A
Anonymous
Guest
Baadhi ya shule za sekondari wilaya Mbinga zimeanzisha hostel bubu ambazo hazifai kwa matumizi ya wanafunzi hususan wa kike hasa madarasa ya mitihani na hata zile shule zenye hostel za wasichana hazina hadhi ya kuwa hostel.
Baadhi ya shule kama vile Kikolo, Mkwaya,Dr.Shein,Mkoha,Matiri zimegeuza madarasa kuwa hostel ambapo wanafunzi wanalala katika sakafu, wanafunzi wanajipikia wenyewe,hawana muangalizi( matron) n k.
Kwenye shule za sekondari za Ngwilizi,Miparu,Mbangamao,Mahilo,Litembo,Kiamili,n.k zinahostel lakini zinamapungufu makubwa sana, kama vile miundombinu mibovu ya vyoo,baadhi ya wanafunzi kuweka magodoro kwenye sakafu,upungufu wa vitanda,wanafunzi kujipikia wenyewe,ukosefu wa matrons,ukosefu wa ulinzi madhubuti.
Vilevile shule ya sekondari Ndela inatumia majengo ya kilimo kama hostel kwa wanafunzi ambapo majengo haya hayana hadhi ya kuwa hostel, wanafunzi wanalala sakafuni, wanajipikia wenyewe,hawana muangalizi( matron),wala mlinzi.
Baadhi ya wanafunzi kwenye shule hizi wanasema wanakumbana na changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea hata kunusurika kubakwa nyakati za usiku wakiwa wenyewe tu,walimu wa kike ambao wameteuliwa kuwa walimu wa mabweni wanaishi mbali na hostel za shule.n.k Vilevile wakuu wa shule wamegeuza hostel hizi kama mtaji kwao kwa kuanzisha michango ambayo baadhi ya wazazi imekuwa ni mzigo kwao.
Mamlaka husika za elimu wilaya ya Mbinga zimekuwa hazifuatiliii kabisa yanayoendelea mashuleni badala yake wanasubiri mpaka DC afanye ziara ......