Siri ya ufaulu ya baadhi ya shule za sekondari hii hapa

E073DCB0-9AD0-40B6-947C-482AAC7224AA.jpeg
 
Mkuu ulichoongea ni ukweli kabisa, me nimesoma st Kayumba Ila matokeo hayakuwa mazuri Ila nilikuwa mwanafunzi mzuri tu, nasema hivi kwa kuwa imagine nilipata 3 ya mwisho, sikuwa mpenzi wa kusoma kabisa Ila nilikuwa najiamini tu na akili ya by nature Ila najiulizaga mfano kama walimu wetu wangekuwa wanafundisha kutokana na format ya mitihani ya kitaifa inavyokuja ufaulu si ungepanda sana?

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ulichoongeq ni ukweli kabisa, me nimesoma st Kayumba Ila matokeo hayakuwa mazuri Ila nilikuwa mwanafunzi mzuri tu, nasema hivi kwa kuwa imagine nikipata 3 ya mwisho Ila sikuwa mpenzi wa kusoma kabisa Ila nilikuwa najiamini tu ana akili ya by nature Ila najiulizaga mfano kama walimu wetu wangekuwa wanafundisha kutokana na format ya mitigani ya kitaifa inavyokuja ufaulu si ungepanda sana?

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
Tena sana!
 
Kuna shule moja ipo Bukoba yenyewe ni kuanzia primary ni private basi watoto wanateleza tu mpaka form four unakuta wote wana one wawili au watatu ndio wana two! Wakitoka pale kwenda A level tofaut na pale wanatengeneza zero za kutosha ktk mitihani yao ya mwisho(form six) last week nimeenda kule mkuu wa shule ananambia ameamua aweke na A level palepale nafikiri mmeelewa kwanini! Najiuliza sijui atafungua na chuo kikuu kabisa
 
Uzuri wa hii nchi yetu ni kuwa, matatizo yote tuliyo nayo wote tunayajua. Solution ya hayo matatizo yote wote tunaijua pia. Ila sasa ni nani wa kuchukua hatua ku implement hizo solution ili kutatua matatizo tuliyo nayo hapo ndio kimbembe kilipo! Kila mtu anakaa pembeni kama vile yeye hahusiki wala hilo swala yeye halimgusi kabisa..😄
 
Kwanza kabisa mjue NECTA imebadilisha mtizamo..inahakikisha by any means; matokeo hayaidhalilishi serikali..hii tabia ni mpya-wengi hawajastukia..hapo nyuma matokeo mabovu yalianza kutumiwa kama hoja ya kisiasa..pili, nataman sana walimu wakuu-public schools wateuliwe kwa kushindanishwa na kupewa malengo!
 
Hatimaye tumeeleweka sasa, haya mambo ya kufanyiana marketing yafike mwisho, video chini inajieleza

Hapa wametumia akili nawapongeza, Mtoto wa Feza eti analinganishwa na wa Kantalamba anayeshindia mihogo wakati mwingine hata asiipate.
 
Kwanza kabisa mjue NECTA imebadilisha mtizamo..inahakikisha by any means; matokeo hayaidhalilishi serikali..hii tabia ni mpya-wengi hawajastukia..hapo nyuma matokeo mabovu yalianza kutumiwa kama hoja ya kisiasa..pili, nataman sana walimu wakuu-public schools wateuliwe kwa kushindanishwa na kupewa malengo!
Hizo mbinu zilikuwa enzi za utawala wa bwana yule baraza lilikua linaendeshwa ovyo na matokeo kila yalipokuwa yanatangazwa ufaulu unapanda yote kumfurahisha mkulu

Saiv tunarud enzi za kabla ya 2015 no kubebana bebana
 
Watu naona wanauliza uliza siri ya mafanikio ya baadhi ya shule binafsi za sekondari hapa nchini, siri ziko 2 tu, kwanza sio siri maana hizi mbinu japo sikubaliani nazo ila zinafahamika na zinatumika sana kwa shule binafsi zenye majina makubwa ili waendelee kupiga pesa ndefu. (Hii ni biashara kama biashara zingine).

1.) Kwa kuwa shule ina jina kubwa tayari, ili kuendelea kulinda heshima yao, huweka michujo mikali mno katika mitihani yao ya kujiunga nao. Kwahiyo from the start wanachukua vipaji maalum, yaani ile cream kabisa, na kwakuwa shule ina jina kubwa tayari, hata wanaoenda kufanya interview pale wanakuwa wameshajipima na kujua kwamba wanauwezo wa juu mno kiasi hata kuthubutu tu kwenda kufanya interview pale.

