Sitaki tena ndoa na Mamndenyi...!!!

Sitaki tena ndoa na Mamndenyi...!!!

Pamoja na kuwa sheria za dini yangu ya kikurya zinaniruhusu kuoa wananwake wengi kadri niwezavyo, lakini kwa Mamndenyi ninatangaza rasmi kuwa nimevunja uchumba wetu tuliokuwa tumeuanzisha hivi karibuni na ndoa ilishasajiliwa kwa mwenyekigoda Baba V

Nimelazimika kuchukua uamuzi huu wa kikatili dhidi ya moyo wangu kwa ajili ya kulinda undugu baina yangu na swahiba wangu Mr Rocky, ndugu yangu wa damu kabisa Slave pamoja na mzee mkuda bin mnoko Bujibuji.

Mwisho kabisa napenda kumhakikishia mama watoto wangu laazizi mwaJ kuwa awe na amani ya bwana huko aliko, atambue kuwa ndoa yetu itaendelea kudumu milele baina yangu mimi na yeye, yeye na mimi, sisi wawili peke yetu.
Kwi kwi kwiiiiii kwiiiiiii! Kwa hiyo baba watoto unaniruhusu nikazitumie zile hela kununulia khanga zenye msemo mppya? Sitaki kuuweka hapa huo msemo maana nataka nije kumrusha roho Mamndenyi! Lol!
 
Last edited by a moderator:
Kwi kwi kwiiiiii kwiiiiiii! Kwa hiyo baba watoto unaniruhusu nikazitumie zile hela kununulia khanga zenye msemo mppya? Sitaki kuuweka hapa huo msemo maana nataka nije kumrusha roho Mamndenyi! Lol!

Ruksa babe wangu mwaJ huu ndio wakati muafaka wa kuwakata ngebe wazabizabina wote. Wala usitaje khanga ina msemo gani ukishajitupia Mamndenyi ataisoma namba mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ajili yako natafuta ngariba, tena nataka ngariba wangu awe Mwita Maranya, aukate mkono wa sweta kwa panga butu, hii yote ni kwa ajili yako Mamndenyi wangu
Bujibuji kama umefikia hatua ya kujilipua kiasi hiki basi hapa umedhihirisha ni kwa kiasi gani unampenda Mamndenyi na uko tayari kufanya chochote anachotaka alimuradi tu akukubali.
Tafadhali sana Mamndenyi hebu mtendee hisani ndugu yangu Bujibuji anaonekana ana mapenzi ya dhati na wewe.
 
Last edited by a moderator:
Ruksa babe wangu mwaJ huu ndio wakati muafaka wa kuwakata ngebe wazabizabina wote. Wala usitaje khanga ina msemo gani ukishajitupia Mamndenyi ataisoma namba mwenyewe.

Si ulisema umenipa talaka kwa shingo upande wewe. Na kwanini umenificha hotelini kama una mke patachimbika.
 
Last edited by a moderator:
Kwi kwi kwiiiiii kwiiiiiii! Kwa hiyo baba watoto unaniruhusu nikazitumie zile hela kununulia khanga zenye msemo mppya? Sitaki kuuweka hapa huo msemo maana nataka nije kumrusha roho Mamndenyi! Lol!

kula hako kahela ka kanga ushangae. mi huyo huyo mumeo naona kaleta manguo kibao hapa na hizo kanga kila maneno yapo. mengine wameandika .jicho la mke mwenza. nyine .utakufa nacho kijiba cha roho. mmmh sijui utapita wapi mwaka huu.
 
Last edited by a moderator:
Bujibuji kama umefikia hatua ya kujilipua kiasi hiki basi hapa umedhihirisha ni kwa kiasi gani unampenda Mamndenyi na uko tayari kufanya chochote anachotaka alimuradi tu akukubali.
Tafadhali sana Mamndenyi hebu mtendee hisani ndugu yangu Bujibuji anaonekana ana mapenzi ya dhati na wewe.

Heee unaniuza? Sitaki sasag
 
Last edited by a moderator:
mwaJ usimwache anarudi kwako as soon as
sikujua kuwa ni mwana siasa
na mimi na hao watu tuko tofauti sana
endelea tu na Mwita Maranya wako.
Kumbe ndio hivyo! Khaaaaaaaaaaaaa! Ila asante sana msiri wangu Kaizer kwa kunipa hii siri. Ningeendelea kujipa moyo kuwa nipo peke yangu huku Mamndenyi ananicheka kwa pembeni. Bora niwaachie tu.
 
Last edited by a moderator:
mwaJ kama ni nyumba hata huko eti kuna nyumba, ha ha haaa
atarudi tu mwaya.
Nimekubamba sijakubambaa? Labda usirudi tena nyumbani! Kwa usalama wako baki huko huko!:A S-fire1:
:A S-fire1::A S-fire1:
:A S-fire1::A S-fire1:
 
Last edited by a moderator:
Nimekubamba sijakubambaa? Labda usirudi tena nyumbani! Kwa usalama wako baki huko huko!:A S-fire1:
:A S-fire1::A S-fire1:
:A S-fire1::A S-fire1:

Babe wangu mwaJ wala usiniwashie moto, nilikuwa namtania tu Mamndenyi wala sikumaanisha.
Mimi na wewe hadi ukamilifu wa dahari na hakuna mtu wa kututenganisha. Hakuna zaidi yako mama watoto wangu please naomba unielewe, hii ni mitihani ya dunia tu imenikuta lakini tumshukuru mungu kwamba nimeweza kuishinda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom