Siungi mkono hotuba ya Rais Kikwete, SA

Siungi mkono hotuba ya Rais Kikwete, SA

Nikiwa kama mtanzania mwenye mtazamo tofauti, nimejaribu kusikiliza hotuba nyingi mpaka sasa naona ya Kikwete imejaa sana ubinafsi na dhihaka wengi wanasifu na kuutambua mchango wa Madiba lakini yeye ameonesha kuwa Madiba si lolote si chochote na asingeyafanya hayo bila Tanzania.

Historia haijirudii na ukweli ubaki kuwa ukweli kuwa tumeshiriki vyema bt yeye katumia chance hiyo kama kujihalalishia masifasifa.

Kama mlikuwa makini, vicheko vya watu havikuwa vya kuvutiwa kwa hotuba bali ni utoto na ulimbukeni wake aliyokuwa anatoa. Just imagine Madiba kusahau viatu na yeye kumpelekea, INAHUSU!!

Kikubwa ameonge mambo sahihi lakini si mahala pake.

Mwenye akili timamu ataona kuwa kuna madhala makubwa juu ya speech hii

Ametudhalilisha sana

Kwanza sio Hotuba, ametoa historia ya mandela. Tangu lini kikwete akatoa hotuba zenye akili? Hajui hata historia ya Mandela.

Kikwete ametuaibisha ni bora angekaa kimya kuliko aibu aliyoitoa
 
Ndivyo ulivyodanganywa ukakubali.

Huyo wa kumuibia kura ni nani? Mzee wa gongo?

Ustake kuchekesha watu.

Umeona leo Jakaya na Kaunda walivyomsifu Nyerere?

Sasa wewe ambaye hujulikani hata magomeni tu unapata wapi guts za kumkashifu Nyerere?

Leo umeumbuka ndio wakati wa live thread umeingia mitini.
 
sio lazima ukaandika,kuna mambo kama huyajui acha,,,hadi sasa hujui kwanini Tanzania maskini kama rais wako,,,,
50+ years of independence hujui Y Tanzania maskini,then unadanganya jukwaa,nimeguswa sana na hapo kwenye blue,,,,hebu soma MKUKUTA I NA II,,,,
umaskin wa Tanzania unaweza ukaujua kupitia Voices of the Poor tafuta gugo

Kwa hivyo hizo Voice of the poor nini kiini chake?

Usijifanye kukwepa ukweli na ukweli utabaki pale pale,Umaskini
wetu ulitokana na huruma na siasa za kipindi kile kwa wenzetu full stop.

Hayo mambo yako ya Voice of the ya hiyo sijui gugo unayajua wewe na hao wenzako waliokuaminisha hayo.

Tatizo hatufuatilili hotuba na kusoma historia,sisi kutwa kucha ni gugo tu hata kitu kinachohitaji upeo mdogo tu kufikiri.

Wao wenyewe SA wamesema Tanzania walitumia kila aina ya uwezo wake katika ukombozi kusini mwa Afrika,alafu wewe eti unakana kwa kisingizio cha gugo.

Kwa mtizamo wangu hizo voice of the poor kwa mtanzania si kitu,bali voice of the freedom and free democracy in among African Countries.Na huo ndio ulikuwa msimamo wa Shujaa wetu Hayati Mzee J K Nyerere kwa wenzake kwani aliamini kuwa Tanzania ikiwa huru alafu majirani zake wakawa hawako huru hiyo si voice of the poor bali ni ubinafsi ambao ungepelekea na sisi tusiwe huru.

Sijalidanganya jukwaa katika hili,nawe pia usipende kila kitu ku-gugo tu vitu vingine tumia akili zako mwenyewe kwani hiyo gugo yaweza kuwekewa data za kukupotosha.
 
Kupondea hotuba ya Mh. Rais eti kwa sababu ameonesha kuwa bila ya Tanzania mchango wa Hayati Mzee Nelson Mandela kwa Taifa lake usingeonekana,hii ni sawa kabisa.

