Maendeleo tu
JF-Expert Member
- Oct 9, 2010
- 347
- 107
Kwani ni kipi ambacho ameongea Jaji Warioba ambacho ni kibaya kwa Watanzania? Kila mtu amesikia aliyoongea, nyie mnaopinga yeye kutoa maoni yake haya wekeni jamvini Watanzania wajue ni nini kibaya
Kutakuwa na elimu ya ujraia kwa umma na kila kundi litashiriki kuitoa elimu hiyo na fedha zim eshatolewa na UNDP..sasa kinachofanyika ni kwa kina Warioba kukimbilia kuwadanganya wananchi kuwa rasimu imetupwa badala ya kutoa elimu ya uraia kupitia makundi husika...Taasisi ya mwalimu Nyerere sio kundi husika hivyo wao wangetulia au wangefanya midahalo yao bila kuwaalika akina Warioba.
Laiza kama mnamtaka Warioba awe kimya vipi JK na kelele za kupiga kura ya ndiyo ? Je hatikiwi kuachia wananchi ?
Njaa zitakufanya wewe uingiliwe kwani unashabikia uvunjifu wa sheria...ungewashauri hao unaowateteta wapeleke hoja zao kwenye vikao vya bunge zijadiliwe na kumbukumbu ziwekwe na sio kumnunua warioba awasemee
Huyo Sitta wako ni vema ukamuuliza ilikuwaje akazomewa ile siku ya kuzima Mwenge kule Tabora baada ya kusimamishwa na JK asalimie.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
Warioba anatakiwa ajiunge na chama au kundi la jamii linalotambulika ili awashawishi wananchi wapige kura ya hapana lakini asitumie hoja kwamba yale aliyoyaweka yeye ndiyo yalikuwa sahihi na yaliyowekwa na bunge sio sahihi. na asiwadanganye wananchi kuhusu maadili na kumwajibisha mbunge kwani angezingatia gharama na muda angeelewa kuwa kama maoni yake yangekubalika basi yule anayeshindwa kazi yake inakuwa kumtengenezea fitina yule aliyeshinda hivyo hakutakuwa na shughuli za maendeleo zaidi ya kunyang'anyana madaraka. Mshauri Warioba asajili chama kwani ni yeye aliyeandika kwenye katiba kuwa chama cha siasa ndicho kitaelimisha raia kuhusu uraia.
Mkuu hawana hoja wanachojua ni kashfa na matusi waliyokaririshwa na watawalaKwani ni kipi ambacho ameongea Jaji Warioba ambacho ni kibaya kwa Watanzania? Kila mtu amesikia aliyoongea, nyie mnaopinga yeye kutoa maoni yake haya wekeni jamvini Watanzania wajue ni nini kibaya
Kwani Warioba sii mtanzania?akili mgando msiyo taka mambo kujadiliwa kwa uwazi mmezoea zidumu fikra sahihi za mwenyekiti hata kama ni utumbo
Na ninyi mnapowaambia watanzania kuwa katiba ni nzuri muipigie kura ya ndiyo mnakuwa mnamaanisha kuwa hawana akili ya kuamua wenyewe? Acha awaelimishe wale wanaotaka kusikia, kama hutaki kaa nyumbani au nenda kafanye unayoyaona ni ya maana. Unatoka huko ulikotoka na mabango kuonyesha kuwa hauungi mkono kisha unafanya fujo, umeitwa na nani? Hivi ninyi watu kwa nini ni wapumbavu namna hiyo? Tutaona mwisho wake tu. Huu ujinga ipo siku utakoma na ninyi mnaoshabikia tutakuwa pamoja tu maana Tanzania iko moja, hakuna ya kwako wala ya kwangu. Vurugeni amani tu lakini taabu zikianza tutazioga sote.
Upeo mdogo kila raia ana haki ya kutoa maoni yake bila kuwa chini ya kundi au chama chochote na anachotetea warioba ni maoni ya wananchi ili hali ccm mnatetea msimamo wa chama ambao unawalinda watawala na kuwanyima wananchi fursa ya kuwawajibisha viongozi wabovu, hivi inakuingia akilini rais kuwaomba wezi wa mabilioni ya umma warudishe ili hali serikali yake ikijaza magereza kwa wezi wa kuku
usitokwe na povu mkuu mjadala ulikuwa halali na ulitimiza vigezo vyote vya kisheria shida ni jazba za ccm kwa kuwa mnapenda kusikia tu yale mnayoyataka na kuyaamini kama vile ndio wenye haki miliki ya nchi hii tambueni kuwa umma umeamka na uozo wenu uko wazi kwa kila mtu
Fujo aliifanya au waliifanya wale waliokwenda kuwanyang'anya mabango wale vijana na kuwapiga na kuwarushia viti...angalia video zitakuonyesha ni kina nani waliokuwa wakirusha viti na kupiga watu..kama wangewaacha wale vijana na mabango yao nao wakaendelea kutoa pumba zao bila shaka mdahalo ungeisha salama..Napata mashaka na umafia wa Butiku kwani yawezekana kabisa kuwa amewaandaa vijana hao halafu akawaandaa na wengine ili vurugu zitokee apate kuitusi serikali...Vinginevyo nilitazamia kuwa angeliomba ulinzi mapema na kawaweka vijana wake milangoni, lakini alijua kuwa angeweka ulinzi mahudhurio yangekuwa hafifu naye alitaka ajaze watu.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
Uzushi mwingine huo..Warioba anatetea maoni gani ya wananchi?? yale ya serikali ya mkataba yapo? yale ya mabaraza ya kata yapo? yale ya wakulima na wafugaji yapo?? au unaota ndoto ya mchana..Warioba aliondoa maoni ya wananchi wengi akaweka maoni ya kikundi cha wachache..Zanzibar wengi walitaka serikali ya mkataba hakuiweka...tanzania bara ukiondoa kigoma na sehemu ya shinyanga na moshi sehemu zilizobaki wote walitaka serikali mbili na wengine hawakujadili kabisa muundo wa muungano...sasa hayo maoni ya wananchi ni yapi???Rais muungwana anaokoa kwanza fedha za umma halafu anawashitaki wahalifu na ndicho alichofanya Mheshimiwa Rais kwanza kuwaomba warejeshe na walirejesha tukaokoa mabilioni kadhaa na bado tukawashtaki na kuwafunga wengine..Wangeshtakiwa hivihivi wangeweza kutorosha hizo fedha nje ya nchi na wao wakakimbilia uhamishoni...Serikali haijajaza wezi wa kuku magerezani, tembelea upate takwimu, waliojaa ni majambazi ya kutumia silaha, wauzaji wa dawa za kulevya, wauaji, wahujumu uchumi na wahaini....UONGO WAKO HAUNA MASHIKO..JARIBU TENA BAADAYE