msnajo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 3,066
- 1,143
hili lizee bora liugue ebola lipumuzike
Una uhakika gani kwamba utabaki milele mkuu?
hili lizee bora liugue ebola lipumuzike
Nyie mliomtegemea huyu sita mmliula wachuya siku nyingi hebu fikiri.huyu bwana kamtimu mtu uwaziri mkuu lengo ajijenge urais na kashindwa kuwashawishi aliobaki nao ndani ya uongozi matokeo yake anakuja na vilio kashindwa na mwanake wewe umeshindwa kuwadhawishi wanaume wote mpaka ushindwe na mwanamke hufai.
Oo kakarupuka naanzisha chama kashindwa,
Oo mafisadi wavue gamba kashindwa kuwavua na leo hii kashindwa kuwashawishi wanzanzibar 10 tu ipatikane katiba inaypoendekezwa kaiba kura alafu eti tumpe nchi tumelongwa.Hiyo sapoti ya chama unayosema labda kile cha cck lakini kwa hiki cha ccm mzee huyu biashara yake imekwisha
Chonde chonde mleta mada lowassa hana ubavu wakupimana nguvu na Sitta. Sitta ana nguvu nyingi kisiasa na mikakati kuliko EL. Pia anayo support yga Chama na El hana. Kwa hiyo kama kuna mabaya yatakayo mkuta Sitta basi itakuwa bahati mbya na siyo ushawishi wa kundi pinzani.
Hii ni kwa mujibu wa fikra zako Binafsi lakini wengi wanajua Kuwa Lowasa ni Mziki mnene na support ya chama anayo kubwa japo ww unadhani hana support , Haya yanayomkuta Sita si bahati mbaya Bali nưi ya kujitakia mwenyewe,ikumbukwe Kuwa Sita akiwa Spika alimkomalia Lowasa akiwa na Mwakembe wakati walikuwa wakijua Kuwa Lowasa alikuwa akitumwa Boss mkuu na kila kitu alikuwa ananijua vyema. Huu mwezi wa Tisa ni mwezi wa Majanga na Vioja, Mungu kaanza kufunua moja moja, angalia Mwakembe treni toka Airport kimesanuka, Sita kaichakachua Katiba , huku Mziki wa Membe juu ya Pesa za Marehemu Gadafi ukianza kuimba kwa mbali , hapa Tanzania Hakuna kiongozi aliye msafii kiasi cha kumunyooshea mwenzake kidole, hata Mfadhili mkubwa wa Sita Mzee Mengi anayo madhambi yake , Nchi hii kila kiongozi akichunguzwa kwa kiiina zaidi Hakuna atakayepona.
Huyu bwana amefanya kazi kubwa aliweza kumuondoa PM wake kama unavyodai wewe. Hii inamaanisha kuwa PM mwenyewe hakuwa smart katika kukabiliana na wanaotajwa kuwa maadui zake kisiasa.
Nadhani Sitta anayo support kubwa sana kwa kuwa aliweza kupats 2/3 - UKAWA. Pia mbinu zake zitaweza kumfanya awashawishi CC, NEC na hatimaye wajumbe wa CCM GA.
Mengi, Sitta na 'mitume wale 12' ni chanda na pete hakuna cha kuwatenganisha. Ule wa Sitta kuteleza kuhusu vyombo vile vya habari kutangaza bunge la katiba, ulikuwa ni upepo tu, huo upepo umeshapita na hautarudi tena kuwatenganisha marafiki walioamua 'kulikomboa taifa kwa dhati' kutoka kwa...........Mengi atapatanaje na sita!wkt sitta alipendekeza Itv wafungiwe kwa sababu wanarusha midahalo ya katiba!!
Aaa kumbe unadhani sasa udhanivyo sivyo ndugu huo ushawishi hana mimi sidhani nimekupa mifano hiyo 2/3 nimekuambia kaiba na mwenyewe hilo unalijua katumua kaweka wajumbe hewa na bado kakwama hata mwanasheria waserekali yake kamkataa sasa useme kuna mtu hapo au ni boya achia mbali hao UKAWA ambao mimi hapa sijawaorodhesha mazuri yako
Ila ndugu kweli Unapigana na mtu ukampiga ngumi moja na yeye akakupiga tatu na nokauti moja utatoka na kusema nimeshinda kwakuwa mimi ndio wa kwanza kumpiga ngumi?
