Sitaki kuolewa

Sitaki kuolewa

Wasalaam wana MMU,

Yaani weekend yangu ya leo imeharibika sana ...

Leo nimepata simu toka kwa mama zangu wadogo wakihitaji wedding dress ya mdogo wangu ambaye anataraijia kuolewa hivi karibuni niwatumie Tz ,baada ya maongezi mada ika badilika nikapachikwa swali WE NAWE UNAOLEWA LINI?

Maana wadogo zako wote wanaolewa we bado upo tu unafikiria nini haswaa?

Mwingine akadakia "Olewa basi uondoe japo mkosi",

kha! This is too much... Hivi jamani kuolewa ni kutoa mkosi???

Msimamo wangu:

1. Sitaki kuolewa kwa kuondoa mkosi

2. Sitaki kuolewa kwa sababu eti umri unaenda

3. Sitaki kuolewa eti wadogo zangu wote wanaolewa

4. Sitaki kuolewa kuwalingishia watu kwa na mimi nimeolewa

5. Sitaki kuolewa ili nivae shela au pete za ndoa kama fashion (ndoa sio fashion)

6. Sitaki kuolewa eti umri unakwenda kwa hiyo yoyote atake kuja mbele yangu anioe tu kisa naingia 30 ....Nope

Ladies haya ni makosa makubwa sana ukiyaamua kwa kufuata maneno ya watu kisa hujaolewa....matokeo yake unaolewa mchana usiku unaachika ni kutojiamiani na maisha yako.

XoXo
Hiyo namba 2 ya umri unakwenda hata mi huwa naishangaa, kwani ukiolewa ndo umri unasimama mbona unakwenda vilevile.
 
Watu wanatumika kama vyombo vya hotelini kila mtu anakitumia hadi chombo chenyewe kinaanza kukataliwa na wateja afu kinalalamika kiwa hakitaki kuwa hotelini tena
 
amu Hongera.Welcome Back !
 
Last edited by a moderator:
hiv jana niliwuliwa?
nilijiwuwa?
waliniwuwa?
au dubwana gani lilinikuta?
tafazali mtu yeyote mwenye mapenzi mema anihelp!
cc lara1, amu Dinazarde Khantwe @ et al
puleeez dada mkubwa anahitaji drip moja tu ya glucose.
 
Last edited by a moderator:
olewa upate heshima uitwe mke wa fulani au mama fulani ...hata uwe na gorofa kumi kariakoo utaitwa yule mwanamke ...

Labda hilo swala la kuitwa mke wa fulani....ila mama fulani unaweza itwa bila hata ya kuwa na ndoa.....
 
hiv jana niliwuliwa?
nilijiwuwa?
waliniwuwa?
au dubwana gani lilinikuta?
tafazali mtu yeyote mwenye mapenzi mema anihelp!
cc lara1, amu Dinazarde Khantwe @ et al
puleeez dada mkubwa anahitaji drip moja tu ya glucose.

Eeeeer diripuuu ya umbeaaaa mayoweeee
 
Last edited by a moderator:
Kuitwa mama fulani au mke wa fulani inakuongezea nini? Bora kuwa na gorofa linaloniingizia pesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom