Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

CHADEMA sasa ni zaidi ya chama kikuu cha upinzani nchini. Bungeni ikiwa na Wabunge 48 ambao ni sawa na asilimia 13.445 ya Wabunge wote 357,inafanya mambo makubwa. Inabuni,inahoji,inajenga hoja na kuomba miongozo ya Spika mambo yanapokwenda mrama. Nje ya Bunge ndio usiseme. Mikutano ya kueleza ukweli na ya kujadili mstakabali wa taifa inafanyika kwa ubunifu,ufanisi na mafanikio makubwa. Sasa imejijengea heshima na uaminifu mkubwa kwa wananchi. Inasubiriwa kutwaa dola. Siri ya mambo haya ni tatu. Kwanza,imesimama yenyewe. Inapambana na yeyote anayeweza kupambana nayo kisiasa. Haiogopi. Pili,inatumia kila nafasi ijitokezayo ipasavyo. Si nje wala ndani ya Bunge. Pia,ina uongozi bora uliojaa ubunifu,busara na uwezo.Natamani na kutumai kujiunga nayo nikijiunga siasani...

mwalimu:sema pipoz
wanafunzi😛iiiipoooozzzz........
 
Mnyika, Lissu, Msigwa na Zitto Vs Wabunge wote wa CCM. Jamaa wanajua sana haisee
 
Unazungumzia bingwa wa kuzusha, Nchemba ni mahili kwa kuzusha, atuambie zile tuhuma zake za kutishiwa kuuwawa na wabunge wa chadema ziliishia wapi? mbona hatujaona wakihojiwa na polisi?
 
mungu gani anabariki vurugu, fujo na kung'oa watu kucha? Labla mungu wa CHADEMA huyo sio mungu wa mbingu na ardhi.

Mkuu ni dhahiri njaa yako sasa imehamia kichwani, kiasi ambacho uwezo wako wa kufikiria upo mashakani. Vipi mmeshatoka kwenye kikao cha kutaka kumnusuru DENTIST ?

Mkuu naona unajitahidi kutafuta posho ya kuishi mjini, kuna mdau mmoja kanitonya ati leo ni public holday, mnalipwa double, hivyo itakuwa sh. 14,000/= badala ya sh. 7,000 /= kwa kila post.
 
kila mtu anaona ni kweli bungeni chadema inafanya fujo,kuvuruga wenzao wasichangie kwa uhuru,kuleta hoja za uongo,uchochezi,kuzungumzia maswala yaliyomahakamani,kuchochea udini nk.
 
Mbunge mmoja wa CDM ni sawa na wabunge 50 wa CCM.

50 haiwezekani kwa bunge hili la bi kiroboto namsimamisha Lissu na wabunge wote wa CCM na maspika na AG,wakitenda haki kwenye mijadala anawatoa KO
 
Kabisaaa Chadema isingekuwa wapinzani wala wasingekuwa wanakamatwa viongozi wao mara kwa mara na kuwapeleka mahakamani,mbona Cuf au TLP viongozi wao hawakamatwi??sasa hapo ndio muone CCM imekalia kuti bovi na lazima watoke kwenye madaraka....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hakiwezi kushika dola kwa mwenendo huu kwakweli tusidanganyane tuliowengi ni mashabiki na sio wanachama wala sio wapiga kura!!!
Tushukuru CDM wapo.wasingekuwepo dowans,epa,kinana tembo,richmond,radar,nchi nzima kufeli 4m 4.ongezea list.Tungejuaje yote haya?tafakari mh masaburi
 
Hakiwezi kushika dola kwa mwenendo huu kwakweli tusidanganyane tuliowengi ni mashabiki na sio wanachama wala sio wapiga kura!!!

arusha mlisema hivyohivyo........idiot
 
kuna watu watakuja mbio wakijua kuna siri umewawekea.
 
Ongelea nafsi yako kwani watu wengi tunaipenda cdm na tutajiandikisha kwa ari kwenye daftari la wapiga kura mwaka huu
 
Back
Top Bottom