Ngumi ya kwanza Uspika chali
Ngumi ya pili Ccj chali
Ngumi ya tatu vua gamba chali
Ngumi ya nne katiba chali
Chezea El wewe
Hizo ni hasira za rasimu kamanda umeshindwa kuelewea siasa za CCM zilivyo unafananisha na za Chadema kufukuzana ovyo.Mtakumbuka mwaka moja au miwili nyuma Sita,Nape,Mwakyembe walitembelea baadhi ya mikoa wakisisitiza na kutaka Chenge,Lowassa na Rostam wajivue magamba. Iweje leo ufanye kazi na gamba?? Inamana Chenge amejivua gamba lini?? Hakuna kipindi kigumu walichopata timu Lowassa kama baada ya Sita kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa bunge la katiba. Hapo akina Lowassa walijua ndio mwisho wao, kwani walijua Sita atapanda chati kwa kuongoza na kupatikana katiba nzuri ya Watanzania na angeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kugombea urais. Kama ccm wasingemsimamisha angeweza kuhamia chama chochote na kufanikiwa. Kwani Watanzania wangekuwa na imani nae. Hapo sasa ndio timu Lowassa ilipocheza kama German na kumvuruga Sita na kumweka karibu kuwa wapo nae kumbe ilikuwa kumwaribia, na yeye bila kujua akaingia mkenge. Na hapo ndio timu Lowassa ikapata ahueni kwani mbio za urais ndio zikaanza upya. Uku Sita akipigwa ngwala akiwa hana la kufanya. Ametendwa mara mbili bila yeye kungamua. TATIZO LA SITA NI TAMAA NA KUJISAHAU KWA MUDA ULIOPO
Hivi 6 ana watoto kweli? Mbona hawasikiki?
Mtii01 unataka kusema huyu bwana is just a spent force. Wajanja wanamtumia ili wa survive kisiasa baada ya kujua kuwa anapenda sifa. Naomba ufafanulie kuhusu hili.
Nakubaliana na wewe ndugu Funza kuwa haw wanasiasa wote ni wachafu na hakuna anayestahili kumnyoshea mwezake kidole. Ushauri wangu CCM iwapambanishe Sitta, Membe, Lowassa, Sumaye na Makamba tuone nani zaidi kwenye NEC ya CCM. Mgombea takaposhindwa pale nafiki atakua ameridhika.
Hivi 6 ana watoto kweli? Mbona hawasikiki?
Mwanaume Ngangari , mwanaume jasiri, mwanaume shupavu hawazi akalia mbele za watu,hawezi toa chozi hata itokee nini, vigezo vya mtoto wa Mkulima au mtoto wa mfugaji au mtoto wa mchonga vinyago kwa sasa havitumiki vilikuwa vikitumika Enzi ya Ujamaa na kujitegemea , Nchi imepita kwenye Utawala wa majaribio ,watu wanataka Utawala wa kuleta maendeleo kwa kasi na kuziba mianya ya Ufisadi huku rasilimali za Nchi zikitumika ipasavyo kuifanya Tanzania Kuwa Kama south Africa .â
Na kama kuna chembe cha ukweli kwenye fedha za Gadafi kuhusu huyu Benard sidhani mambo yatamuendea vizuri. Hata hivyo, taarifa zinaonesha kuwa kuna a sort of diversification on candidates kwenye ''WAMA''project. The best option ya prince na baadhi ya bunge ni mtoto wa Mkulima. Mtoto wa mkulima is ok, tumuunge mkono iwapo ataamua kugombea. Lile suala la kutokwa na machozi ilikuwa ni ishara ya utu wahali ya juu na pia upendo kwa watu wake. Na lile la wapigwe tu nawaachia mtafakari wenyewe.