Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,032
- 3,129
Hapana, hii ipo kwenye jamii fulani fulani na huko hufanywa km mila na desturi, nimewahi kushuhudia kwenye hio jamii ukifika km wewe huna nyumba huwezi kukaa ukafanya mazungumzo na wale wanaomiliki nyumba, km wewe huna gari huwezi ukakaa chini ufanye mazungumzo na wale wenye magari, huna mtoto huwezi ukakaa unafanya mazungumzo na wenye watoto, huwezi kuongea na waliooa sababu wewe bado hujaoa, hio imekua km hamasa kwamba kwa mfano utasema sasa nataka kuongea na fulani na mimi sina mtoto nafanyaje?
Kamata kamanzi kamoja hapo kalikozubaazubaa mtaani piga mimba unapata mtoto, huyo aliekua haongei na wewe sababu huna mtoto akisikia unaitwa Baba fulani atataka kua na mazungumzo na wewe, sio wewe utataka kua na mazungumzo na yeye tena, sababu ya levels sasa level zenu zitakua zinaendana wenyewe hizo wanaziita levels,
wewe haujataliwa huwezi kukaa na watu waliotahiriwa eti unapiga nao story, story zenu zitakua haziendani au uchangiaji wako utakua wa hovyo lazima watakutimua tu utafute level zako mkae mzungumze,
wewe haujawahi kuzaa unakaa na waliozaa unajifanya wewe ndio unajua kuzaa kuliko wao yaan mazungumzo yenu yanakua hayaendani lazima watakutimua sababu ya levels
Uko sahihi bro.
Umeongelea Levels up.
Mfano.
Samahan nitaongelea mfano personal.
Miaka kama 8 nyuma. Nilinunua kiwanja na nikaanza kujenga. Ila Hela ikakata wakat bado niko kwenye msingi. Na nikakaa miaka 3 sijapagusa. Hadi msingi ukapata ukungu wa kijani.
Jiran zangu wanaonizunguka mmoja ana ghorofa na mwingne nyumba kubwa na mwingne nyumba ya kawaida. Wote wana ukuta na mageti.
Nilikuwa nawasiliana kwa simu na hao wawil wenye nyumba za kawaida. Ili kama kuna matengenezo ya barabara au maendeleo mengne ya mtaa wanishirikishe. Ila hakuna aliyenishirikisha😊😊😊 na ukiongea nao kwa simu wala hakuna mtu anakuchangamkia.
Wananiona dogo na sina hela.
Ila Nyumba imeisha miaka kama 3 hiv na imependeza. Na ina geti na kagari kama wao.
Sasahivi tunaongea tunacheka na tuko mabesti na tuna ushirikiano wa kutosha 😂😂😂😂. Had mwenye ghorofa ananipigia simu kama kukiwa na ishu mbili tatu kunipa taarifa.
Kwahiyo muda mwingne. Hii kutokupewa attention sehem. Tuigeuze iwe kama hamasa ya kupambana zaidi.
Na sio Kulalamika na Kulia