Sasa imagine mnaenda kufanya interview vipanga 1000 ambao tayari mnajiamini na uwezo wenu huko mlikotoka, halafu mnachujwa kiasi mnachukuliwa 200 tu, kwahiyo hao 200 wanaokubaliwa kujiunga ni vipanga wa vipanga tayari, kiasi hata kama wakifundishwa ‘physics’ na Speaker mtarajiwa Mwijaku, bado possibility ya kufeli haipo. Sasa hii inawezekana endapo shule yako inajina kubwa tayari, kama huna jina huwezi kupata fursa ya kuchagua cream, shule zingine zisizo na majina hulazimika kupokea makapi baada ya shule kubwa kulamba icecream yote pale juu, sasa utashindana vipi na mtu aliyeshika mpini kama huyu?! ( Nitawaeleza mwishoni).

2.) Sasa hawa jamaa ni wajanja sana, naongea hivi from experience kutokana na kwamba nami nilisoma moja ya shule binafsi zinazoogopwa ogopwa kwenye ufaulu wa mitihani, hivyo nawapa experience yangu ya mbinu (siri) wanayotumia. Hawa jamaa bwana mkofika ule mwaka wa mtihani, wanaanza mchaka mchaka wa kuwafanyisha mitihani ya taifa ndani ya shule , either kwa kutumia past papers au kwa kutunga wenyewe mitihani yenye format ya mitihani ya taifa, ili kujpima kuona ni yupi ataipaisha shule na yupi ataiangusha shule, basi unaambiwa kila mwezi ni mitihani ya taifa mnapigishwa, yaani i mean kila mwezi, hadi kuna wakati nilitaka kubwaga manyanga, it was too much! Mtu hadi unatamani kulia bhana!

Sasa ikikaribia kile kipindi cha uandikishaji na usajili wa kupata namba za mitihani ya taifa, wale wazazi wa wanafunzi ambao katika mitihani ya majaribio wanapata Div. 1 ya 11, 12 na kuendelea wanaitwa na kupewa taarifa wanafunzi wao watafanya mitihani ya taifa kwa kutumia vituo binafsi, na mzazi atakayelalamika anaweza hata kurudishiwa ada yake if the need be. Sasa nyie mnaokubaliwa kufanya mtihani kwa kutumia jina la shule ni wale mnaopata Div.1 ya 7,8,910 tu.

Sasa unakuta shule ilikuwa ina wanafunzi 400 wa kidato cha nne, ila wanaofanya mtihani mnajikuta mpo 92 tu, hadi mtu unashangaa, ni nini hiki?! Is this legal??!! Matokeo yanatoka waote mmepiga 1.7 hadi nyie wenyewe mnajiogopa. Sasa nawapa dawa ya kupambana na shule za namna hiyo, maana wanasema aliye juu mfuate huko huko, ukishidwa mrushie hata mzinga wa nyuki, stay tuned.

1) Ifahamike pasi na shaka, kwamba hakuna uhusiano kati ya kufaulu mitihani na kuwa na maarifa. Mitihani ina lengo la kupima uelewa wa wanafunzi, lakini kwa Tz lengo la mitihani si hiyo, lengo ni kutangaza biashara ya shule, hata ukitoka na maarifa ‘0’, ili mradi unaufaulu mzuri, the school is happy, parents are happy, inatosha...! Na hapo utanielewa kwenye point yangu inayofuata..

2) Hivyo basi, mwanafunzi mwenyewe inabidi ajue kutofautisha kati ya kufaulu mitihani na kuoata maarifa. Kwa teknolojia ya sasa, unaweza ukapata maarifa makubwa na mengi zaidi kwa kuangalia ‘instuctional videos’ za ‘Youtube’ndani ya mwezi mkoja kuliko maarifa utakayopata kwa kuhudhuria vipindi vya darasani mwaka mzima! Ila kumbuka maarifa haya hayawezi kukusaidi kufauli mitihani ya taifa ya Tz ambayo main goal ni kufaulu, wewe na maarifa yako tupa kule, kwenye mitihani ya Tz nobody gives f@ck na maarifa yako, nobody!!! Lengo ni kufaulu, pata maarifa kwa njia kama hizo za mtandaoni, ila kikubwa unatakiwa kufaulu, basi!!! Yes , its idiotic, but its the reality, live with it!! (Na hii ndio tunaulizana kwamba mzungu alituroga vipi waAfrika, kumbe kurogwa ndio huku), wao wanakazia maarifa sisi tunakazia kufaulu, what do you expect?! Mtoto wa primary China unaunda radio ya Fm huku kwetu anakariri formula za ‘Resistance’ na ‘Voltage’,

