DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 944
- 1,253
Katiba mpya imekuwa ni mjadala baada ya makundi mbali mbali ya watu yakitaka ule mchakato uliositishwa wa mabadiliko ya katiba uanze upya kwa kuanzia kwenye rasimu ya Jaji Warioba.
Mimi ni mmoja ya watanzania wanaotamani kuona kama taifa tunapata Katiba mpya inayotokana na maoni ya Watanzania (wenye nchi) yenye kukidhi matarajio, malengo na kasi ya maendeleo tuyatakayo.
Makundi mengi yamejitokeza kujadili na kusisitiza mahitaji ya katiba mpya ikiwemo vyama vya siasa. Hoja yangu ni juu ya CHADEMA kujiinua katika hili swala la kudai Katiba mpya na hizi ni sababu zangu kwanini siungi mkono CHADEMA kuinjinia mjadala wa katiba mpya.
KATIBA NI YA WANANCHI SI YA VYAMA VYA SIASA.
CHADEMA ni chama cha kisiasa na kwasaabu hiyo hakina sifa za kudi katiba mpya kwasababu kufanya hivyo kutaifanya katiba hiyo ionekane kuwa ni takwa la kisiasa na hivyo kuwakosesha wananchi ambao ndio hasa walengwa wa katiba kukosa nguvu kwenye mjadala mzima na kumwezwa na wanasiasa hasa wa upinzani.
Kama CHADEMA wanaamini kwamba ni wajibu wao na wana haki ya kudai katiba mpya basi CCM wako sahii na waha haki na wajibu wa kukataa Katiba mpya. maana wote ni wanasiasa na wana haki sawa linapokuja suala la kutoa maoni.
MADAI YAO HAYATAZINGATIA WANANCHI BALI WANASIASA.
Kwa miaka 5 mfululizo CHADEMA na vyama vingine vya siasa vya upinzani vimepitia kipindi kigumu kuwahi kushuhudiwa kwenye historia ya vyama vingi Tanzania, kwahiyo basi kama CHADEMA ndio watakaoinjinia huu mjadala wa Katiba mpya vitu pekee ambacho vitakuwa vipaumbele kwenye mijadala yao itakuwa ni siasa kama tume huru ya uchaguzi, uhuru wa kufanya mikutano, uhuru wa kutoa maoni, haki za kisiasa, haki za watu kukusanyika ndani ya nchi na hivyo kuondoa dhana nzima ya katiba ya wananchi ambayo intakaiwa kugusa makundi yote kwenye jamii.
KUTAWATENGA WASIO NA VYAMA AU WASIOPENDA SIASA YA UPINZANI.
Kuna kndi kubwa la watanzania amabao hawapendezwi na siasa au siasa za upinzani, kama chama cha siasa ndio kitainjinia mjadala wa katiba hii sehemu kubwa ya watu itaachwa katika hili la katiba na kufanya mjadala uonekane ni kwa maslahi ya kisiasa pekee.
Nashauri CHADEMA na vyama vingine vya siasa wasiinjinie mchakato wa kutaka katia mpya na kama wanashiriki washiriki kwa kualikwa tena kwa kuzingatia kuwa CCM nao wapo kwenye huo mjadala ili kuleta balansi ya hoja kwenye mijadala.