Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,015
- 144,372
Mtanisamehe kwa mada hii inayoweza kuleta ukakasi ila hili ni Jukwaa huru.
Tumekuwa tukiambiwa kuwa alietuweka hapa duniani alifanya hivyo ili tumuabudu. Binafsi hili swala kwangu linanifanya nikjiule maswali mengi sana;
1. Yaani alijichosa kisa tu kuabudiwa?
Na kama ni kweli ili tumuabudui, basi ni wazi ananufaika na sisi kumuabudu na hapa hoja yangu sisi viumbe hai kuwa kama mifugo kwake inapopata nguvu nyingine.
2.Kama alituumba ili kumuabudu, vipi kuhusu wanyama ambao wala hawatambui uwepo wake?
Hapa naendelea kupata imani kuwa sisi wanadamu na viumbe wengine wote alituumba kwa makusudi fulani na hii dunia ni kama zizi na sisi viumbe hai wote kwake ni mifugo, mifugo inayompa faida fulani.
Pia, ukichunguza, utagundua aliyeuumba huu ulimwengu, aliweka mazingira ya kuhakikisha hakuna siku hii dunia itakuwa na ombwe la viumbe hai, na moja ya mbinu hiyo ni kufanya tendo la ndoa(tendo la kujaamiiani) kuwa ni tendo la burudani(lenye utamu) ili viumbe hai wazaliane.
Hakuishia hapo, bali alihakikisha kila kiumbe hai naturally kinakuwa na upendo na watoto wake na zaidi kila kiumnbe hai naturally kinahakikisha mtoto wake anakuwa salama na anakua mpaka kujitegemea. Hapa lengo ni kuhakikisha kiumbne hai kikizaliwa kikue na kijaze hiii dunia ndio maana hata kuku anaweza kukudonoa unapotishia uhai wa kifaranga chake(this is work of nature).
Jambo lingine ni kuhakikisha hakuna tukio,ugomjwa au jambo lolote linaloweza kuangamiza kabisa uwepo wa vimbe hai hapa duniani.
Hii ni sababu kwanini tangu kuumbwa kwa hii dunia, hakuna ugonjwa uliowahi kutokea na kuangamiza aina yote ya kiumbe hai iwe ni binadamu, wanyama au wadudu. Likitokea gonjwa tishio, mwisho wa siku ama litatoweka au dawa yake kupatikana, na ndio maana akatupa mpaka maarifa ya kujitubu huku hata wanyama nao wakijitibu kwa kula majani na vitu vingine kama dawa,
Kwa kifupi, yako mambo mengi ya kiasili yanayohakikisha viumbe hai wanaendelea kuwepo hapa duniani, na wasitoweke kabisa licha ya species chache kudaiwa na wanasayansi kutoweka au kuwa katika tishio la kutokweka(extinction)
Pia, ukichunguza, utaona kabisa Nature ilishajipanga tangu kuambwa kwa hii dunia kuhakikisha viumbe hai wanaendelea kuwepo hapa duniani katika mazingiora yoyote na zaidi viumbe hai wasiwe wengi kuliko uwezo wa dunia kuwa-accomodate na bila shaka hii ni sababu kwanini viumbe hai wote hufa,
Kewahiyo, hapa conclusion yangu ni kuwa, hii dunia ni kama zizi, na sisi viumbe hai ni mifugo, mifugo ambayo inamnufaisha aliyetuumba kwa namna ambayo sisi hatuelewi kama ambavyo ng'ombe unaemfuga haelewi namna anavyokunufaisha.
Nawasilisha.