Mtakumbuka mwaka moja au miwili nyuma Sita,Nape,Mwakyembe walitembelea baadhi ya mikoa wakisisitiza na kutaka Chenge,Lowassa na Rostam wajivue magamba. Iweje leo ufanye kazi na gamba?? Inamana Chenge amejivua gamba lini?? Hakuna kipindi kigumu walichopata timu Lowassa kama baada ya Sita kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa bunge la katiba. Hapo akina Lowassa walijua ndio mwisho wao, kwani walijua Sita atapanda chati kwa kuongoza na kupatikana katiba nzuri ya Watanzania na angeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kugombea urais. Kama ccm wasingemsimamisha angeweza kuhamia chama chochote na kufanikiwa. Kwani Watanzania wangekuwa na imani nae. Hapo sasa ndio timu Lowassa ilipocheza kama German na kumvuruga Sita na kumweka karibu kuwa wapo nae kumbe ilikuwa kumwaribia, na yeye bila kujua akaingia mkenge. Na hapo ndio timu Lowassa ikapata ahueni kwani mbio za urais ndio zikaanza upya. Uku Sita akipigwa ngwala akiwa hana la kufanya. Ametendwa mara mbili bila yeye kungamua. TATIZO LA SITA NI TAMAA NA KUJISAHAU KWA MUDA ULIOPO