Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Ni Ujinga uliokithiri kwa mtu mzima kama yeye! Hivi kwa umri wake haoni kuwa haya yametokea kwa ujinga wa mtoto Makonda?????? alitakiwa kukemea hilo kwanza na Pia asisahau "What goes around comes around" asubiri rumba lake tu ........ Mbona ameanza kuomba msamaha mapema kwa maaskofu??? Ujinga wake utammaliza.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
 
Uhuni wa vijana wa chama tawala unaoungwa mkono na bwana sitta ni dhahiri kwamba udhalimu huu ulipangwa na watu ambao ni wakubwa kiumri lakini hawajapevuka kidemocrasia. Mnaishi katika nyakati zilizopita wakati huu ni mwingine mbwa na risasi mnazojivunia iko siku zitawarudia tu, historia huwa haidanganyi. Kwetu sisi Waryoba is a hero na sitta ni mwizi tu wa kawaida anayeiba hata kura za siri.
 
cha msingi ni kuisoma hiyo rasimu ya katiba; tena umakini then ndo uzuri wake na ubaya wake. dokezo: hakuna katiba ambayo imewahi kukubaliwa na wananchi wote 100%; popote duniani, ila wengi wakiikubali inatumika. tuwe na subira
 
Sita ana upungufu wa akili kichwani.apuuzwe
 
Samuel Sitta ni mwanasiasa wa maji taka. Hana moral authority ya kumshauri hata mwendawazimu
Siku zote nimempinga EL lakini kwa sasa kati ya wawili hao the lesser evil ni EL

Kama kuna siku ntaambiwa nimpigie kura mmojawapo kati ya Sitta na EL ama sivyo ntauwawa basi ni bora EL mara mia kuliko paxx!>m*+?*&fuuuu Sitta
 
Hivi huyu Sita na Siti ni mapacha nini mbona akili zao zinafanana? Unaulizwa swali unasema sijibu hilo swali?
 
Huyu sitta Ni kenge kweli wananchi wepi waliopendekeza? yaani aombe mungu mabadiriko yasimkute Hai
Maana atafanyiwa kama alivyofanyiwa Samwel DOe Mshenzi huyu sisi tunamusubiria
 
Utabiri, kwa ubishi wa sita tutamsahau kweny anga siasa, na kuwa mzee wa viwango atamsimulia mke wake wala mind set yake asiwekee hata ujumbe wa nyumba kumi
 
vijana tunaimpact kubwa kwenye jamii tusikalie kuwachekea hawa wanasiasa kwani wameshatufanya wote akili zetu sawa sasa tuonesheni kuwa tunatofautiana katika kufikiria na tumechoka na maovu yao.
 
hivi kweli mh.sitta ana dini,kama anayo basi hajui atendalo.kama unaona mtu mzima anashabikia fujo ujue ana kasoro kubwa kiakili au kimwili. aelimishwe vita au fuja huletwa na kitu kidogo sana kimatendo au kimaneno. chunguza kote duniani utaona.
 
Halafu jaman wanajukwaa niwaulize kwa nia nzuri, hivi kuna kiongozi mkuu wa nchi, natia shaka nchi inakoelekea ni kubaya halafu kwa msimamo wa mawazo yangu jeshi letu lisijeingilia haya mambo ya siasa yatakapoharibika, tutaisahau tanzania tuliyoipenda na kusifika kwa mambo mengi.
 
Nimekuwa nikijiuliza siku zote..ile dhana ya ccm kuwa chama cha mapinduzi hasa enzi za mwalimu nyerere imekwisha na sasa mapinduzi yanayoongelewa na kusimamiwa na hao vijana wapya wa ccm baada ya nyerere ni mapinduzi ya kupindua mambo mazuri yenye manufaa kwa nchi na kuleta mabovu na mabaya yanayopingwa na wanachi wengi au hata wote kwa uwingi wao.

Jk kama mwenyekiti wa ccm..aliingia bungeni na kupindua maoni ya wananchi yaliyoratibiwa na mzee warioba na wengineo wengi kwa mwavuli wa tume ya katiba, sita akasimamia mapinduzi ya kuondoa vifungi vinavyoleta mapinduzi ya kweli kwa uchumi na siasa endelevu za nchii iliokwama kwenye lindi zito la umasikini wa kujitakia kwa viongozi wetu kukosa maadili na kuheshimu tunu za taifa.


