Siri ya dada wa kazi na mume wa boss wake ni nzito

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Fanta Baba yake alikuwa balozi, makazi yake yote alisoma kwenye shule za kimataifa. Kwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa darasani chuo kikuu alipata ufadhili Harvard Marekani kwa utaratibu wa shule yao.

Alihitimu shahada ya Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa. Alipata ajira Umoja wa Mataifa kama msaidizi mwanafunzi huku akiwa anasoma shahada ya uzamili. Huko kazini alikutana na Jeff muandishi wa habari. Alifungua ndoa na Jeff na kupata mabinti wawili.

Ajira ya Fanta baada ya kumaliza shule ilikuwa na majukumu mengi ya safari. Alitafuta binti wa kulea watoto wake. Dereva wake Simon alimletea binti aliyemaliza darasa la saba. Binti alifundishwa kizungu kwani watoto ndani ya nyumba walimwaga yai. Alifundishwa pia kuwatengenezea watoto mlo kamili yaani lazima kuwe na nyama wanga na mboga za majani pia umuhimu wa kuwapa watoto matunda na maji.

Fanta alisima shahada ya uzamifu na muda mwingi hakuwa nyumbani. Jeff alilea watoto na dada wa kazi. Watoto walikuwa na walitumia muda mrefu shuleni. Jeff akiwa anafanyia kazi nyumbani muda mwingi wa editing na kuwasiliana na kazini kwa internet. Jeff alianza mapenzi na dada wakati huo dada amekuwa mwari wa kupendeza na Fanta anamnunulia nguo maridadi.

Jeff alimpa mimba dada wa kazi, ilibidi aache kazi lakini Jeff alimuahidi kumtunza. Alimpa shilingi laki tano kila mwezi mpaka amejifungua. Alijifungua mtoto wa kiume. Jeff alifurahi sana kwani kwao yeye alikuwa mtoto pekee.

Jeff alimuomba dada Fanta asiyajue haya ya mtoto. Aliwajengea wazazi wa bint nyumba ya kisasa kijijini kwao. Aliahidi kumtunza mtoto na kumsomesha.
 
Hadithi hiiinatufundisha nini?
Ina mafunzo mengi;
1. Wanaume wengi wakikosa mtoto wa kiume kwenye ndoa watamtafuta nje ya ndoa.

2.Wanaume ni wachawi, binti aliyekuja kwako akiwa 15 unaweza kulala nae akiwa mkubwa?

3. Jalala la tajiri si sawa na la maskini. Mume wa Fanta aliwatoa wazazi wa dada kwenye umasikini ingawa uhusiano wao ulikuwa si halali.
 
story zako hua fikirishi na hutuacha na ham yakutaka kujua zaid bt bahat mbaya hakuna mwendelezo wala nini
 
Ina mafunzo mengi;
1. Wanaume wengi wakikosa mtoto wa kiume kwenye ndoa watamtafuta nje ya ndoa.

2.Wanaume ni wachawi, binti aliyekuja kwako akiwa 15 unaweza kulala nae akiwa mkubwa?

3. Jalala la tajiri si sawa na la maskini. Mume wa Jeff aliwatoa wazazi wa dada kwenye umasikini ingawa uhusiano wao ulikuwa si halali.
1 na 2 ndio lengo la hii habari? Amelaumiwa mwanaume.

4. Kadiri vyeti vinavyoongezeka, ndivyo maarifa ya kuishi yanavyopungua.
 
Ndio tamati au Kuna sehemu ya pili?

Fanta alijua kuwa mumewe kamnanihii dada wa kazi?

Nani mbaya kati ya hao watatu?

Naomba majibu mama akee
 
Back
Top Bottom