Abdul karim atiki aichambua hotuba ya warioba

Makonde plateu

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
1,447
3,490
NAITAFAKARI HOTUBA YA JAJI WARIOBA.
KAULI ZAKE ZENYE UTATA, ZINAHITAJI UFAFANUZI!

Mzee Joseph Sinde Warioba kitaaluma ni mwanasheria. Msomi wa zamani wa mwanzo wa Chuo kikuu chetu cha Dar es Salaam, kilichoanzia Mtaa wa Lumumba.

Kabla ya hapo wanafunzi wote waliotoka Tanganyika, walikwenda kusomea shahada zao aidha Makerere nchini Uganda ama Ibadani nchini Nigeria.

Mzee Warioba ameitumikia serikali kwa muda mrefu, ameshika nyadhifa kadhaa serikalini, Mwanasheria Mkuu kwenye utawala wa awamu ya kwanza chini ya Rais Julius Kambarage Nyerere, baadaye akawa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais chini ya Rais wa pili Ally Hassan Mwinyi.

Rais wa tatu Benjamin William Mkapa alimteua Mzee Warioba kuongoza Tume iliyochunguza mianya ya Rushwa.

Lakini utumishi wake haukuishia hapo.

Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete alimteua tena Mzee Warioba kuongoza Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu yale ambayo wananchi wangependa yaingizwe kwenye Katiba mpya. Mzee Warioba aliwasilisha mapendekezo ya Tume aliyoongoza, hadi leo yanajulikana kama mapendekezo ya TUME YA WARIOBA.

Kwahiyo huyu mzee ni mmoja wa viongozi wastaafu wenye busara na hekima. Ni mzee mwenye kuheshimika sana.

Hivi karibuni Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba aliitisha Press Conference akasema na jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari, nami nimemsikiliza kwa makini. Kwasababu kwetu sisi wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, tunamchukulia Warioba kama Raia mwandamizi senior Citizen.

Mzee Warioba ni aina ya viongozi wastaafu mwenye kuheshimika sana, ambaye anapaswa kusikilizwa na kuchukuliwa kwa umakini na uzito mkubwa, kwasababu ni mwenye busara na hekima.

Mzee Warioba anapaswa kusikilizwa kwa kituo, na kwa kila kauli inayotoka kinywani mwake, kwakuwa kila kauli yake huacha ujumbe .

Nlivyomsikiliza kwa makini niliona dhahiri Mzee Warioba alikuwa na mtimamnyongo ambao kwa muda mrefu alitamani kuitema, huenda alisubiri wakati mwafaka wa kuutema.

Hata hivyo njia aliyotumia inanipa mashaka, kwani njia hiyo imeacha maswali yasiyojibika na yeyote bali yeye mwenyewe.

Kwasababu kauli zake zenye utata hakuna mwingine awezaye kuzitolea ufafanuzi.

Bado mimi najiuliza, huenda pia Watanzania wengine wanaoitakia mema nchi yetu, nao aidha wanamshangaa Mzee Warioba au wanajiuliza kama mimi maswali yasiyojibika.

JE, Mzee Warioba alilenga kuufikisha ujumbe wake kwa nani? Kwa Rais ama serikali yake? Kwa Chama Cha Mapinduzi kama chama tawala au kwa wananchi?

Kati ya haya makundi matatu ni lipi hasa ambalo lilikusudiwa kama mlengwa mkuu wa ujumbe wa Mzee Warioba?

Ikiwa Mzee Warioba alikusudia kuufikisha ujumbe wake serikalini, kwanini aliamua kutumia Jukwaa la wanahabari?

Maana kwa uelewa wake wa mambo na uzoefu wake alio nao jinsi serikali ya nchii inavyoendeshwa, hapana shaka anajua vilivyo ni habari ipi ambayo fit for public consumption na ipi ambayo ni siri inayopaswa kuishia serikalini tu!

Kwa nafasi yake mzee Warioba anazo haki tatu, anayo haki ya kuonya, anayo haki ya kushauri pia anayo haki ya kukemea hata kwa lugha ya ukali, endapo ataona kuna baya linalofanyiloka, ambalo linalohatarisha Amani ya nchi.

Kwakuwa Mzee Warioba ni Mkristo namtolea mfano kutoka kwenye Biblia kitabu cha 2 Samweli 12: 1-25 ambako kuna kisa cha Mfalme Daudi, aliyetenda dhambi mbaya sana mbele za Mungu wake, Daudi alimtwaa mke wa mtu kisha akamuua mumewe.

