Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Pamoja na kujinasabahisha na wasomi, Ukweli ni kuwa kinachowasaidia ni uwepo wa wanasheria Manguli nchini ndani ya chadema kwani kesi zote wanazotupiwa wamekuwa wakizishinda na wanaposhinda inazidi kuwaongezea huruma kwa wananchi kuwa wanaonewa na MACCM.
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.

What a dream!
 
Leo umeamua kuja na verified Id yako badala ya ile unayokuja nayo kila mara hapa. Naona umeamua kujipigia chepuo la kisiasa na kujiandaa kwa uongozi kanda ya Mashariki.
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.

Wewe wasema.Mimi,Yeye,Yule na mwingine wanasemaje?.
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.

Kazi kubwa ni kuvunja propaganda za Ccm.Chadema wakifanikiwa katika hilo kitu kinatinga magogoni kiulaiini kama vile kumsukuma mulevi.
 
Hongera nyingi kwa viongozi wote wa CDM na wanachama nchi nzima kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuikomboa nchi toka mikononi mwa Serikali dhalimu.

Alutta continua! continua!
 
Mkuu Mselewa umemaliza kazi yako ngoja waje wazee wa lumuba watakavyo tokwa na mapovu........
 
CHADEMA sasa ni zaidi ya chama kikuu cha upinzani nchini. Bungeni ikiwa na Wabunge 48 ambao ni sawa na asilimia 13.445 ya Wabunge wote 357,inafanya mambo makubwa. Inabuni,inahoji,inajenga hoja na kuomba miongozo ya Spika mambo yanapokwenda mrama. Nje ya Bunge ndio usiseme. Mikutano ya kueleza ukweli na ya kujadili mstakabali wa taifa inafanyika kwa ubunifu,ufanisi na mafanikio makubwa. Sasa imejijengea heshima na uaminifu mkubwa kwa wananchi. Inasubiriwa kutwaa dola. Siri ya mambo haya ni tatu. Kwanza,imesimama yenyewe. Inapambana na yeyote anayeweza kupambana nayo kisiasa. Haiogopi. Pili,inatumia kila nafasi ijitokezayo ipasavyo. Si nje wala ndani ya Bunge. Pia,ina uongozi bora uliojaa ubunifu,busara na uwezo.Natamani na kutumai kujiunga nayo nikijiunga siasani...

Hilo halin ubishi...umetisha
 
Mkuu, siasa za kung'oana kucha zipo ndani ya cdm. Hata dr slaa analijua hilo isipokuwa ameamua kusema uongo kwa makusudi kwa kuisingizia ccm. Muda si mrefu wataumbuka

Waliong'olewa kucha wamesema kuwa wameng'olewa na vyombo vya usalama ambavyo viko chini ya Ccm wamethubutu hadi kuwataja kwa majina.Ninyi ambao hamjang'olewa kucha wala kutolewa macho munajifanya kuwa muliwaona Chadema wakifanya hivyo.Kawadanganyeni mabwege wenzenu wengine hatudanganyiki wengekuwa ni Chadema wanafanya hivyo mungewaacha wakati munaomba usiku na mchana ili CHADEMA kife.
 
nchemba hana lolote bana tunataka alete jipya na si kung'oa watu kucha na meno
 
Mkuu, jana waziri nchimbi kawabomoa sana. Sijui kama watakuwa na pa kutokea

Nchimbi ni mbunge hoyahoya hana umaana wowote.Mtu asiye na adabu hata kwa wapiga kura wake hapa songea atakuwa na hoja gani zaid ya kujipendekeza.Kuna mtu kilaza toka darasni hadi nje kama emmanuel?na hapa mjini harudi tena labda aende kwao Mbeya na huko nadhani watamtoa balu
 
Mnyika tu ni zaidi ya wabunge 150 akiwemo nchemba jumlisha mawaziri 10 jumlisha katibu mkuu wa magamba jumlisha wakuu wa mikoa wote na wale wa wilaya wa bara na visiwani jumlisha mabalozi wote jumlisha yule wa uenezi mnape jumlisha rais vasco da gama JUMLISHA USALAMA WA CCM. Endelea kujumlisha ili uone ubora wa mbunge mmoja wa CDM, UKICHUKUA KATIBU MKUU WA CDM NDO USISEME.
 
Nchimbi ni mbunge hoyahoya hana umaana wowote.Mtu asiye na adabu hata kwa wapiga kura wake hapa songea atakuwa na hoja gani zaid ya kujipendekeza.Kuna mtu kilaza toka darasni hadi nje kama emmanuel?na hapa mjini harudi tena labda aende kwao Mbeya na huko nadhani watamtoa balu

acha uongo, kuanzia bombambili, ruvuma, majengo, matalawe, msamala nk. Wote bado wanampenda. Hata kura ya diwani wakupe wewe lakini ya ubunge yake. Mwambie na mpeni ujumbe Mbogolo kuwa NCHIMBI ni tingatinga.
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.

Umesha ingiza buku 7
 
CHADEMA wamejipanga sio siri , CCM inabidi wafanye kazi ya ziada kwa kufanya siasa za kistaarabu., Gutter politics haziwezi kuwasaidia watz wa sasa wameamka.
 
Usimdhihaki MWenyezi Mungu kiasi hicho. Mungu hana ushabiki wa siasa. Labda kama slaa ndo mungu wenu

Unajidanganya..Yupo sahihi kabisa!Mungu hubariki chenye haki,Mungu huchukia udhalimu,alimuumba mwanadamu na ajitambue umuhimu wa uwepo wake duniani,istoshe Vyote vijazavyo ulimwenguni ni mali ya Mungu ikiwamo siasa.kwakukusaidia tu ni kwamba Jeshi la haki halijawahi shindwa tangu Dunia kuumbwa.ukitaka kufahamu zaidi kamuulize Farao na majeshi yake.

A lie has speed,but truth has endurance
 
Back
Top Bottom