3) Sasa jibu ni moja tu, fanyeni kama wao wanavyofanya, nunueni mitihani bila kuwaambia wanafunzi, kisha badilisheni namba na maneno kidogo kisha wafundisheni, ikifika NECTA wanakutana na maswali yale yale ila namba tu ndio tofauti, basi, hata usaili TRA watu waliiba mitihani, ishu ni ufaulu tu, haya mengine huku mtaani ni simple sana, utatumia hata Youtube tu, mtanishukuru baadae, ibeni mitihani daadeki, kwani wao wanafanyaje mnafikiri..😂😂

==================================
Update: 21/01/2022
Sponsored ad ya Feza schools wakinadi ufaulu wao (Sio maarifa)

View attachment 2090256

===========================
Update: 29/01/2023

Hatimaye tumeeleweka sasa, haya mambo ya kufanyiana marketing yafike mwisho, video chini inajieleza

Wasaga kunguni, hatimaye viziwi wamewasikia.
 
Wanafunzi wa Serikali hakuna wachopata ni Maarifa 0-0 Bora hat seminary Mtu unaambulia kuwa na maadili Mema na jamii yako
Hapo mwisho ume conclude vizuri andiko lako, pia serikali lengo ni watoto wafike Hadi form four wawe na uelewa hata wakila zero kikubwa kupunguza ujinga na kutoa huduma huko private ni business Ili wapate wanafunzi wapige ada
N
 
2.) Sasa hawa jamaa ni wajanja sana, naongea hivi from experience kutokana na kwamba nami nilisoma moja ya shule binafsi zinazoogopwa ogopwa kwenye ufaulu wa mitihani, hivyo nawapa experience yangu ya mbinu (siri) wanayotumia. Hawa jamaa bwana mkofika ule mwaka wa mtihani, wanaanza mchaka mchaka wa kuwafanyisha mitihani ya taifa ndani ya shule , either kwa kutumia past papers au kwa kutunga wenyewe mitihani yenye format ya mitihani ya taifa, ili kujpima kuona ni yupi ataipaisha shule na yupi ataiangusha shule, basi unaambiwa kila mwezi ni mitihani ya taifa mnapigishwa, yaani i mean kila mwezi, hadi kuna wakati nilitaka kubwaga manyanga, it was too much! Mtu hadi unatamani kulia bhana!

Sasa ikikaribia kile kipindi cha uandikishaji na usajili wa kupata namba za mitihani ya taifa, wale wazazi wa wanafunzi ambao katika mitihani ya majaribio wanapata Div. 1 ya 11, 12 na kuendelea wanaitwa na kupewa taarifa wanafunzi wao watafanya mitihani ya taifa kwa kutumia vituo binafsi, na mzazi atakayelalamika anaweza hata kurudishiwa ada yake if the need be. Sasa nyie mnaokubaliwa kufanya mtihani kwa kutumia jina la shule ni wale mnaopata Div.1 ya 7,8,910 tu.

Sasa unakuta shule ilikuwa ina wanafunzi 400 wa kidato cha nne, ila wanaofanya mtihani mnajikuta mpo 92 tu, hadi mtu unashangaa, ni nini hiki?! Is this legal??!! Matokeo yanatoka waote mmepiga 1.7 hadi nyie wenyewe mnajiogopa. Sasa nawapa dawa ya kupambana na shule za namna hiyo, maana wanasema aliye juu mfuate huko huko, ukishidwa mrushie hata mzinga wa nyuki, stay tuned.
Waziri wa Ilmu dunia yupo ila huvishwa miwani ya mbao
 
Wanafunzi wa Serikali hakuna wachopata ni Maarifa 0-0 Bora hat seminary Mtu unaambulia kuwa na maadili Mema na jamii yako

N
Na seminary lazima ufaulu tu maana mwanafunzi mwadilifu lazima atoe tofauti na serikalini siasa plus tabia chafu na umalaya wa wanafunzi lazima wafeli tu
 
Back
Top Bottom