Kama haitoshi...ccm wakajitekenya wakacheka wenyewe na kuserebuka wenyewe kusherehekea mapinduzi ya katiba mbovu waliyoipitisha wenyewe.....cha kustaajabisha jk akapindua tena..maridhiano yake na vyama vya siasa kuwa katiba itayopendekezwa ipigiwe kura chini ya rais mpya ajaye baada ya ujaguzi wa 2015.....amepindua upigaji kura uwe kabla ya uchaguzi wa rais...kwanini?


Mapinduzi hasi yanaendelea...rais anawatuma wabunge wa ccm wakaitangaze katiba mazuri yake kwa wananchi ili ipigiwe kura ya ndio ila sie wananchi tunaotakiwa kupiga kura tunanyimwa haki ya kuelezwa ubaya wa hiyo katiba pendekezwa....haya ndio mapinduzi yanayosimamiwa na chama cha ccm?

Nikimaliza kustaajabu ya musa haya sasa yanakuja ya firauni...."watu wote waongee....hata sitta?"....kweli sitta..where on earth didi you get the audacity and even morral credibility to give your blessings for the "planned sagga" against our soo holly-hearted, heavenly sent, little messiah...a true hero of our remaining last breath of the nation....mzee warioba..aka the warrior.

Sitta kama unaamini mungu yupo....nakuomba ukafanye patano naye la amani...hawezi kukuacha bila kukuonjesha machungu ya haya majibu uliyotoa plus madudu uliyofanya kwenye bunge la katiba....and believe me...rais ajaye atakuwa el....atakusulubisha kwa kuifutilia mbali hii katiba yako na kuileta ile ya warioba na mutaelewa kwanini warioba alikuwa, yupo na atakuwa sahihi milele juu ya ile katiba.

Mungu atujaalie uhai mrefu tuone kama tutakuwa na macho wakati huo, tusikie kama tutakuwa na masikio wakati huo na tuseme kama tutakuwa na kauli wakati huo...maana mwaweza hata kututia vilema....ila haya tuandikayo yataishi kuja kuonwa na kusomwa na wajukuu wa vijukuu vyetu.

Mungu ibariki tanzania mungu ibariki africa
 
Aliwatukana maaskofu. Ngoja aone matokeo yake. Ndio kwanza yanaanza kujionyesha. Halafu kashakubali kisaikologia ndiye kawatuma hao wahuni. Ykiulizwa swal jibu. Ukisema hujibu ina maanisha nini? Mbona kasema Warioba kajitakia? Hivi nae bado ni mwenyekiti wa Bunge maalum. ?
 
Mheshimiwa Sitta yuko sahihi kabisa nami namuunga mkono kwa asilimia mia...Warioba anatakiwa awaachie watanzania wataamua wenyewe lakini huku kuhangaika kwake na kujidai yeye ndiye aliyekaa na Mwalimu kuliko watanzania wote kutamuumbua siku si nyingi

Huyo Sitta wako ni vema ukamuuliza ilikuwaje akazomewa ile siku ya kuzima Mwenge kule Tabora baada ya kusimamishwa na JK asalimie.
 
Kwa maelezo yake Sitta, inawezekana kabisa kuwa ndiye aliyemtuma, kugharamia na kuratibu mpango wa Makonda!

Hilo halihitaji mjadala. Sita na genge lake wanaumbuliwa na ukweli ndo maana hawataki wananchi wajue ukweli. Wananchi tunataka katiba ya kuwawajibisha viongozi wetu na siyo ya viongozi wetu kutuwajibisha. Hili hatutalikubali na tutapambana hadi ushindi.
 
hivi kweli mh.sitta ana dini,kama anayo basi hajui atendalo.kama unaona mtu mzima anashabikia fujo ujue ana kasoro kubwa kiakili au kimwili. aelimishwe vita au fuja huletwa na kitu kidogo sana kimatendo au kimaneno. chunguza kote duniani utaona.
 
Back
Top Bottom