Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sita ni mmoja kati ya wapumbavu niliowahi kuwasikia katika nchi hii!

Sitta alishaambiwa mapema aje ulingoni akimaliza kuchakachua, mwenzie Warioba kitu ya Musoma Originali inamsubiria kitaa kwa lolote, na hana utani na hilo kwani anafahamu kuwa suala la katiba si la kichama bali ni la kitaifa

images
 
Mheshimiwa Sitta yuko sahihi kabisa nami namuunga mkono kwa asilimia mia...Warioba anatakiwa awaachie watanzania wataamua wenyewe lakini huku kuhangaika kwake na kujidai yeye ndiye aliyekaa na7 Mwalimu kuliko watanzania wote kutamuumbua siku si nyingi
Kwani Warioba ni Mhutu? Unaposema awaachie watanzania waamue yeye sio mtanzania? Kama mtanzania ana haki ya kuikubali au kuikataa. Sasa mtu kama Six anavyosema wengi wanaikubali, waliofanya fujo walikuwa wengi? Huyo ni Waziri na mtu anayefikiria kuwa raisi?. Pytuuu!!!
 
Ichondi...
kwani warioba ni mhutu? Unaposema awaachie watanzania waamue yeye sio mtanzania? Kama mtanzania ana haki ya kuikubali au kuikataa. Sasa mtu kama six anavyosema wengi wanaikubali, waliofanya fujo walikuwa wengi? Huyo ni waziri na mtu anayefikiria kuwa raisi?. Pytuuu!!!
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.

Mwendawazimu huyo, ulevi wa madaraka kitu kibaya sana, anataka Warioba akae kimya ili wapitishe ujinga wao?
 
And that time is 14th december 2014; 30th april 2015 as well as 30th October 2015..IT WILL TELL WHO AMONGST US IS perfect..
Aha, kama j.k alivyowaachia wananchi waamue sio? Mtavuna mlicho na mnachopanda definitely only time will tell
 
Kumbe Mantissa ungekuwepo ungemuua Makonda...angalia jinsi unavyodhihirisha utakavyokuwa tukikupa dola utawale...hakika utakuwa zaidi ya mumiani..
Cha kufanya hapa, ni jino kwa jino. Kama red bridged wapo, wafanye hiyo kazi. Naamini kama Makonda jana angekuwa Musoma, kilikuwa kifo chake. Kule hawataki upumbavu kabisa. Daa wajinga na wapumbavu ni wengi, wanakalia maneno tu vitendo hakuna, sijui kwanini, shit!
 
Na ww SITA njoo tukuonyeshe ulivyojitakia mwenyewe, tunakusubiri mtaani mkuu, malipo ni hapa hapa duniani hatusubiri hukumu ya Mungu huko ni mbali tutakuwa tumeshakufa wote, JITOKEZE NA WW TUKUONYESHE MHESHIMIWA WATANZANIA WA LEO TUKOJE
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
 
Samwel Sitta amekosea. Hakuwa na sababu ya kufurahia yaliyotokea au yaliyomtokea Jaji Warioba. Nafikiri yeye amejikita zaidi kwenye mapambano na Warioba amesahau kuwa katiba pendekezwa ni kwa ajili ya wananchi/watanzania wote Warioba akiwa miongoni mwao.

Yaliyomtokea Warioba kwa mazingira ya sasa atarajie kuwa yanaweza kumtokea yeye pia na pengine kwa namna ya fedheha zaidi. Kimsingi kongamano lilikuwa halali na waandaaji walifuata taratibu, hakukuwa na sababu ya vijana wale waliojitambulisha dhahiri kuwa ni wanachama au wafuasi wa CCM kusababisha vurugu ile ilhali walikuwa na nafasi ya kutumia hoja kupinga anachokiamini Warioba.
 
ati uko tayari kwa mapambano labda kubonyeza keybord ..ikiwa kile chama chenu na Seif wake wameshindwa kuwatetea wale muasho wasidhalilike huko kwa wagalatia unadhani utaweza kupambana na six ? UKAWA wote wameharisha kwa mjomba six achane nae usijaribu hata kutia mguu utazama wewe chubwi.
 
Kama sio mpango wao kumpiga mzee warioba ungekuta sasa hivi wale wote waliohusika wameshakamatwa lakini kwa sababu huu ni mpango wa ccm hakuna kitakachofanyika na kwa kweli hii katiba tulio wengi hatuhiitaji ila kwa ccm tuu ndio wanaitaka wala sio wote na wewe sita usipoangalia utapigwa tuu subirini mwone.afathali mzee warioba tuliowengi tunampenda huku mtaani.shida ni kwako wewe hakuna anayekutaka tena huku mtaani.
 
kama kweli Sitta ameongea hivyo inabidi aone aibu kwa kushabikia uharifu
 
Unaweza kujiuliza maswali mengi sana, kwa nini watawala wanang'ang'ania hii katiba pendekezi na wanajaribu kushadadia kwa nguvu zote na kuhakikisha hakuna anayetoa elimu juu ya hii katiba kwa wananchi. Tatizo hasa ni kwenye suala na Miiko ya Uongozi, Tunu za Taifa na Uwaijibikaji kwa viongozi yaani hapo ndipo CCM hawataki hata kupasikia. So wakisikia au wakiona mtu anazungumzia juu ya hayo mambo wako tayari hata kumtoa roho ili tu hii katiba pendezi ipitishwe. We jiulize kwa nini wanailazimisha? hapo utagundua kwamba kuna maslahi makubwa sana ndani yake.
 
namii naunga hoja ya mzee sita hivi nawauliza anachotaka nini mzee warioba au ndio tukubali alivyosema tutakutana mitaani ndio ameanza kupiga kampeni? aelewe kipindi chake kimepita
 
Back
Top Bottom