Mandela alifungwa miaka 27. Nyerere hakukaa selo hata mwezi.
Mandela hakutaifisha mali ya mtu alipotoka jela wala hakuleta azimio la Arusha wala azimio la Cape Town.
Mandela alisamehe wote waliomtenda na hakulipiza kama Kambarage alivyofanya. Kambarage alimfunga Kassanga Tumbo, Chief Fundikira, Chief Lugwishwa, na akamkimbiza Oscar Kambona nk
Mandela alitaka uhuru kwa watu wote bila kubagua mtu. Kambarage aliwafanyizia wote waliokuwa na mawazo tofauti. (Kambona, Mtei, Mapalala etc).
Mandela alikuwa anashaurika na anaambilika. Kambarage alikuwa hashauriki wala haambiliki.
Mandela hakutaka kuwatesa watu na siasa uchwara za ujamaa na kujitegemea. Kambarage alituletea balaa kiuchumi. Hata Colgate ama soda ilikuwa ni luxury item kwa watanzania!!
Mandela hakuwalazimisha watu kuhama kwenye makazi yao. Kambarage aliwalazimisha watu kuhama bila ridhaa yao.
Mandela hakuwa mnafiki. Kambarage alisababisha vita ili amrudishe swahiba wake Milton Obote madarakani.
Mandela alikuwa rafiki kwa wote na hata wale waliompinga. Kambarage aliwachukia waliokuwa maadui zake i.e.chief Fundikira, Kambona, Mtei, Kassanga Tumbo.
Mandela hakutaka vita bali amani. Kambarage alijiingiza kwenye vita na kuwaita majirani zake nduli. (Idd Amin/Biafra/Banda)
Mandela alitawala kipindi kimoja. Kambarage alikaa miaka 30 madarakani.
Mandela alijali free enterprise economy. Kambarage alitaka African socialism ambayo haikutekelezeka hadi leo.
Mandela alijali vyama vingi na wapinzani. Kambarage aliogopa na hakutaka multipartism wala kusikia wapinzani hadi alipotoka.
Mandela aliwapenda viongozi wote barani Africa. Kambarage alikuwa na siasa za makundi na majungu na hakuheshimu sovereignity ya nchi nyingine (alitaka kumrudisha Obote wakati alikuwa sio raisi wa Uganda, alimsupport Ojukwu na Biafra).
Mandela alipenda ku-reason na watu hata opponents wake. Kambarage aliwatisha opponents wake.
Mandela hakutishika wala kuwaogopa machifu wa makabila mengine. Kambarage aliogopa na kuwapiga marufuku machifu wa makabila mengine nlakini akamwacha chifu wa kabila lake tu (Chief Wanzagi).
Mandela haku-take sides. Nyerere alikumbatia Warsaw pact during the cold war.
Mandela alitaka uhuru wa kisiasa na kiuchumi. Nyerere alipinga uhuru wa kisiasa wala kiuchumi na kutusababishia majanga e.g. bidhaa ziliadimika kiasi cha kwamba hata kumiliki mafuta ya Kimbo au TV ilikuwa ni kuhujumu uchumi.
c/o SHERRIF