- Thread starter
- #81
Mkuu nahisi ukitoa mrejesho kidogo itasaidia kuwainspire watu - Just thinking bro hata kama sio very positive kuna kitu watu watajifunza mkuu
Sabayi, ni mimi au unataka CHE GUEVARA II ?
Mkuu nahisi ukitoa mrejesho kidogo itasaidia kuwainspire watu - Just thinking bro hata kama sio very positive kuna kitu watu watajifunza mkuu
Sabayi, ni mimi au unataka CHE GUEVARA II ?
Wakuu...kheri ya mwaka mpya......kwa wale ambao tulianzia kwenye ile mada ya "Mtaji Milioni 10".....binafsi ningependa niwa-encourage.....kwa sabu hii biashara kilimo/mifugo inalipa....hivyo wekezeni......Tanzania siku hizi hakuna sehemu ambayo ni "MBALI".......uwe na dhamira na malengo.......
Malila Mkuu....nimekuwa kimya kidogo huku kwani......kwa muda sasa (more than a year)....sija-settle....lakini yote kheri....miradi ile...i.e. shamba....sikumbuki kama niliwahi kutoa feedback kuwa nilianzisha na kilimo cha mifugo (hiki kinanielemea....i.e. its too good! but complicated.......muda si mrefu nitahitaji msaada zaidi) inaendelea vyema sana...........
Tuendelee kupashana habari.........
Asante,
Sijui umri wako wala kipato chako, lakini kama umri wako ni chini ya miaka 45 basi weka juhudi ktk kuwekeza ktk ardhi na kama una nafasi ya muda pia wekeza nje ya mji kuliko na unafuu wa bei. Haya tukutane shambani, pale kwenye viti virefu mda bado.
mKUU FAFANUA HAPA KIDOGO, UNA MAANA WENYE ABOVE 45 HAWAFAI KUFANYA HIZI SHUGHULI?
Kuwekeza kwenye ardhi hasa mashamba zaidi kunahitaji plan nzuri. Watu wengi walinunua mapori huko Bagamoyo na kwingineko yamewashinda kuyaendeleza, kwa kijana wa chini ya miaka hiyo anaweza kutunza pori lake kwa kuotesha miti ya boriti, au mbao ( mitiki, misederela,eucalyptus,cyprus,pines, mivinje nk) na akavuna akiwa ktk umri sahihi. Ninao wazee wa umri mkubwa ambao nafanya nao kazi hii ya kuotesha miti, lakini si wengi na wengi ni kwa ajili ya vijana wao, vijana chini ya umri huo ni wengi zaidi.
Mtu mwenye umri mkubwa zaidi ya hapo hahitaji long term investment, short term investment zinahitaji mitaji mikubwa na ya uhakika ili kupata mrejesho wa haraka. Kwa kijana mwenye mtaji mdogo, toka nje nenda ktk miji midogo yenye future nzuri nunua eneo, anza kuliendeleza kidogo kidogo hata kwa kupanda milonge.Hata kijijini nenda kaanzishe shamba la mazao ya kudumu litakulipa siku moja.
Nikiangalia nyie wote ni vigogo wa jukwaa hili nini kimejiri Mbona mmeanza kuwa na ubinafsi kila mmojawenu anataka PM zamani nakumbuka mambo yote yalikuwa kweupe imekuwaje?
Mkuu Malila Mungu akutangulie katika safari yako
Umesomeka mkuu. jamaa zangu gani mkuu
Jamaa zako unapiga nao kazi huko uliko.
Hongera sana Mkuu Malila kwa hapo ulipofikia na pia hongera kwa kuinspire wengine na kutujenga kwenye mtazamo wa kujiajiri badala ya kuajiriwa.Ingawa me ni mwanafunzi napenda sana kuwa hata na shamba la mahindi,but source za kupata capital ziko limited maana sikubahatìka kupata loan ya board ,kwa hiyo hela ninayopewa na parents inatosha kwenye mambo ya chuo tu,ingawa natamani kuwa na viwekezo.All in all najua nitafanikiwa tu!Na lazima nijiajiri by any means,kama siyo sasa basi baadae.Hongera Mkuu,ahsante sana.
Asante,
Siku ukipata hata laki mahali nishitue ili nikutafutie kashamba pembeni yangu, nitakusaidia miche ya miti ili uanze kuitimiza ndoto yako ya kuwekeza japo kidogo. Kutokea hapo utaona mbegu yako inavyokuwa na kuongezeka sana. Mi nilianza na miti 50 ya pines, na nilipewa na jirani yetu.
Nimekuchagulia miti ya mbao sababu haitakusumbua kwenye management. Miradi mingine kama unasoma ni pasua kichwa.
Asante,
Siku ukipata hata laki mahali nishitue ili nikutafutie kashamba pembeni yangu, nitakusaidia miche ya miti ili uanze kuitimiza ndoto yako ya kuwekeza japo kidogo. Kutokea hapo utaona mbegu yako inavyokuwa na kuongezeka sana. Mi nilianza na miti 50 ya pines, na nilipewa na jirani yetu.
Nimekuchagulia miti ya mbao sababu haitakusumbua kwenye management. Miradi mingine kama unasoma ni pasua kichwa.
mkuu malila upo? tafadhali naomba contacts zako via Pm kuna maujuzi nataka niya pate kutoka kwako mkuu.
Angalia pm yako nimekurushia mkuu.
ninaipenda jf sana maana imenifanya niwe na mawazo +ve zaidi katka mmaendeleo na kuona kuwa ninayoyawaza ni mawazo mazuri zaidi.nmepanda miti yangu ya mbao ekari kazaa na nnataka kila mwaka nipande miti si chini ya ekari 5.wazo kuu ni kuanzisha sasa ni kuanza mradi wa kuku na mwakani ndio ntauanza.umasikini nauona unakimbia wenyewe maana ukiamua jambo na kuliwekea mipango na heshima juu yake utafanikiwa tuuu.respect to malila.