Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

Jamani naitwa mpwayungu nina miaka 24 hv hapo teku mtapata kweli koz ya kufundisha nursery jamani ntapata kweli. Ushaur plz jamani naomba
 
habarini wanajamvi?

Nimekuwa nwalimu wa miaka 5 sasa katika mkoa X na shule nayofundisha kwakweli si mbaya sana ina mazingira mazuri kiasi.Lengo la kuja hapa JF ni kuomba ushauri juu ya hatma ya maisha yangu.

Najua kila mtu hajawahi kutosheka juu ya mishahara yao lakini kwa sisi walimu naona hali inazidi kuwa mbaya, Serikali inatukandamiza kwa makato ya siyo ya lazima kama kuchangia mwenge na tunalazimishwa eti mwenge ukija mkoani kwetu lazima walimu tuwepo kuupokea.

kwanini kila kitu mpka sisi walimu tushiriki aiseee, nimechoka kuona kada yangu pendwa imekuwa inadharaulika na serekali kwa kutupiwa kila kitu cha kisiasa matokea yake walimu tumekuwa watu wa mkakati kwa wanasiasa ili kufanikisha azma yao.

Natamani kuacha ualimu ila naogopa wapi ntapata chanzo kingine cha mapato,na sitaki mikopo kabisaa

Naonmbeni ushauri wa wa biashara gani ya kufanya ili niondoke kwenye ualimu

(Sitaki kufungua kijiwe cha tuisheni, walimu tumekuwa tukiona tuisheni kama ni njia pekee ya kujiajiri SITAKIII)

msaada jamani
Ahahaahaaaaaa
 
Usiache kiboya mtaani kugumu, kopa kachukue viza embassy utapata kirahisi kwa Dhamana ya utumishi wanaamini hautozamia nenda shule kule Yuesiei, canada, japan, Korea kusini, Denmark, sweden, yukei, ukiwa chuo unapiga part-time, huku mshahara unaingia ndani ya miaka 3 baada ya chuo utafanya mafekechee jinsi ya kupata permit huko ukisimama vizuri unaadika barua ya kuacha Kazi juu kwa juu.
Mambo yakigoma unarejea zako bongo unaendelea na kazi.
Ualimu ni wito.
 
Acha Kazi upate Kazi ya kuitamani hata buku. Biashara zote zinalipa kwenye makaratasi, ingia field ndo utajua kwann frem nyingi zimefungwa.
Bongo kama wewe sio fisadi, mwizi, black market, au roga Sana Ili ulambe bila hivyo sahau kuhusu kutoka.
Mifumo yetu haisapoti watu kutoka.
 
Ni kwel inakera.ila usiache kazi mdogo wangu.piga kazi na jiongeze na izo bizness nyingine.halafu ukitoa iyo buku tano ya mwenge na kwenda kuupokea mwenge hautapungukiwa chochote.KWA MSISITIZO USIACHE KAZI
 
Tulia Sasa mkuu vuta pumzi, hapo cha kufanya kopa benki, baada ya hapo nenda Bayport kopa mpaka moja ya Tatu hakikisha kadi yako mshahara unaingia buku tano tu, baada ya hapo usiache kazi mwenyewe fanya kudoji kazini mwezi mzima bila taarifa utakuta barua ya kufukuzwa kazi juu ya Meza ya mkuu wa shule ndipo lengo lako litakuwa limetimia maana mkopo una Bima kwahiyo watajijua na mwajiri wako na Bayport itakuwa imekula kwao

Fanya biashara ya huduma za kifedha na ufugaji wa kuku kienyeji hutajuta baada ya miaka mitatu pesa yako ya mwezi utakuwa mshahara wa walimu watano wenye TGTS Wasio kuwa na madeni yoyote
Unamfunza wizi!
 
Ningependa kujua levo yako ya elimu?
Sababu ulizotoa za kuacha kazi ni za hovyo,mchango wa Mwenge ni hiyari,kuyumbishwa na wanasiasa ni maamuzi yako,walimu wengi ni waoga,hawawezi kujisimamia hata wanapoonewa,suala la kujisimamia ni la mtu binafsi,wapo baadhi ya walimu wanaheshimika kwny halmashauri zao,wanaogopwa pia kwa misimamo yao.
ukiendekeza uoga ipo cku utachapwa viboko hata na M/kiti wa serikali ya kijiji.
Kabla hujaacha kazi inakubidi uwe na kazi au shughuli nyngne yny maslahi kuliko unayoiacha.
 
Wewe SI ndio mwenye degree ya Russia ya engineering Hadi jirani yako kakununia.
Furahia uhalisia wako na upambane na hali yako
 
Ukwa mwongo uwe na kumbukumbu, si ulisema wwe una degree ya engineering Tena umeioigia Moscow, sio voice uume kuwa je mwalimu Tena na ulimponda yule ticha eti ana kuvimbia mbwa wewe huna akili
 
Hizi Halmashauri za vijijini ni kawaida.
Watu wanakopa na kusepa wengi sanaaa.

Kuna wanajeshi wengi sanaa wanakopa na kusepa.

Niliajiriwa na jamaa mmoja 2012, ye alifanya Kazi mwaka mmoja tu akakopa nakusepa.

Mpaka leo ana maisha japo si makubwa wala madogo ila yanaenda.

Kifupi Nina access na wengi waliokimbia na mikopo halmashauri, hivyo najifunza sanaa juu yao.

#YNWA
Kwani wanajeshi wapo halmashauri?
 
Walimu, kataa ndoa, Single mothers, wamekua maarufu sana JF, haipiti wiki hawajaongelewa masuperstars hao
 
Back
Top Bottom