Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Binafsi mimi naona kijana kakosea, huenda alikuwa sahihi kumuacha ila namna alivyomuacha alikosea, ilibidi amuache kivingine, mkasa huu hapa nawapeni.

Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Hapa sasa nitaongea zaidi kama yeye mwenyewe alivyojitetea, ndipo penye kuamua kazingua au lah, twendeni pamoja.

Kijana ni kama alipata mstuko akataka kumuacha binti kienyeji ila alishindwa, ikabidi amuweke wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, alimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata ulemavu muda wowote maana hujafa hujaumbika, pia mtu yoyote anaweza kupata mtoto mlemavu maana hakuna anaemuumba mtoto atakavyo lakini yeye anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi endapo wao wakipata mtoto kwa kuhofia kwamba ulemavu wa wanafamilia ni magonjwa ya kurithi, hivyo hata kama binti ni mzima yawezekana karithishwa genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu, sababu ya zaida ambayo hakumwambia binti ni kwamba anahofia kuna mambo ya kiafrika kwenye mila au matambiko yaliyowahi kudanyika huko zamani yanarithishwa,

Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.

Je, ni sawa?
 
Huyo jamaa ni wewe sasa...Yapo maradhi ya kuambikizwa ila ulemavu sio kwa sana ...

Binadamu anayeishi basi mda wowote anaweza kupata ulemavu...Inaweza kuwa yupo sawa kama hao watu wamezaliwa hivyo ila kwa sasa tatizo kama maskini ni hatar vijana wanalipata bila ya kujua.
 
Huyo mtoto hamjui Mungu
Hapana, kusema hvy sio sahihi.

Hivi ni familia ngapi zenye watoto walemavu bado wapo pamoja?

N kwann mara nyingi baba hukimbia ikiwa mke wake atapata mtoto mlemavu?

Kwa upande wangu jamaa yupo sahihi kwa 55% na hayupo sahihi kwa 45% mana ni afadhali hayo maamuzi yake kuliko kuja kukimbia familia kisa mtoto ni mlemavu.
 
Kuna kijana wa kiume miaka 26 alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Kijana akamkimbia mwenzake na kumuweka wazi kwamba anampenda lakini hawezi kurisk kumuoa kwasababu anahofia alichokifundua kwenye familia anayotokea huyo binti, sababu yake kuu anahisi huenda magonjwa hayo yapo kwenye kizazi cha binti na huenda watoto wakayapata, hivyo kamwambia binti anachukua tahadhari

Binti kabaki analia sana bila kujua cha kufanya

Je, ni sawa ?
mapenzi huwa ni upofu ukipenda haswa,huyo hakumpenda binti vilivyo, alikuwa mguu mmoja sawa mguu mmoja upande mguu mmoja ndani mguu mmoja nje!
 
Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Kijana akamkimbia mwenzake na kumuweka wazi kwamba anampenda lakini hawezi kurisk kumuoa kwasababu anahofia alichokifundua kwenye familia anayotokea huyo binti, sababu yake kuu ni kwamba mtu yeyote anaweza kupata mtoto mlemavu lakini anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi akimuoa binti anaetokea familia yenye walemavu, hivyo kamwambia binti anachukua tahadhari

Binti kabaki analia sana bila kujua cha kufanya

Je, ni sawa ?
JF Imekuwaje siku hizi ? Jarida la mipasho utoto ujinfa tuu mambo personal ....sio ile mijadala ta kukuza nchi na vision 2030 to 50 yaanii nadhani JF ya $$ subscription ni muhimu na lazimaa....
 
Kosa alilolifanya Ni kumwambia( kuropoka) kwa Nini anaachana naye, angetafuta tu njia ya kuachana naye tu kiaina kwa ustaarabu bila binti kujua, Hata wazee wa zamani walikuwa wanafuatilia familia ya mtu mnaetaka Kuoana nae, Kama familia Ina changamoto walibadili maamuzi na ilisaidia Sana kuepusha changamoto mbalimbali.
 
Back
Top Bottom