Nikiwa kama mtanzania mwenye mtazamo tofauti, nimejaribu kusikiliza hotuba nyingi mpaka sasa naona ya Kikwete imejaa sana ubinafsi na dhihaka wengi wanasifu na kuutambua mchango wa Madiba lakini yeye ameonesha kuwa Madiba si lolote si chochote na asingeyafanya hayo bila Tanzania.
Historia haijirudii na ukweli ubaki kuwa ukweli kuwa tumeshiriki vyema bt yeye katumia chance hiyo kama kujihalalishia masifasifa.
Kama mlikuwa makini, vicheko vya watu havikuwa vya kuvutiwa kwa hotuba bali ni utoto na ulimbukeni wake aliyokuwa anatoa. Just imagine Madiba kusahau viatu na yeye kumpelekea, INAHUSU!!
Kikubwa ameonge mambo sahihi lakini si mahala pake.
Mwenye akili timamu ataona kuwa kuna madhala makubwa juu ya speech hii
Ametudhalilisha sana
Ama kweli Watanzania wenzangu exposure nikitu kizuri sana.
Kama hukuona Kikwete kazungumza la msingi nadhani wewe ni kati ya wale waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiibeza nchi yetu.
Naomba nikuulize toka Mandela amefariki hivi kuna media yeyote ambayo imeigusia Tanzania, Baba yetu Nyerere au hata kuulizia ni kwa jinsi gani tumeshiriki katika UKOMBOZI WA MWAFRIKA HUKU KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA.
Umemsikiliza Ramaphosa MC alivyosifu juhudi za nchi yetu au ulikuwa unaangalia TV ZA KUNASA NA MANATI? Umemsikia Kaunda alivomalizia, jamani sasa nimeamini kuwa kweli ELIMU YETU INAFAA KUANGALIA UPYA NA HATA UKWELI NDANI MIOYO YETU PIA.
Nimetoka kuangalia BBC hakuna hata neno toka Tanzania iki maanisha kuwa wameumbuka na elimu ya ujuzi wa historia. THE WORLD HATE TANZANIA NA WEWE UNASUPPORT Samahani ingawa umesema ni mawazo yako lakini think BROAD. Juzi MADIBA CHANNEL sijui kama uliona hakuna historia hata kidogo juu ya Tanzania ilivyojitolea.
Hivi Nyerere angekataa kuwapa fadhila ingekuwaje?
Rais wangu mpendwa kwa hapo kafanya kweli kuelezea UMUHIMU WA TANZANIA KATIKA STRUGGLE FOR FREEDOM IN AFRICA NA HASA JINSI ALICHOKIFANYA AFRIKA KUSINI na nampa HEKO kwa kuenda na MAMA NYERERE ili waandishi uchwara waumbuke na wote ambao hawelewi kama wewe ufunguke!
Ebu rudi tena kama unaweza kuapata jinsi Kaunda alivyomalizia..... pole sana
Nadhani hii itakufungua angalau usome INTERNATIONAL NEWS NA UWEZE KUANGALIA UPUUZI UNAOANDIKWA KUHUSU NCHI ZENYE MSIMAMO BAADALA YA KUSOMA MAGAZETI YA UDAKU TU NDUGU YANGU
Je ulibahatika kuhudhuria mkutano wa AFRICAN AMERICAN uliofanyika Arusha miaka ya nyuma, kuna mwandishi wa CNN aliulizwa kwa nini hawandiki ukweli kuhusu Afrika? ALISHINDWA KUJIBU LAKINI UKWELI NI KWAMBA WANAOGOPA UKWELI!
Sasa nani amfunge PAKA KENGELE KAMA SIO SISI WENYEWE ? Leo Kikwete kaonyesha mfano it was all about REALITY and not FAME..!PERIOD