Kupondea hotuba ya Mh. Rais eti kwa sababu ameonesha kuwa bila ya Tanzania mchango wa Hayati Mzee Nelson Mandela kwa Taifa lake usingeonekana,hii si sawa kabisa.
 
Mandela alifungwa miaka 27. Nyerere hakukaa selo hata mwezi.
Mandela hakutaifisha mali ya mtu alipotoka jela wala hakuleta azimio la Arusha wala azimio la Cape Town.
Mandela alisamehe wote waliomtenda na hakulipiza kama Kambarage alivyofanya. Kambarage alimfunga Kassanga Tumbo, Chief Fundikira, Chief Lugwishwa, na akamkimbiza Oscar Kambona nk
Mandela alitaka uhuru kwa watu wote bila kubagua mtu. Kambarage aliwafanyizia wote waliokuwa na mawazo tofauti. (Kambona, Mtei, Mapalala etc).
Mandela alikuwa anashaurika na anaambilika. Kambarage alikuwa hashauriki wala haambiliki.
Mandela hakutaka kuwatesa watu na siasa uchwara za ujamaa na kujitegemea. Kambarage alituletea balaa kiuchumi. Hata Colgate ama soda ilikuwa ni luxury item kwa watanzania!!
Mandela hakuwalazimisha watu kuhama kwenye makazi yao. Kambarage aliwalazimisha watu kuhama bila ridhaa yao.
Mandela hakuwa mnafiki. Kambarage alisababisha vita ili amrudishe swahiba wake Milton Obote madarakani.
Mandela alikuwa rafiki kwa wote na hata wale waliompinga. Kambarage aliwachukia waliokuwa maadui zake i.e.chief Fundikira, Kambona, Mtei, Kassanga Tumbo.
Mandela hakutaka vita bali amani. Kambarage alijiingiza kwenye vita na kuwaita majirani zake nduli. (Idd Amin/Biafra/Banda)
Mandela alitawala kipindi kimoja. Kambarage alikaa miaka 30 madarakani.
Mandela alijali free enterprise economy. Kambarage alitaka African socialism ambayo haikutekelezeka hadi leo.
Mandela alijali vyama vingi na wapinzani. Kambarage aliogopa na hakutaka multipartism wala kusikia wapinzani hadi alipotoka.
Mandela aliwapenda viongozi wote barani Africa. Kambarage alikuwa na siasa za makundi na majungu na hakuheshimu sovereignity ya nchi nyingine (alitaka kumrudisha Obote wakati alikuwa sio raisi wa Uganda, alimsupport Ojukwu na Biafra).
Mandela alipenda ku-reason na watu hata opponents wake. Kambarage aliwatisha opponents wake.
Mandela hakutishika wala kuwaogopa machifu wa makabila mengine. Kambarage aliogopa na kuwapiga marufuku machifu wa makabila mengine nlakini akamwacha chifu wa kabila lake tu (Chief Wanzagi).
Mandela haku-take sides. Nyerere alikumbatia Warsaw pact during the cold war.
Mandela alitaka uhuru wa kisiasa na kiuchumi. Nyerere alipinga uhuru wa kisiasa wala kiuchumi na kutusababishia majanga e.g. bidhaa ziliadimika kiasi cha kwamba hata kumiliki mafuta ya Kimbo au TV ilikuwa ni kuhujumu uchumi.

c/o SHERRIF

Watoto wa sikuhizi hakuna adabu unamlaumu hata Nyerere kuingia vita ya Uganda? Tuliokuepo sisi ndo tunajua kwanini aliitwa nduli. Kila nchi inashujaa wake na ni haki rais wako kusema ukweli kwani lipi lililokuuma kusema watanzania tumeisaidia SA. We did it and we are so proud for it. Upeo wako wa kufikiri ni finyu na ndo matokeo ya elimu ulionayo kichwani inaonesha hujaelimika wala kustaarabika.
 
Nikiwa kama mtanzania mwenye mtazamo tofauti, nimejaribu kusikiliza hotuba nyingi mpaka sasa naona ya Kikwete imejaa sana ubinafsi na dhihaka wengi wanasifu na kuutambua mchango wa Madiba lakini yeye ameonesha kuwa Madiba si lolote si chochote na asingeyafanya hayo bila Tanzania.

Historia haijirudii na ukweli ubaki kuwa ukweli kuwa tumeshiriki vyema bt yeye katumia chance hiyo kama kujihalalishia masifasifa.

Kama mlikuwa makini, vicheko vya watu havikuwa vya kuvutiwa kwa hotuba bali ni utoto na ulimbukeni wake aliyokuwa anatoa. Just imagine Madiba kusahau viatu na yeye kumpelekea, INAHUSU!!

Kikubwa ameonge mambo sahihi lakini si mahala pake.

Mwenye akili timamu ataona kuwa kuna madhala makubwa juu ya speech hii

Ametudhalilisha sana

umejidhalilisha mwenyewe tu kwa upeo mfupi

kwenye shughuli kama zile, na hasa dunia ya leo ambapo west wanataka kuandika historia yetu upya, ni vyema uiweke wazi

JK amefanya alichotakiwa kufanya, nacho ni kuiweka kwenye ramani historia ya Tanzania katika kufanikisha utokomezaji wa apartheid in SA

Daym i wish Lucky Dube was alive... this was a day we would recognize how gifted the man was
 
toa ya kwako ambayo unadhani kikwete angestahili kuitoa.

kwani yeye ni rais mbona mnakuwa na skili za kushikiwa..yaani tufananishe taasisi ma speech ya dr dt dr dt kikwete, kikwete akubali kukodolewa kuwa speech yake ilikuwa mbaya hata mtoto wangu wa chekechea asingeandaa speech mbovu kiasi hicho
 
Mimtamu, naomba tujuzane kidogo...Naipongeza sana hotuba ya Rais wangu kwa sababu Ukweli ni kwamba Watu wa South Afrika hasa weusi wenzetu wamesahau kabisa ni kiasi gani Tanzania ilijitolea kuwasaidia kupigania kutokomeza ubaguzi wa rangi. Ni hivi inashangaza ni kiasi gani South Africans hasa weusi wanawatendea vitendo vibaya Waafrika wengine waliopo South Afrika Rais wetu amejaribu kuwakumbusha..Katika msiba mzima wa Mzee Madiba South Africans waliwaabudu sana watu wa Magharibi, Middle East, Central and South America na kusahau Afrika yote kuwa ndiyo iliyojitolea kwa kiasi kikubwa kuwasaidia kujikomboa toka mikononi mwa makaburu. Hakuna nchi hata moja ya Magharibi na kwingineko waliiweza kueleza ni kiasi gani Afrika ilikuwa mkombozi mkubwa wa Afrika Kusini. Vyombo vyote vilikuwa vikieleza oh USA ilifanya hivi Canada ilifanya hivi UK ilifanya hivi bila kuihusisha Afrika kwa ujumla na jumuiya zao kama OAU etc.. Rais wangu umefanya kazi nzuri sana nakupongeza kwa hili.. South Afrika kumsahau Mwl. Nyerere kiasi hiki???
 
Kwa hivyo hizo Voice of the poor nini kiini chake?

Usijifanye kukwepa ukweli na ukweli utabaki pale pale,Umaskini
wetu ulitokana na huruma na siasa za kipindi kile kwa wenzetu full stop.

Hayo mambo yako ya Voice of the ya hiyo sijui gugo unayajua wewe na hao wenzako waliokuaminisha hayo.

Tatizo hatufuatilili hotuba na kusoma historia,sisi kutwa kucha ni gugo tu hata kitu kinachohitaji upeo mdogo tu kufikiri.

Wao wenyewe SA wamesema Tanzania walitumia kila aina ya uwezo wake katika ukombozi kusini mwa Afrika,alafu wewe eti unakana kwa kisingizio cha gugo.

Kwa mtizamo wangu hizo voice of the poor kwa mtanzania si kitu,bali voice of the freedom and free democracy in among African Countries.Na huo ndio ulikuwa msimamo wa Shujaa wetu Hayati Mzee J K Nyerere kwa wenzake kwani aliamini kuwa Tanzania ikiwa huru alafu majirani zake wakawa hawako huru hiyo si voice of the poor bali ni ubinafsi ambao ungepelekea na sisi tusiwe huru.

Sijalidanganya jukwaa katika hili,nawe pia usipende kila kitu ku-gugo tu vitu vingine tumia akili zako mwenyewe kwani hiyo gugo yaweza kuwekewa data za kukupotosha.

ajabu kabsia,yani ww ukiulizwa kwanini Tanzania maskini,utasema kwa sababu ya harakat za ukomboz kusini mwa afrika????
Nimekwambia usome kitabu hiko acha uvivu,,,,,,
 
Na hii ndio aina ya baadhi ya members tulionao JF sasa....Hajui hata anachokiandika. ..Eti Nyerere kusahau viatu!!

Ok..Ina maana Tata Madiba alirudi kwao pekupeku?

Umaarufu wa Madiba na legacy aliyoaacha ni kwa mambo aliyoyafanya na kuifanyia nchi yake baada ya kufunguliwa kutoka kifungoni alikokuwa kwa miaka 27.

Kabla ya hapo alikuwa ni mwana mapinduzi na shujaa tu kama Steve Biko na wengine.
 
Hotuba ya JK ni nzuri sana imesaidia kuiibua tz ktk sura ya dunia kwa sababu ripoti nyingi zilizokuwa zinatolewa (aidha kwa makusudi au la) hazikuitaja kabisa tz achilia mbali kuelezea ina mchango gani ktk ukomboz wa wenzetu hawa. Na km mleta hoja ni mfatiliaji mzuri wa hoja zinazoletwa hapa hili tulikwisha lilalamikia km ni upungufu ktk msiba huu.Kwa hiyo (kwa mtazamo wangu) ile ilikuwa ndio fursa ya mwisho kwa dunia kufahamu mchango wa tz. Au mtoa hoja ww ulitakaje? waliopaswa kutusemea wameshindwa kutusemea,je nasisi tukae kimya!!?

Unajua nchi yetu kwa sasa ina vibaraka wa aina nyingi. Simshangai mleta hoja.
 
Nikiwa kama mtanzania mwenye mtazamo tofauti, nimejaribu kusikiliza hotuba nyingi mpaka sasa naona ya Kikwete imejaa sana ubinafsi na dhihaka wengi wanasifu na kuutambua mchango wa Madiba lakini yeye ameonesha kuwa Madiba si lolote si chochote na asingeyafanya hayo bila Tanzania.

Historia haijirudii na ukweli ubaki kuwa ukweli kuwa tumeshiriki vyema bt yeye katumia chance hiyo kama kujihalalishia masifasifa.

Kama mlikuwa makini, vicheko vya watu havikuwa vya kuvutiwa kwa hotuba bali ni utoto na ulimbukeni wake aliyokuwa anatoa. Just imagine Madiba kusahau viatu na yeye kumpelekea, INAHUSU!!

Kikubwa ameonge mambo sahihi lakini si mahala pake.

Mwenye akili timamu ataona kuwa kuna madhala makubwa juu ya speech hii

Ametudhalilisha sana
Umejidhalilisha mwenyewe kwa thread yako. Speech ilikuwa muafaka katika wakati muafaka.
 
Rais Kikwete alialikwa kutoa hotuba hii katika mazishi ya Mzee Mandela kwa niaba ya the former Front Line States [FLS] zilizo ongoza mapambano ya kukomboa nchi za kusini mwa Afrika kuanzia Mozambique miaka ya 1960s. The FLS zilikuwa ziki-ongozwa na Mwalimu Nyerere mpaka mwaka 1985 alipostaafu na uenyekiti ukaenda kwa Kaunda wa Zambia mpaka 1991 aliposhindwa kwenye kura ya Urais wa Zambia na Chiluba. Rais Mugabe wa Zimbabwe ali take over mpaka 1994 when South Africa ilipopata uhuru na kazi ya FLS ikawa imemalizika. FLS ilibadilishwa na kuwa the Security Organ ya SADC.