Mungu alimtuma Nabii Nathan kwenda kumjulisha Mfalme Daudi dhambi yake, kiuhalisia Nabii alitumwa kwenda kumkemea Mfalme, tena kwa ukali.

Lakini Nathan hakumsuta Mfalme wake hadharani, bali alimwendea kwenye faragha, wakiwa wawili alimtolea Daudi mfano wa tajiri aliyekuwa na kondoo wengi na maskini aliyekuwa na kondoo mmoja. Tajiri alipotembelewa na wageni, alimnyang’anya maskini kondoo wake ili kuwakirimia wageni wake.

Mfalme Daudi aliposikia alikasirika, akahamaki akisema huyo aliyefanyanya hivyo kama aishivyo Mungu wa Israeli huyo anastahili kuuawa. Ndipo Nabii Nathan akamwambia Daudi, mtu huyo ni wewe. BWANA asema…..

Najua mzee Warioba siyo Nabii kama Nathan, lakini kwa umri wake, Rais Samia ni sawa na binti yake wa kuzaa, anaweza kumwendea nyumbani ama Ofsini akamshitakia lile analoona linafanywa vibaya na watendaji wake, ama akaenda kumkemea akiona kuna kosa amelifanya yeye binafsi. Lakini siyo kumkosoa hadharani, hiyo njia aliyotumia haikubaliki hata kwa Mungu.

Kwa nafasi yake kama Senior Citizen, Warioba anakiri yeye mwenyewe kwamba ni mwenye kuongea na wengi bila mipaka, kumbe kwanini alichagua njia hiyo ya kusema na wanahabari, badala ya kwenda kusema moja kwa moja na wanaoongoza serikali?

Katika hali ya kawaida si raia wengi wa Jamhuri ya Muungano wenye kuweza kufunguliwa milango wakati wote kwa mazungumzo na Rais wa nchi ama kupokelewa simu zao wakati wowote wakiwa na jambo kubwa.

Lakini mzee Warioba ni mmoja wa hao Raia wachache wenye nafasi hiyo, kumbe kwanini alichagua njia ya kusema na walengwa kwa mbali, ili kuufikishia ujumbe wake kupitia Jukwaa la Wahariri?

Nihitimishe kwa kumuuliza mzee Warioba swali. Je, anadhani hiyo njia aliyochagua itasaidia kuimarisha umoja, upendo, Amani na mshikamano wetu?

Warioba anajisikiaje jina lake linaponasibishwa na maneno makali ya kwenye midia: Warioba amchana laivu Samia?

Mzee Warioba aliulizwa, swali la kwanza lilitoka kwa Deodatus Babile, mwanahabari mwandamizi, ambaye aliuliza kuhusu idadi ndogo ya wagombea wa upinzani kweye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitendo vya vurugu na mauaji bila kujali ni wafuasi wa vyama gani.

Balile anauliza lilipo tatizo, kama nafasi zilikuwa 64,000 na wapinzani wakaweka wagombea 14,000!

Tafsiri yangu inahusu uhaba wa wagombea wa upinzani, maana pengo la 50,000 ni kubwa mno. Hivi ni kweli wapinzani kushindwa kuweka wagombea 50,000 hilo nalo ni tatizo linatokana na CCM? Au ni udhaifu wa viongozi wao kukosa mbinu za kueneza vyama vyao hadi ngazi ya vitongoji?

Mzee Warioba anawalaumu Polisi na zaidi serikali kuu kwa kuwaingiza Polisi kwenye siasa. Jambo jema ni kuwa Mzee Warioba hakusema wala hakupendekeza Jeshi hilo lifutwe.

Maana ni kweli pamoja na kwamba Jeshi hilo lina mapungufu yake na linahitaji kujengewa uwezo zaidi, bado hakuna mbadala wake unaoweza kuifanya nchi ikatawalika na ikatulia.

Kama kwenye Taasisi ya Polisi kuna wachache wasio waadilifu, hiyo haihalalishi sisi kuihukumu Polisi yote, kwakuwa bado wapo Polisi wengi nchini, wanaojitoa mhanga kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao.

Ni Polisi hao hao ndio wamepangiwa kuwalinda viongozi wetu, wakiwemo wastaafu. Kwasababu hilo ni jukumu lao.

