Wasalaam wana MMU,
Yaani weekend yangu ya leo imeharibika sana . Leo nimepata simu toka kwa mama zangu wadogo wakihitaji wedding dress ya mdogo wangu ambaye anataraijia kuolewa hivi karibuni niwatumie Tz ,baada ya maongezi mada ika badilika nikapachikwa swali WE NAWE UNAOLEWA LINI?
Maana wadogo zako wote wanaolewa we bado upo tu unafikiria nini haswaa? Mwingine akadakia "Olewa basi uondoe japo mkosi", kha! This is too much... Hivi jamani kuolewa ni kutoa mkosi?
Msimamo wangu:
1. Sitaki kuolewa kwa kuondoa mkosi
2. Sitaki kuolewa kwa sababu eti umri unaenda
3. Sitaki kuolewa eti wadogo zangu wote wanaolewa
4. Sitaki kuolewa kuwalingishia watu kwa na mimi nimeolewa
5. Sitaki kuolewa ili nivae shela au pete za ndoa kama fashion (ndoa sio fashion)
6. Sitaki kuolewa eti umri unakwenda kwa hiyo yoyote atake kuja mbele yangu anioe tu kisa naingia 30 ....Nope
Ladies haya ni makosa makubwa sana ukiyaamua kwa kufuata maneno ya watu kisa hujaolewa....matokeo yake unaolewa mchana usiku unaachika ni kutojiamiani na maisha yako.
XoXo[/QUOTE
To every action there is an equal and opposite reaction by Isaac Newton.............."Happiness in life means making others happy ".............olewa upate hiyo reward,lakini siku zote moyo unauma,just imagine >30 wanapiga tu na kusepa,we unafikiri hao wazazi wako hawaumii kama we unavyohisi unaumia?