Maoni: Serikali itumie njia hii kudhibiti ukwepaji kodi.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,602
Kwanza, Ninampongeza Waziri mkuu kwa kutatua mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo uliodumu kwa siku 3 mfufulizo. Katikati ya mgomo huo mpaka kutatuliwa kwake tumeona na kusikia mengi hususani madhila waliyokuwa wanakutana nayo wafanyabiashara kutoka kwenye vikosi kazi vya kodi.

Pamoja na mambo mengine, licha ya baadhi ya wafanyabiashara kuonewa lakini kuna wengine ni wakwepaji kodi. Na hapa ndio kwenye msingi wa hoja yangu KUDHIBITI UKWEPAJI KODI.

Kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lolote duniani hivyo ni jukumu la walipakodi kulipa kodi kulingana na Sheria na taratibu zilizopo. Na hapa ndio panahitajika uwepo wa vidhibiti ili kudhibiti ukwepaji Kodi.

Na haya ndio maoni yangu:

Moja, Kwa kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanaagiza bidhaa zao kutoka nje ya nchi au kutoka viwanda vinavyotengeneza hapa nchini serikali itengeneze " inventory management system" ambayo itafungamanishwa na mfumo wa EFD.

Nikiwa na maana ya kwamba ' importer' wakiagiza bidhaa kutoka nje ya nchi huo mfumo utatumika kufatilia ' inventory' ya huo mzigo kutoka kwa muagizaji mpaka kwa mlaji wa mwisho. Vivyo hivyo kwa bidhaa zinazozalishwa nchini mfumo ufanye udhibiti kutoka kwa mzalishaji mpaka kwa mlaji wa mwisho.

Tukianza kwa 'importer' au muagizaji ,mfumo ufanyaje kazi?

Kwanza, Serikali kwanza idhibiti mianya yote ya kuingizia bidhaa kimagendo kutoka nje na bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nje zipitie kwenye mfumo wa forodha iwe bandarini au mipakani. Na hapo kwenye forodha bidhaa zote zisajiliwe na ziingizwe kwenye mfumo wa EFD wa muagizaji. Kwa mfano, vimeagizwa vitenge vitenge 5000 kutoka nje, vitenge hivyo viingizwe wenye mfumo wa EFD wa muagizaji kwamba vitenge hivyo ndio vinakuwa Stock yake mpya. Kama huyo muagizaji akitaka kuuza labda vitenge 200 kwa mteja A ,kupitia kwenye mfumo wa EFD atapunguza vitenge 200 na kubaki 4800 na hivyo 200 atasajili kwenye mfumo wa EFD wa huyo mteja huo.

Mteja A akitaka kuuza vitenge 20 kwenda kwa mteja B atapunguza stock kwa 20 na kubakiwa na 180.

Vivyo, kwa mzalishaji kwenye kila kiwanda kikubwa na vya kati wawepo maafisa wa TRA na hao kazi yao ni kuwasajili wafanyabiashara wanaonunua bidhaa moja kwa moja kwa mzalishaji na hapa tumuite mteja ambaye pia ataingiza kwa mteja B na process itaendelea hivyo mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

Pili, ili hili liwe maana wafanyabiashara wote wawe na mashine za EFD isipokuwa kwa wale tu ambao wanatambuliwa kama machinga na machinga wote wawepo kwenye maeneo waliyopangiwa. Machinga yoyote anayefanya biashara mbele ya duka la mtu aliyesajiliwa kwenye mfumo naye ni lazima atoe risit za EFD kama wenzake.

Tatu, badala ya kuhusisha task force na mengineyo TRA ijikite kwenye kaguzi za kushtukiza kwenye maduka au waajiri kampuni za ukaguzi wa mahesabu kuwasaidia kufanya kazi wanapohisi pana ubadhirifu. Kwa kuwa stock zitakuwa zimesajiliwa kwenye mfumo itakuwa ni rahisi kujua ubadhirifu.