Mzee Warioba ni mmoja wa wastaafu wanaolindwa masaa 24 na Jeshi la Polisi kulingana na sheria na Amri za Jeshi hilo, bila kujali Polisi ni wapenzi wa vyama gani.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Kwani ni nani huyu hatumjuo? Anamjua mkewe tu! Afanye yake aache kusafiria nyota ya mzee wa watu! Dunia ina mambo mengi sana so aangalie wapi anatokaje tu, hii ipo nje sana ya madesa yake
 
Afadhali ya Warioba kuliko wewe unayedanganya kuwa wapinzani waliweka wagombea 14,000 . Ungekuwa sio mnafiki kwanza ungejumlisha na wale waliokatwa na kutaja idadi yao kamili kabka hawajakatwa..
 
1. Ofisi ngapi za wasimamizi wa uchaguzi zilifungwa kabla ya deadline ya kupokea fomu za kugombea?
2. Wanachama wangapi wa kila chama waliomba kugombea katika kila kituo?
3.Wagombea wangapi wa kila chama walienguliwa katika kila kituo?
4. Sababu za kuenguliwa wagombea ni zipi katika kila kituo?
5. Wagombea wangapi kutoka kila chama walikata rufaa?
6. Rufaa ngapi kutoka kila chama zilikubaliwa?
7. Wananchi wangapi walijiandikisha wangapi katika kila kituo?
8. Wananchi wangapi walijitokeza kupiga kura katika kila kituo, na wangapi walizuiwa na wangapi walizuiwa?
9. Kila mgombea alipata kura ngapi katika kila kituo?

Kwenye uchaguzi ulioendeshwa kwa haki, hizi taarifa ni rahisi kupata. Matokeo ya uchaguzi wa Marekani unaonyesha mambo yote haya kwa uwazi kabisa. Sisi tunashindwa nini?

Naomba pia majibu ya maswali yafuatayo:
1.hivi kura zinahesabiwa katika vutuo cha kupigia kura na kuthibitishwa na mawakala kabla ya kupelekwa kwenye kituo kikubwa?

2.Kura zinatakiwa zihifadhiwe kwa muda gani ba ada ya uchaguzi kuisha?

Amandla...
 
Umeanza kwa namna ya kisiasa sana.
Hizo Haki ambazo umedai anazo unadhani ana uwezowa kuzisimamia? Je una uhakika hajawahi kutumia njia za kufikisha ujumbe na kugonga mwamba?
Unasema anajua Siri za serkali kwahiyo unataka kufunga kwenye boksi la kubaki na siri?

Hoja muhimu . Je hoja za ni za kweli? Kama sio basi umutuhumu kama ndio au sio ZIJIBIWE hadharani kama zilivyotolewa.
Ingeshangaza kama mhusika wa tuhuma hizo ndio angekuwa analalamika
 
1. Ofisi ngapi za wasimamizi wa uchaguzi zilifungwa kabla ya deadline ya kupokea fomu za kugombea?
2. Wanachama wangapi wa kila chama waliomba kugombea katika kila kituo?
3.Wagombea wangapi wa kila chama walienguliwa katika kila kituo?
4. Sababu za kuenguliwa wagombea ni zipi katika kila kituo?
5. Wagombea wangapi kutoka kila chama walikata rufaa?
6. Rufaa ngapi kutoka kila chama zilikubaliwa?
7. Wananchi wangapi walijiandikisha wangapi katika kila kituo?
8. Wananchi wangapi walijitokeza kupiga kura katika kila kituo, na wangapi walizuiwa na wangapi walizuiwa?
9. Kila mgombea alipata kura ngapi katika kila kituo?

Kwenye uchaguzi ulioendeshwa kwa haki, hizi taarifa ni rahisi kupata. Matokeo ya uchaguzi wa Marekani unaonyesha mambo yote haya kwa uwazi kabisa. Sisi tunashindwa nini?

Naomba pia majibu ya maswali yafuatayo:
1.hivi kura zinahesabiwa katika vutuo cha kupigia kura na kuthibitishwa na mawakala kabla ya kupelekwa kwenye kituo kikubwa?

2.Kura zinatakiwa zihifadhiwe kwa muda gani ba ada ya uchaguzi kuisha?

Amandla...
Ukiitaja tu Marekani tayari ushakosea.
Jamaa wanatuzidi kushughulisha akili zao.
 
Back
Top Bottom