Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

wewe unashadadia nini kalale au kakunwe kama umechoka jamvini

Kamanda umepanic,ila nshakusoma wewe nani mbona unapanic hiv.utajitaja muda si mrefu shauri yako.
 
Kama ulivyosema, kuna baadhi ya watu huwa wako hapa 24/7 kujibu kila bandiko linalohusu CHADEMA na baadhi ya viongozi. Huwezi kuwaona wanamtetea Mh. Zitto na ndiyo maana kwa sasa hawaonekani na hata wale ambao wanaonekana, kwa sasa wako mstari wa mbele kumpongeza Mh. Zitto kwa pongezi za kejeli. Hii ni ishara tosha kuonyesha kuwa CHADEMA kumejaa vijana vinyonga na maslahi tumbo. Hawako kwa maslahi ya CHADEMA bali kwa maslahi ya viongozi wachache ndani ya CHADEMA.

Na hili ndilo tatizo tulilo nalo waafrika: chuki na mtimanyongo na ubinafsi pale unapoona mwenzako amebarikiwa kipawa zaidi yako. Matokeo yake tunapigana sisi kwa sisi na kuendelea kuwa maskini.

Nilitegemea CHADEMA wangefurahi kuwa na kiongozi kama Zitto ambaye mfano wa utendaji wake huwezi kuulinganisha na wengi ndani ya CHADEMA.

Unfortunately, ubinafsi unawatia wengi upofu na kujifanya hawayaoni mazuri aliyoyafanya Zitto ndani ya chama.

Badala yake they capitalize on the human weaknesses ambazo kila binadamu anazo.

Matokeo yake, CHADEMA nayo itavurugika baadae waje kutoa visingizo visivyokuwa na msing ilhali wamejiua wenyewe.

Inakatisha tamaa ukifuatilia mwenendo wa siasa za Tanzania, hujui ni nani wa kumuamini. Its sad!
 
MHeshimiwa zitto, with all due respect, please do not sell us short, we are educated lots. I am one of your ardent supporter. Na ninajua ya Kuwa u were aware that there has always been A sinister plan to eliminate you anyways possible by some of the high ranking CDM leaders, who could never compete with you and saw you being the only obstacle to their plans. Yes I like the idea of trying to pull together the party, lakini usitufumbe macho, an usijaribu kuficha uchafu china ya carpet. Let the bad elements in Charlemagne be exposed and good riddance of them, Leo unawatetea bure tutu hao majangili, an usipoangalia watakupata tutu, Kama hukai makini. You are a thorn in their throat and there is no love between yourselves.
watu kama nyie ni wanafiki wakubwa,pretenders are worse than devils,kwanini hukutoa taarifa police.
 
Zitto hawezi pelekwa mahakamani na wanachadema ,mahakama ya zitto ni wananchi credibility yake zero hana nyimbo huyo anabebwa na CCM kwa sasa ndio alikoegemea
Mkuu, mimi naona kama umeamua kusema tu bila hata vipimo. Credibility gani hiyo ya Mh. Zitto unayodai imeanguka wakati thread yake hii ina mistari 20 ya sentensi lakini mpaka sasa inachunguliwa na watu karibia 1000.

Hata hivyo, kwa madai yako haya, kwa nini CHADEMA kiendelee kukaa na mzigo usiokuwa na manufaa sana sana unazidi kukiumiza kisiasa. Kwa nini wasimfukuze ili tujue moja. Kama kweli yeye ni debe tupu.

I'm sorry, Makelele yako hapa nafikiri hayasaidii wala kubadilisha lolote.
 
Ufafanuzi na maelezo makini kutoka kwa kamanda Zitto. Hawa waandishi wa mtanzania wamekuwa wapuuzi sana kadri siku zinavyokwenda.
Badala ya kujikita kuihoji serikali juuu ya kutekwa na kuteswa kwa mhariri wao Kibanda wao wamekalia kueneza udaku.
Wanachadema tusikubali kugawanywa na hizi propaganda nyepesi za waganga njaa wa habari corporation.
 
Last edited by a moderator:
zitto ni kiongozi na mwana siasa alie komaa...
 
You might be right, but my point is, hizi habari alitakiwa kuzikabnusha tangu mara ya kwanza hapa JF badala ya kuziacha!! Hainiingii akilini kwamba habari ile ilitolewa hapa JF na akaiacha watu wa-swalllow kama ilivyo lakini miezi kadhaa baadae anakuja kuikanusha hapa hapa JF lakini baada ya kutoka gazetini! Suala la Zitto kuiacha ile habari hapa JF ilikuwa ni kama aliona haikufaa kukanushwa na si ajabu ndio maana watu wakaiendeleza!

Maajabu 7 ya dunia...
 
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.


=============


Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html


Cheers!!.... waache wanaofikiria 'Mchemba-mchemba style' na kung'a kucha na meno ya wenye mioyo safi...waendelee hukohuko, wasizinduke kamwe...come 2015 CDM itakamata 'jukumu'...watasaga meno!
 
Mmmh!haya ndiyo maneno ya muumini au shabiki.na kwa maneno haya unajenga chama au unakibomoa chama?
Acha ujinga kijana, Mimi si muumin wa CHADEMA tu bali ni muumini watu wanaosimamia ukweli ambao wapo CHADEMA mfano Rais wangu Dr.W.Slaa, Sasa yanapotokea mazingira yenye utata kutoka kwa wanafiki kama ww kwa lengo la kuwachafua viongozi ambao wanatupigania, Mimi hapo huwa sileti unafiki bali ni kutoa ukweli tu, Ndio maana huwa nasema mtu yeyote anayepinga na kudharau kazi aliyoifanya Ben Saanane mpaka tukagundua uozo wa masalia basi mtu huyo atakuwa ni mwendawazimu zaidi ya pepo mchafu.
 
Wakuu mkitaka kumhukumu zito soma Paragrafu yote hii,nachukulia mawazo yake chanya! Usichulie tungo ya Mwisho tu hutatenda haki . Nadhani kaeleza vyema! Kuna watu wanachukua mstari wa mwisho tu!
CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
 
Wewe ndio Ben nini umekuja na ID hiyo uliyoambiwa uje nayo? Bado you need to prove your allegations kwa sababu mwingine anaweza kuja na kusema mwongo ni Ben!

Bottomline: Viongozi wa CHADEMA ni waongo?
hahaha..naona mkuu umeshitukia deal..hawa jamaa ben na zito wanapersonal bifu,au huyu ben ni proxy.yaani there is someone behind this guy and he is pulling strings.
 
Na hili ndilo tatizo tulilo nalo waafrika: chuki na mtimanyongo na ubinafsi pale unapoona mwenzako amebarikiwa kipawa zaidi yako. Matokeo yake tunapigana sisi kwa sisi na kuendelea kuwa maskini. Nilitegemea CHADEMA wangefurahi kuwa na kiongozi kama Zitto ambaye mfano wa utendaji wake huwezi kuulinganisha na wengi ndani ya CHADEMA. Unfortunately, ubinafsi unawatia wengi upofu na kujifanya hawayaoni mazuri aliyoyafanya Zitto ndani ya chama. Badala yake they capitalize on the human weaknesses ambazo kila binadamu anazo. Matokeo yake, CHADEMA nayo itavurugika baadae waje kutoa visingizo visivyokuwa na msing ilhali wamejiua wenyewe. Inakatisha tamaa ukifuatilia mwenendo wa siasa za Tanzania, hujui ni nani wa kumuamini. Its sad!

Mkuu Bocho nadhani wewe ndo unachanganya mambo, siyo kwamba Zitto leo anapewa sifa za kinafiki, la hasha, leo kafanya vyema kwa kutoa maelezo yaliyo ondoa mkanganyiko ulio kuwepo na ndo maana kapewa stahiki yake ya pongezi.

Lakini pia pale anapokosea ni stahiki yake pia kukosolewa na kulaumiwa ili kusudi arejee kwenye msitari. Kwa hili tunampongeza lakini pia anapobugi hatutasita kumkosoa
 
Mmmh!haya ndiyo maneno ya muumini au shabiki.na kwa maneno haya unajenga chama au unakibomoa chama?

Nikibome chama kwani nyundo na sururu umenipa saa ngapi?!

Yet Ingnored...............
 
Back
Top Bottom