Faida za uwepo wa INVENTORY MANAGEMENT SYSTEM

Kwanza, kutakuwa na udhibiti mzuri wa stock utakaowezesha kufanya makadirio sahihi ya Kodi. Kupitia kwenye mfumo TRA itajua ni mzigo kiasi gani mfanyabiashara alioingiza, kiasi gani alichouza na kwa kiasi gani alichouza na kilichobaki ni kipi kwa hiyo itawezesha kufanya physical stock taking kwa urahisi na kujua udanganyifu.

Pili, Mfumo utarahisha ufanyaji kazi wa TRA na kuweka kwa uwazi mkubwa shughuli za wafanyabiashara na walipakodi

Wanasema namba hazidanganyi, mfumo huu utapunguza udanganyifu kwa kiwango kikubwa na matukio ya kupika stock ili kulipa kodi pungufu yatapungua.

Tatu, mfumo huo utatumika kama mbadala wa usajiri wa stoo kwa sababu imezoeleka wafanyabiashara kutumia stoo Kama kichaka Cha kutoa bidhaa bila risiti hivyo kwa kuwa mfumo huu utasaidia kujua inventory nzima ya mfanyabiashara tafsiri yake tutaijua tu stoo kwa sababu kwenye physical stock taking stoo pia itaoneshwa.

Ni hayo tu kwa leo
 
Mkuu, rudi field ukaone na kujifunza ukweli na uhalisia ndipo utoe ushauri.

Kwa sasa baki na huo ushauri wako, it's too academic.

Kwa ufupi matatizo makubwa ni:'-

1. Utitiri wa kodi/tozo nk

2. Viwango (rates) ni vikubwa

3. Retrospective ni sheria haramu

4. Mazingira ya biashara na uwekezaji yaboreshwe.

5. Serikali iache uonevu wa kuchuma isikopanda. Ijifunze kuwekeza mfano elimu, masoko na mitaji sio kukwapua, kufilisi, kutaifisha kama sasa.
 
Dawa ni kupunguza utititri wa kodi.
Kodi za dhuluma na za kubambikiwa hapo sawa nakubaliana nawe zifutwe.

Jambo hili yawezekana wengi wakawa hawajuhi. Kuna jedwali fulani la Kodi ya ya kuagiza bidhaa nje na jumla ikawa Kama 62.5% kama sikosei.

Huu ndio ukweli, wengi wa wanaoagiza mzigo nje wanaagiza "in bulk" . Jaribu kupitia Alibaba, eBay na kwingineko uone faida za bulk. Kwa mfano ingia Alibaba uone mwenyewe, gharama ya kiatu kimoja ni tofauti sana na gharama ya kiatu kimoja kwa jumla. Kwa mfano kiatu kimoja kikiwa kinauzwa kwa Shs 1000 kwa kimoja ila jumla ukiagiza kwa jumla ukiagiza viatu 10000 unaweza kuuziwa 100 kwa kimoja. Ukipiga mahesabu 10000 zidisha kwa 100 ni shs 1000000 ukijumlisha na usafiri na insurance labda inafika 1500000 au 2000000.

Kodi atalipa kwenye shilingi 1.5m au 2m.

Hapa tunaona kuna punguzo kubwa na unafuu mkubwa. Kwanza badala ya kugharamia shs 1000 kagharamia shs 100 tu. Pengine hiyo bidhaa yeye anakuja kuiuza kwa shs 5000 na zaidi kwa kila moja lakini Kodi imekatwa kwenye shs 100 tu .Ni faida kiasi gani inayopatikana mpaka kudai Kodi ni kubwa?
 
Jambo hili yawezekana wengi wakawa hawajuhi. Kuna jedwali fulani la Kodi ya ya kuagiza bidhaa nje na jumla ikawa Kama 62.5% kama sikosei.
Import duty bado iko juu sana kuliko Nchi zinazotuzunguka haswa Uganda ambayo haina hata Bahari.
 
Back
Top Bottom