Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Mleta hoja, nimekuelewa mkubwa. Vidole vyangu viwili ( Shahada na cha kati ) viko juu kwa ajili yako na sina hoja zaidi. Asante!
 
napatwa na wakati mgumu wanaposema chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.


kujipanga wapi bwana sisi ni wanajeshi hatujui lini vita vitatokea na hatujui ni lini vitaisha kwahiyo hatuogopi.
 
data alizozimwaga Lisu Bungeni leo kuhusu kubaka mchakato wa katiba kwenye mabaraza ya kata, wote wakibakia kimya hawakuamini; CDM inawasumbua sana CCM; waoneeni imani.

Sikusikia sauti ya kuomba mwongozo wa spika ili Lissu atoe ushahidi hakuna.
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.

Na wanaotoa mitusi kama Lusinde& Co na chama chao ndio wanaofaa kuongoza nchi kwa maono yako yako?
 
mungu wenu ni yule alienuniwa mbeya leo
MBEYA NI NOMA. Kwanza jamaa alipanga kukaa siku tatu. Wakatangulia na suti zao wakawa wanajaa kwenye mabaa, baadae wakajiona wako tofauti na jamii ya Mbeya hali ikawa ngumu kwao. Ghafla Mbeya FM radio ikandangaza kufupishwa kwa ziara, baada ya kuona upepo hauvumi kwao. Airport Songwe kulikuwa na ukaguzi wa kufa mtu kila mtu alikaguliwa kwakila kifaa walichoweza kukitumia. Alipofika Mbeya stadium [maccm wanaita Sokoine] akapunga mkono cha ajabu sana hata Kandoro hakunyanyua mkono. Mvua ikaharabu zaidi, akabaki na majukwaa yasiokuwa na watu. CDM wanapokuja hawatoi taarifa, lakini Uwanja wa Dk. W. P. Slaa, huwa watu wanakosa nafasi. Bahati nzuri Mbeya hata polisi wakikusanywa nchi nzima hawawezi kitu. Walifanya utafiti ikaonekana Watu wa hapa hawataki kuingiliwa mambo yao ndo maana hata Kandoro hasikiki kama ilivyokuwa DSM na Mwanza. Polisi wanaogopa raia coz wakileta fujo wanaweza kusakwa hata wanakoishi ndo maana hawasumbui. Arusha njooni mjifunze, Mbunge wenu hatakatwa kamwe.
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.
Hivi kama JK naye ameweza kuwa raisi je ni mtanzania gani atakayeshindwa kuongoza taifa lililojaa mbulumbulu kama wewe!
Kwa taarifa yako CCM hata ikitawala miaka mingine 50 hawataweza kubadilisha hali hii ya sasa. Maendeleo yanaletwa na wananchi wakikubali kushirikiana na uongozi na si viongozi peke yao. Wananchi wasipokuunga mkono huwezi kufanikiwa hata siku moja. CCM watu wameichoka na hawatoe ushirikiano tena badala yake ni kulaumiwa tu kila kukicha!
Chadema wanaweza kuleta maendeleo ya ghafla kwenye hii nchi kisa tu wanaungwa mkono na watanzania na watu wako tayari hata kushiriki katika shughuli yoyote ya maendeleo kama itakuwa ni kuiunga mkono chadema! Chadema hawatahitaji mapesa mengi kuleta mabadiliko ya haraka kwenye hii nchi maana nchi hii si masikini ila shida ni mfumo mbaya ambao unahitaji mabadiliko makubwa ambayo ccm kamwe hawawezi kuyafanya.
Watanzania hawahitaji kugawiwa pesa mifukoni mwao ila wanahitaji mfumo usiokuwa na rushwa na wenye kuwatendea haki na usawa wa kufaidi rasilimali zao kwa furaha ndani ya nchi yao. Chadema watafikia malengo yao kwa sababu ccm hawana ushawishi tena kwa watanzania wamejichafua wakachafuka sasa kila mtu anawakimbia!
 
Back
Top Bottom