Nape Nnauye uliweza kumuangukia Hayati Magufuli; ni wakati wa kumuangukia Mungu na Mzee Lowassa kwa laana hii

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,966
6,652
Tunaoweka kumbukumbu sawa kwenye hii Video. Tunakumbuka hizi kauli zikitoka timu ya kampeni ya Hayati JPM, zikiongozwa na Nape Moses Nnauye na Abdulrahman Kinana chini ya mwamvuli wa Afya na uhai wa Rais atakayekuwa madarakani. Sihitaji kujua kama Msajili wa vyama vya siasa alikuwapo ama lah.

Hoja yamgu kwao hasa Nape ni kuwa, Kama Mheshimiwa Nape aliweza kwenda kumuomba msamaha Hayati JPM kwa kosa dogo la kusengenya utendaji wake na kubainika baada ya mawasiliano yao kudukuliwa jambo ambalo aliamua kutolilalamikia; Basi ni wakati wa Nape kwenda kumuomba radhi huyu mzee wa watu ambaye hakuwahi kumumtukana mtu kwenye kipindi hiko cha kampeni na hata baada ya hapo.

Na mwisho wanapaswa kutubiia kwa Mungu kwa dhambi hiyo ambayo KARMA kuna wakati inakuja kulipa. Si Ngumu kwa Bwana Nape kwani aliweza kumuangukia mwanadamu kwa kosa la kawaida sana. HATUWEZI JUA KESHO na Mungu amewaprove WRONG hiyo theory yao waliyotumia kuwahadaa watanzania majukwaani.Kiambata:
Binadamu tunapokuwa na Afya na nguvu huwa tunajawa na kiburi cha uzima na kujikuta tunaongea na kufanya mambo mengi sana yakiwemo mabaya na mazuri.

Watanzania ndimi zetu na ziwe na mipaka bila kujali tofauti zetu za kidini, kisiasa, kielimu, kiafya na hata kikabila.
Wewe kama unajihisi ni mzima wa Afya hebu usimdhihaki yule ambaye wewe kwa macho yako tu ya kiburi na dharau unaona kuwa sio mzima, hana Afya njema. Maana Watanzania kila mtu ni Daktari tena kwa vipimo vya macho tu atakuambia yule kaungua kitambo tu, yule hafiki mwakani hana maini yalishaungua yote n.k.

Hebu kama Mungu amekujaalia Afya njema mshukuru Mungu na uwaombee wale unaowaona kuwa ni DHAIFU sana kiafya ili nao Mungu awafanyie wepesi badala ya kuwasema vibaya, kuwadhalilisha, kuwanyanyapaa na hata kuwatabiria vifo. Wewe sio Mungu hata ujue kesho ya mtu mwingine au hatima yake. Ni Mungu pekee ajuaye kesho na hatima ya mtu.

Mwaka 2015 baadhi ya Ndugu zetu walimdhihaki na kumdhalilisha sana Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia alikuwa mgombea Urais kupita upinzani. Wakalionya Taifa kuwa lisimchague Edward Lowassa kwa sababu atafia Ikulu ya Magogoni muda si mrefu kwani ni dhaifu kiafya, ni mgonjwa sana. Atafia Ikulu atatupatia tabu na kutuongezea gharama za kuchagua Rais mwingine.
Wakaongeza Mzee Lowassa ni mgonjwa ndio maana anaongea dakika 15 hawezi kusimama kuongea masaa 2, mara ooooohhh mzee kajinyea, mzee alikula matusi balaa mpaka aibu.

Wakati anagombea Urais aliitwa majina mengi mabaya ya dhihaka kama vile MGONJWA, MAITI INAYOTEMBEA, ATAFIA IKULU.
Kiongozi mwingine kwa kiburi tu cha uzima na madaraka akajiapiza hadharani kuwa ikifika 2020 upinzani utakufa.

Mwanasiasa Marehemu Christopher Mtikila naye akaingia kwenye mtego wa kudhihaki Afya na maisha ya Lowassa. Akasema Lowassa Ni mgonjwa akienda Ikulu atafia huko na atalitia hasara taifa kuingia kwenye uchaguzi mwingine.

Katika dhihaka, matusi na kejeli hizo zote dhidi ya afya yake Lowassa alichagua kunyamaza kimya ili Mungu atete na kupigana nao wanaoteta na kupigana kinyume chake.

Lowassa akasema mwenzenu Mimi sipigani nanyi na wala sishughuliki nanyi ninyi shughulikeni na kuikejeli Afya na hatima yangu lakini Mimi namuachia Mungu ashughulike nanyi na apigane na wote wanaopigana kinyume changu. Lowassa "AKAMUACHIA MUNGU KUHUKUMU".

Lowassa alichowajibu wao ilikuwa ni "Mwenye kufahamu wwisho wa uhai wa Mtu ni MUNGU pekee...hao wanaosema mimi MGONJWA Je wakitangulia kuondoka wao wataenda kusema nini kwa MUNGU?"

Jifunze nguvu ya kunyamaza kimya hata pale ambapo unaona kuwa ulistahili kuongea. Si lazima kumjibu adui yako. Unapokaa kimya unatoa nafasi ya Mungu kumjibu adui yako kwa niaba yako. Iko hekima na siri kubwa sana katika kunyamaza.

Jifunze kutokuwa mwepesi wa kuhukumu. Usitoe hukumu za Afya za wengine, usitoe hukumu za hatima za wengine, usiwe mwepesi kukimbilia kuhukumu kwa macho tu. Jipe muda jiridhishe kwa ushahidi usioacha shaka yoyote ile. Jifunze kumuachia Mungu ahukumu kwa niaba yako maana hukumu yake ni ya HAKI na KWELI.

Lakini muhimu jifunze kuwa mvumilivu. Ili uweze kunyamaza kimya ni lazima kwanza uwe mvumilivu na ili usiwe mwepesi wa kuhukumu ni lazima pia uwe mvumilivu.

Mungu anasema mawazo ninayo wawazia ninyi ni mawazo ya amani na wala mawazo yenu si mawazo yangu na wala njia zenu si njia zangu.

Ukikaa kimya Mungu anazungumza na kukupigania. Anawajibu maadui zako, anawahukumu kwa niaba yako. Ohhh Yes! Hebu kumbuka orodha ya waliomdhihaki Lowassa na kumtabiria MAUTI leo wengi wao wapo kaburini, wapo vitandani n.k.

Bado ile sauti ya Celina Kombani, Kapteni John Komba, Christopher Mtikila, Nape Nnauye, Makamba na wengine nazisikia masikioni. Waliokufa Mungu awarehemu na walio hai Mungu awape rehema na Neema ya kutubu.

Nini maoni yako?
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
 
Wanasiasa hufuata upepo unapoelekea mkuu. Kisiasa yule mzee hana impact yoyote kwa nape. Japo wazo lako la kuomba radhi ni la kiungwana sana.
 
Wanasiasa hufuata upepo unapoelekea mkuu. Kisiasa yule mzee hana impact yoyote kwa nape. Japo wazo lako la kuomba radhi ni la kiungwana sana.

Ni kweli Mkuu, Basi aseme tu na Mungu wake kuwa pale Nilikufuru kuingilia mamlaka yako. Na tumejifunza pia
 
Hapana! Nape aiombe radhi familia ya Lowasa. Mzee hana makuu lakini kifamilia inaumiza sana. Kauli ngumu sana.
 
Dooh

Nakumbuka jamaa ile clip yake anavyotembea toka Getini kule huku anajifuta jasho Kwa leso.

Siasa hizi. Acha tu.
 
Back
Top Bottom