Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

CHADEMA sasa ni zaidi ya chama kikuu cha upinzani nchini. Bungeni ikiwa na Wabunge 48 ambao ni sawa na asilimia 13.445 ya Wabunge wote 357,inafanya mambo makubwa. Inabuni,inahoji,inajenga hoja na kuomba miongozo ya Spika mambo yanapokwenda mrama. Nje ya Bunge ndio usiseme. Mikutano ya kueleza ukweli na ya kujadili mstakabali wa taifa inafanyika kwa ubunifu,ufanisi na mafanikio makubwa. Sasa imejijengea heshima na uaminifu mkubwa kwa wananchi. Inasubiriwa kutwaa dola. Siri ya mambo haya ni tatu. Kwanza,imesimama yenyewe. Inapambana na yeyote anayeweza kupambana nayo kisiasa. Haiogopi. Pili,inatumia kila nafasi ijitokezayo ipasavyo. Si nje wala ndani ya Bunge. Pia,ina uongozi bora uliojaa ubunifu,busara na uwezo.Natamani na kutumai kujiunga nayo nikijiunga siasani...

Mkuu Petro, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, ila napenda kuongezea ya kuwa siri nyingine ya mafanikio ya CHADEMA ni kumtegemea Mungu wetu muumba Mbingu na Nchi.
 
7000 per day,maisha bora kwa kila mwana lumumba
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.

haya mmemwaga wengi sana sjui tuite lumumba fasta au nini make uwezo wenu ni mdogo sn hamjafundishwa hata kujenga hoja
 
Mkuu, umesahau kuwa nchemba tu peke yke anafanya viongozi na wafuasi wote wa cdm washindwe kulala usingizikucha

kweli kabisa make spidi yake ya kung'oa kucha hakuna asie iogopa hyu chemba
 
CCM wameamua kung'oa watu kucha na meno wakidhani eti ni kuimaliza nguvu CDM
Mkuu, siasa za kung'oana kucha zipo ndani ya cdm. Hata dr slaa analijua hilo isipokuwa ameamua kusema uongo kwa makusudi kwa kuisingizia ccm. Muda si mrefu wataumbuka
 
Mkuu Petro, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, ila napenda kuongezea ya kuwa siri nyingine ya mafanikio ya CHADEMA ni kumtegemea Mungu wetu muumba Mbingu na Nchi.

mungu gani anabariki vurugu, fujo na kung'oa watu kucha? Labla mungu wa CHADEMA huyo sio mungu wa mbingu na ardhi.
 
Mkuu, jana waziri nchimbi kawabomoa sana. Sijui kama watakuwa na pa kutokea

mwizi anakili kua alibeba mali za wizi, mtu na masharubu yake anarokeza hazarani na kua we hujabeba, yani ccm hamuishiwi vituko
 
Hakiwezi kushika dola kwa mwenendo huu kwakweli tusidanganyane tuliowengi ni mashabiki na sio wanachama wala sio wapiga kura!!!

hatuwezi kua na mwanachadema mbumbu hivi
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.



Sasa kwanini mnamuita padre ? au ndio mbinu yenu ya Mwisho? ....nashangaa CCM wamekua na hasira haijapata onekana!
 
Mkuu umesema ukweli usiopingika kama kuna wanaopinga basi hawa akili zao ni sawa na za maiti.Chadema ndio habari nchini na nje ya nchi.
 
kweli kabisa make spidi yake ya kung'oa kucha hakuna asie iogopa hyu chemba
Nchemba na lusinde wanatisha kweli. Ndo maana kila wakisimama kuongea akina lissu na mnyika hukimbilia kuomba miongozo ya spika ili kudisturb flow yao
 
Jiulize kwanini mchimbwa ooh sorry mchimbi na spika hawakutumia sheria za bunge kumtaka Rev Msigwa kusibitisha hicho nyie mlichokiita kuwa ni uongo
Mkuu, jana waziri nchimbi kawabomoa sana. Sijui kama watakuwa na pa kutokea
 
yaani mtu akiwa na mawazo tofauti na wewe ndo adui? Unalazimisha mawazo yako yawe mawazo ya wote?

Ni bora kuwe na restriction JF wale wote wanaopinga chama chetu wapigwe BAN



Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom