Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

This is what i callTalk firstTalk fast Talk truthBravo Zitto.
 
Heshima ya Upande mmoja! Hapa Zitto utapongezwa kwakuwa tu 'umem-save' 'nabii' SLAA. Hawa hawa ndio wanaokuporomoshea matusi kila siku! Lengo lao wakutumie tu kama 'kile kifaa' kisha waku-dump! Sijui kama hulijui hili!

Ndugu acha kuwewezeka Mh. Zitto amesema yote. Fahamu kuwa CDM wana udhubutu wa hali ya juu wa kukemea mabaya ya mtu ye yote bila kificho. Kigezo hiki cha kupendaukweli na uwazi kinaongeza zaidi nafasi ya CDM kushinda uchaguzi 2015.Elewa kama unasubiri Dr. Slaa na Zitto wagombane utasubiri sana,
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Zitto yaani umenusuru Moyo wangu na msongo wa mawazo maana kwa hakika mimi huwa napendelea kusoma magazeti na kusikiliza radioni ila ya leo asubuhi yameniharibia siku baada ya kusikia habari hii japokuwa kwa hakina nilikuwa naamini kuwa si ya kweli ila uongo ni dhambi sikuweza kujizuia NIMEHUZUNIKA SANA na nkawa najiuliza nani wa kuniondolea tongo tongo hili kichwani mwangu...yaani mh zitto umenisafisha akili yangu na ule msongo umepotea ghafla...
ahsante zitto..
chadema oyeeeeeeeeeeeeeee....
hekima zako zitto ni nzitto sana regardless of your shortcomings as human being....
Chama kinakutegemea sana zitto na busara zako na promptness kama hii ya ku pre-empt njama za wabaya wa chama kama hawa watu wanaokichafua chama kwa mbinu mbali mbali.
Endelezeni mshikamano baina yenu wakubwa wa chama wekeni tofauti zenu za kibinadamu pembeni,jengeni chama ili wabaya wa chadema waumie matumbo yao..
maana wabaya wa chadema wanafurahia sana habari kama za gazeti la mtanzania la leo ziwe za ukweli ama za uongo wao hawajalishi...

asalaaaam....
 
mjomba life is not a rehersal is a performance nimefurahishwa sana na hii paragraph ya nne!!!!!!!umemaliza kila kitu ccm mijinga mijinga tu.
 
Nilipoiona habari ile katika gazeti, kwanza nilicheka, kisha nikapandwa na hasira, nakisha zaidi nikazama katika tafakuri pana,

Nilifanya hivyo kwa dhana ileile ya hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu,


Nilisubiri kauli ya ndugu yangu Zitto kwakuwa niliamini fika kuwa ni lazima ajibu, tena mapema na jibu lake ndio hili.

Kwanza kabisa dhana yakujibu namsifu kwa asilimia mia, Pili mizani ya majibu yake inahitaji tafakuri pana na ya nera zaidi.
 
Hivi ni nani yule aliimba: kumbe CCM waongo, au nilikuwa naota? Nayachukia haya maCCM.
 
Hakuna mwana chadema anayependa zitto afe ila wanataka mikono ya ccm inayomuelekea zitto ikatiliwe mbali ..
zitto ni kipenzi cha wana chadema hilo halina ubishi..wanachadema huwa wanasikitika sana wasiojua mienendo ya zitto....
wanataka kumuona zitto wao majukwaani,kwenye kila matukio ya chadema wanataka kumuona yupo ...hivyo ndo ilivyo mkuu...
zitto ni chadema na chadema ni zitto...
zitto + mbowe +dr.slaa == ushindi wa chadema 2015...

zitto + mbowe +dr.slaa== maumivu,kuchanganyikiwa kwa ccm
mbowe +dr.slaa - zitto == furaha na ahueni kwa ccm na mafisadi wote...
 
Bwana Mtela, Saanane na Shonza njooni huku mmevuliwa nguo hadharani na kila mtu anatazama viungo vyenu vya uzazi bila hata malipo!! Hongera kamanda Zitto kwa kuusema mtazamo wako hadharani, wengine wangefukia chini ya kapu.
 

