Felister,
Asante sana kwa ushauri wako murua.............huu ndio uzuri wa JF.............shule kila kukicha...........sio kuangalia upande mmoja tu............hisia yangu inaniambia uko/ulikuweko sana kwenye maeneo ya utafiti ...........kama assumption yangu kuhusu wewe ni sahihi............je kuna maeneo hapa nyumbani ambayo yametengwa/highlighted kuwa protected kwa kuwa ni highly sensitive kwenye ecosystem................je kama yapo information hizi ziko wapi............
Wakuu hii argument...................iliyoletwa na Felister ni muhimu kuizingatia...................
Ogah my friend am not that much deep..lakini niko njiani kuelekea huko Mungu ni mwema.......
Kuhusu maeneo yaliyotengwa yes yapo lakini kuna contradictions nyingi sana katika policies zetu so harmonization is of paramount....
Kubwa na lakuhofu ni enforcement ndo tatizo letu kubwa. Kwa uzoefu wangu mdogo wananchi vijijini wana feel impact ya environmental degradation kuliko mijini lakini poverty na ignorance inawa betray and have no choice other than kuendelea kuharibu hata kama wanaona wanachokifanya kina madhara kwa environment. Malalamiko yao makubwa ni kwamba hawako informed and so dont know how to save their environment.
Nilienda kijiji kimoja kinaitwa kikwawila wanasema ilibidi kijiji kizima ki abandone eneo walilokua wakilitumia kwa kilimo kwa maana hawapati kitu hata kwa kutumia mbolea. So wakasema wameamua kuhamia bondeni maana kule milimani wamepa conserve kwaajili wanaogopa kukata miti and so kwa vile kule bondeni hakuna miti so wamegawa mashamba kule... Was about to cry and had nothing to say look at how ignorant they are on environmental issues; to them conservation means planting/no cutting of trees....
Then they continued saying mwanzoni walikua wanapata shida kwani maji yalikua mengi sana lakini sasa afadhali baada ya kulima kwa muda maji yamepungua so they are now getting something..Imagine hawajui kwamba hiyo ndo destruction yenyewe ndo maana maji yamepungua and to them its afadhali.... Its terrible!
Well this is the very place which is ratified as Ramsar site....means wise use application is demanded..Lakini the question is what is wise use to the poor person? Leaving his children dying of hunger for the sake of environment?
Lakini wapo ma researcher wengi tu tena wenye elimu ya ajabu humu humu nchini kunizidi mara mia mimi; wenye uwezo wa kuleta ufumbuzi wa matatizo ya hawa watu...Watafikaje huko bila resources? Wako busy na kuangalia baada ya kupoteza muda wote nakua nyuma katika social issues sasa wanaangalia jinsi gani wata ziba hiyo gap maana anaelewa maana ya elimu so kumwacha mtoto wake apotelee kwenye ujinga yeye yuko busy na watu wengine is this possible?
Sasa ninachojiuliza wanasiasa huwa hawapati hizo information and if wanapata hawajui wataalamu wako wapi? Wakati mwingine najiuliza maswali mengi nakuishia kufanya lile naloweza na mengine kuyapeleka kwa Mungu kwanjia ya maombi....
Think of what is happening to Lake manyara; sijui kama hata kuna models za kujua what is the sedimentation rate ya hilo ziwa per minute... Lakini wapo wataalamu wa udongo, Climatology, hydrology, Ecology, environmental economics you name it wa hali ya juu wanatumika na mataifa yanayoendelea kwenye research zao tena kwakutumia samples za tz.... Hakuna mtu wakuwapa resources wafanye multi disciplinary research na kuja na long lasting solutions. Ziwa Victoria ndo hilo limekua source of livelihoods kwa some of academicians but no permanent solution... watoe majibu walogwe watakula wapi? Police? Na hata wakitoa who cares matokeo yana pamba CV za watu tu huku Ziwa likiendelea kukauka taratibu......
Matukio ya Kilosa tumeyasikia sijui solution yake ni kuwapa misaada wanachi bila kujua kwamba wetlands are very much degraded there; some of them are converted into other uses such as crop cultivation and habitation no alternative wetlands constructed na sijui kama resources zitatolewa kufanya scientific researches za uhakika ili kuja na permanent soulutions. Tena washukuru wamaasai kwa kuwatunzia baadhi ya wetlands zao vinginevyo hizo flooding ndo zinge kuwa oder of the day lakini kwa kutoelewa wanataka kuwahamisha ili wafyeke yale mapori waendelee na kilimo maana ardhi yakulima haitoshi...