kazi kwelikweli, maswali ya TRUE na FALSE kupata na kukosa ni fiftefifte
 
lakini jamani katika hali,ya kawaida hii transition ijaribu kumuangalia mtu wa chini kabisa ambae maisha yake ni ya kubangaiza na hana pato lilokuwa rasmi ie mshahara au ndio wale wa kima cha chini na majukumu chungu mbovu.
how does such a person stay in touch with global events in the aspect of news? kwani taarifa ya habari ni basic right ya karibia kila mwananchi au ndio tubakie kusikiliza maredioni tu? au ndio turudi zama zile za kuangalia mikanda? TCRA ijaribu kuevaluate ni raia wangapi wataweza kuafford hii kitu?
 
Unanidai Double LiKe

lakini jamani katika hali,ya kawaida hii transition ijaribu kumuangalia mtu wa chini kabisa ambae maisha yake ni ya kubangaiza na hana pato lilokuwa rasmi ie mshahara au ndio wale wa kima cha chini na majukumu chungu mbovu.
how does such a person stay in touch with global events in the aspect of news? kwani taarifa ya habari ni basic right ya karibia kila mwananchi au ndio tubakie kusikiliza maredioni tu? au ndio turudi zama zile za kuangalia mikanda? TCRA ijaribu kuevaluate ni raia wangapi wataweza kuafford hii kitu?
 
Hii digital migration ina faida nyingi kuliko hasara, hivi vituo vyetu vya TV vyote vinageuka production houses kwa kuprovide contents tuu!. Ule ukiritimba wa kuitegemea sijui TBC au ITV kutudengulia kurusha vipindi vyetu ndio unamalizika rasmi!.

Mfano Chadema hawahitaji kuwa kituo cha TV kurusha matangazo yake, kinalipia tuu chaneli kwa hao multiplex providers na kwenda hewani!.

Hata mimi na vile vipindi vyangu vya "Wiki ya Utumishi wa Umma na PPR", "Saba Saba na PPR " na " Nane Nane na PPR" sina haja ya kuwanyenyekea tena hao wenye TV zao!, nalipia chaneli nakwenda hewani!.

Mfano kila Jumapili asubuhi karibu kila dhehebu litakuwa hewani kwenye ibada

Chan 1 Katoliki
Chan 2 Kakobe
Chan 3 Rwakatare
Chan 4 Walutheri
Chan 5 Waangalikana
Chan 6 Pentecoste
Chan 7 Menonite
Chan 8 Mzee wa Upako
Chan 9 Mwakasege
etc, etc

Wigo wa chaguo la nini cha kuangalia linakuwa kubwa zaidi

Tatizo kwangu ni moja tuu, nitalazimika kuwa na ving'amuzi vingi zaidi!, saa hizi niko na DSTV kwa ajili ya African Magic, Niko na Star Time kwa ajili ya TBC-1, Agape kwa ajili ya HBO sasa kuna Zuku hicho cha ITV na star kinakuja, hapo sijakihesabu hiki cha Easy TV cha mchina etc!.

Ala, kumbeee!!
I can see the greatest and potential business opportunity is coming on our way….Kwahiyo mkuu unachotaka kuniambia ni kwamba with some $$$ I can have NasDaz Channel?! Kama hivyo ndivyo, then I want that transformation to be effective now…not even tomorrow!! Let me google for more infos on this ili niwe well prepared!
 
Nadhani ww ndo hujaelewa mkuu PJ! Kuna watu wenye ving'amuzi lakini hizo local channels zote hazionekani! Unasemaje local channels zitaonekana? Halafu umasikini uko pale pale sio watanzania wote wana uwezo wa kununua ving'amuzi sababu ww unaona unaweza ndo maana unafikiri wote wanaeza! Labda inawezekana hujui kama kuna watanzania wengi wanaoishi chini ya dola moja! Jipange

Hapo kwenye red....
Je, hizo local channels zote unazotaja zipo kwenye digital tayari?!
 
Wakuu Naomba Nichangie Kidogo Kwenye Hii Mada japo niliianzishia Uzi Na Nikaomba Mod waufanye kuwa Sticky Lakini Naona wana Mambo mengi sana. Ukitaka Kupata Maelezo yangu Mengi basi tembelea link

https://www.jamiiforums.com/tech-ga...zaji-wa-digital-maswali-na-majibu-muhimu.html

1. Niweke Wazi Kabisa kwamba Kuhamia Mfumo wa Utangazi wa Digital kwa kutumia Mitambo iliyoko Ardhini ( Earth Based Transmmiters) si Takwa la TCRA bali ni Dunia nzima. Kwa hiyo tujiandae Kuupokea huo Mfumo una Faida nyingi sana nitakwenda kuzielezea.

2. Mfumo wowote wa Mawasiliano hutumia Njia zifuatazo Kupeleta Taarifa kwa Watumiaji

a. Kwa Kutumia Mitambo iliyoko kwenye Satelite ( Satelite base transmitters)

b. Kwa Kutumia Mitambo iliyoko Ardhini ( Terestrial Communication System) Earth based Transmitters

b. Kwa Kutumia Cable

3. Broadcasting ni Moja kati ya Mifumo ya Mawasiliano kama ilivyo Simu n.k ambao hutumia Satelite, Cable ama Masafa ya Mitambo iliyoko ardhini kufikisha Matangazo.

4. Kwa miaka mingi sasa Mufumo wa Urushaji wa matangazo kwa Njia ya Satelite na Cable umekuwa Digitized lakini Mfumo wa Urushaji wa Matangazo kwa Kutumia Mitambo iliyoko Ardhini imeendelea kuwa ya Analojia.

5. Sasa Dunia imeamu kwamba Mfumo wa Urushaji wa Matangazo kwa Kutumia Mitambo ya Ardhini nayo ibadilishwe kuwa Digital ( Faida za Digital ni nyingi sana)

6. Kwa Hiyo kilichopo sasa ni Ubadilishaji wa Mfumo wa Utangaziji uliopo sasa na kuwa wa Digitali

Labda niweke Sammary

1. Mabadiliko haya hayawahusu watumia wa Madishi.

2. Wenye TV za Chogo au Tumbo au CRT wataendelea kutumia TV zao kwa miaka mingi sana ijayo ila watatakiwa kuwa na King'amuzi ili waweze kuona matangazo ya Dijitali ( Kama ilivyo kwa watumiaji wa Madish ni lazima uwe ni King'amuzi)

3. Mabadiliko haya ni Muhimu sana na kwa jinsi nilivyofuatilia Maelezo ya watu wa TCRA yana fursa nyingi sana maana Channel capacity imeongezeka maana tulikuwa tukienda TCRA kuomba leseni ya TV tunaambiwa kwamba Masafa yameisha kwa Dar Es Salaam but with Digita Masafa sasa yanatafuta Watumiaji

4. Watu waache kupotosha kwamba wenye TV za Chogo wazitupe

Niite Polo
 
lakini jamani katika hali,ya kawaida hii transition ijaribu kumuangalia mtu wa chini kabisa ambae maisha yake ni ya kubangaiza na hana pato lilokuwa rasmi ie mshahara au ndio wale wa kima cha chini na majukumu chungu mbovu.
how does such a person stay in touch with global events in the aspect of news? kwani taarifa ya habari ni basic right ya karibia kila mwananchi au ndio tubakie kusikiliza maredioni tu? au ndio turudi zama zile za kuangalia mikanda? TCRA ijaribu kuevaluate ni raia wangapi wataweza kuafford hii kitu?

Kwani unafikiri King'amuzi ni shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom