Bado hujanipata, sisi/mimi nazungumzia small scale ya eka 30 mpaka 50,ambazo kwa mishahara yetu bado hata kuziendeleza ni kazi ngumu,kama umepitia post zote utaona wengi wanalalamikia ugumu wa kilimo. Sasa hawa wachache wanaojitahidi ni sehemu ndogo sana ktk mamilioni ya Watz wanaotaka kuingia ktk kilimo cha Kisasa. Ukisoma sera za kilimo kwanza utaona kabisa,lengo ni kuwa na wakulima wenye tija ili taifa liweze kujitosheleza kwa chakula na hatimaye ziada iuzwe.
Ukitoka Mkuranga mpaka Lindi ni pori tupu,ukitoka Mikumi mpaka Ilula ni pori tupu,ukipita na Reli ya Tzr kuna mapori kibao yenye mito. Hoja yako inakosa nguvu kwa sababu,kilimo chetu hakitoshelezi mahitaji yetu. Hakuna aliye nyimwa ardhi ya kilimo. Watz tunapenda vitu laini kama DECI hivi,juzi kiongozi kawapa wawekezaji shamba la umma pale Usangu Chimala,badala ya kulima mpunga wao wanalima mibono,mbona hiyo husemi,bado sisi/mimi nasisitiza tukiweza kulima,basi tulime kilimo chenye tija cha mashamba makubwa,tuache paper work.
Leo pale Dar tunakula mpunga toka Thailand/India nk lakini mabonde yetu yenye maji yapo yapo pale Moro na Rufiji,na kesho jamaa toka middle east wanakuja kumegewa hekta 5000 walime.