Viongozi wote was Kusini mwa Afrika wanamtambua Julius Nyerere kuwa ndiye aliyekuwa chief strategist wa vita vya ukombozi wa nchi zao kuanzia Mozambique iliyopata uhuru 1975; Angola 1975 and Zimbabwe 1980. Baada ya Zimbabwe makaburu walikuwa mbogo na kuzi-sabotage nchi za FLS wakiwatumia kina Savimbi & UNITA in Angola and Renamo in Mozambique.

Hii ilifanya vita vya ukombozi wa Namibia na Afrika ya Kusini kuwa ngumu. Hata hivyo Makaburu walipata pigo kubwa sana katika the battle of Cuito Canavale huko Angola mwaka 1987/88 wakati vikosi vyao vya askari zaidi ya 30000 [elfu thelathini] vilipopigwa vibaya sana na combination ya vikosi vya Angola; SWAPO na ANC wakisaidiwa na askari wa ki Cuba na Ugermani ya Mashariki. Vikosi vya SWAPO na ANC vilikuwa trained Mgagao, Tanzania na inasemekana pia kuwa vilikuwa vikipata technical support ya JWTZ. Inasemekana brigedi mbili au tatu za makaburu ziliteketezwa kabisa hapo Cuito Canavalle na ndipo hapo makaburu wakasalimu amri na wakaanza kukubali kutoa Uhuru kwa Namibia ambayo ilifanyika mwaka 1991.

Kushindwa kwa Makaburu katika vita vya Cuito Canavalle vilisababisha kuanguka kwa serikali ya P. W. Botha huko South Africa na badala yake akaingia de Klerk ambaye ndiye aliye mwachilia kutoka Gerezani Nelson Mandela mwaka 1991. Kutoka hapo historia ya South Africa ikabadilika na wakapata uhuru/serikali ya demokrasia mwaka 1994 chini ya Mzee Mandela.

Katika hotuba yake ya leo Kikwete did an excellent job in explaining the role of Nyerere and Tanzania in the liberation of Southern Africa. Watu wengi huko Southern Africa na hata wengine hapa Tanzania hawajui hii role ya Nyerere and Tanzania vizuri. This was therefore a God given opportunity for Tanzania through Rais Kikwete to inform the World of this contribution. Indeed Mzee Kaunda alipoitwa naye kuzungumza alimtaja Mwalimu Nyerere several times pamoja na Mama Maria Nyerere na kumshukuru Kikwete kwa hotuba yake.

Utaona pia baada ya hotuba yake ya leo Rais Banda wa Malawi kama Mwenyekiti wa SADC - the master of ceremony ali comment kuwa hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Malawi kujisafisha kwa Wa South Africans maana nchi yao ilijulikana kama kikaragosi and kibaraka mkuu was Makaburu hata mpaka mwaka 1994 wakati Rais Kibaraka Hastings Banda alipo-ondolewa madarakani - indeed umati katika Mazishi yale ulicheka kwa dharau.

In short Rais Kikwete did an EXCELLENT JOB TODAY IN TELLING THE SOUTH AFRICANS AND THE WORLD of THE ROLE OF JULIUS NYERERE AND TANZANIA IN THE LIBERATION OF THE SOUTHERN AFRICA STATES. THIS WAS A GOLDEN OPPORTUNITY AND ONLY A NAIVE PERSON WOULD NOT HAVE TAKEN IT UP. LET US GIVE DUE CREDIT TO OUR PRESIDENT WHEN HE REPRESENTS THE COUNTRY WELL. THERE WERE NO OTHER PRESIDENTS/external leaders FROM AFRICA or elsewhere who were ALLOWED TO SPEAK AT THIS FUNERAL CEREMONY TODAY OTHER THAN THE CHAIRPERSON OF AFRICAN UNION - PM of Ethiopia and the SADC Chair President Banda of Malawi and of course President Zuma himself. So Let us give our President the due credit he deserves.

Nilichopenda kuongeza hapa karibu wale Wote waliokua kwenye system ya kuikomboa SA walikua mazimbwi Morogoro na pia ata baadhi walioko sasaivi kwenye system SA walikua hapa Morogoro!
 
Back
Top Bottom