LOGIC
wapo wale wawazao mema kuanzia nafsini mwao hadi kwenye jamii yao, hawa huitwa wenye hekima
kuna wale wawazao njama, visa,chuki, machafuko na hata vita,hawa tunawaita washenzi
''

CONCLUSION: ZITTO : MWENYE HEKIMA
DR.SLAA: MSHENZI

LOGICALLY PROVED.

ww unasemaje????????????????????????????
 
Mkuu Zitto,

Unaonanaje ungewaomba Mtanzania wakuombe radhi kwa kuandika habari nzito kama hiyo bila ridhaa yako?
Tena , unaonaje ukaitisha Press conference uwakane hao akina Shona & Co. kwamba huhusiani nao? Maana huko nyuma hujwahi kuwakana na mpaka leo wanakutetea kwa hali zote. Mie nadhani, badala ya kukanusha kijuu juu hivi uonyeshe kuchukizwa kwako na hilo kundi kwa matendo
 

Jamani wabongo tu wagumu kuelewa hata Kiswahili rahisi ama mantiki sahili kama hii! Chama ni taasisi au asasi ambayo inakamilishwa na ujumla wa mtu mmoja mmoja wawe viongozi au wanachama hata washabiki. Mimi ninafikiri ametaka kusisitiza kuwa huyo mtu mmoja mmoja ni binadamu ambaye anaweza kutenda makosa yake binafsi (hakutumwa na chama) kama walivyo binadamu wanachama wa CCM au CUF au hata wafanyakazi wa kampuni. Makosa binafsi ya mwanachama, kiongozi, mfanyakazi, nk yasichukuliwe kuwa ni makosa ya kitaasisi kama ambavyo inaelekea kuwa utamaduni wa kisiasa (siasa za majitaka) unaoibukia nchini bongoland!!
Pokea pongezi zangu Mhe Zitto kwa kulitolea suala hili ufafanuzi wa kuridhisha. Wewe ni mfano kwa vijana wanaowania kuingia katika siasa jinsi ulivyoanza, na unavyoendelea kukua na kuelekea kukomaa!
 
Ben saanane is typing.............

Ndugu jaribu kuficha husuda yako kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Kamanda Zitto keshatoa tamko,chapa kazi za kujenga taifa. BenSaanane anafahamu Zitto ni kiongozi wake hivyo anaelewa nini kifanyike kwa ajili ya kuimarisha afya ya chama. Time is money and remember 2014/2015 is around the corner,
 
Last edited by a moderator:
Hajamsfundisha bali amemshauri. Hakuna mtu asiyeshauriwa, huenda wewe utakuwa wa kwanza. Hata rais ana rundo la washauri.
Mkuu ni kweli hakuna mtu asiyeshauriwa lakini ushauri unatolewa pale mtu anapotaka ushauri, halafu pia kuna taratibu zake. sidhani kama Invisible ametaka huo ushauri.

Ni wazo langu tu.
 
Last edited by a moderator:
Matendo ya Lwakatare yasifanywe ni malengo ya taasisi.
 
Ben: 'Nimeshawahi kuonana na Zitto'
Zitto: '
Sijawahi kuonana na Ben'


Integrity: Sifa kuu ya kiongozi


Ukweli ndio msingi wa uaminifu kwa kiongozi. Kiongozi ni Yule anayesema ukweli siku zote na sehemu yoyote.


Nimegundua kitu kimoja ndani ya CHADEMA: Baadhi ya viongozi si wa kweli.

Ni nani mkweli kati ya Zitto na Ben Saanane?

Kwa vile wote hawawezi kuwa wakweli, what is the future of politics in our country and CHADEMA in particular?

Ikiwa mmeanza kuwa waongo ndani ya chama chenu, mtakuwa wakweli kwa taifa?
Kwa vile wote hawawezi kuwa wakweli, what is the future of politics in our country and CHADEMA in particular?

Ikiwa mmeanza kuwa waongo ndani ya chama chenu, mtakuwa wakweli kwa taifa?



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…