Siri imefichuka.. Viongozi CHADEMA kuweni makini

Siri imefichuka.. Viongozi CHADEMA kuweni makini

Enzi Mike Tyson anawika kwenye masumbwi ungemwambia mtu kuna siku mbabe huyo angeelemewa ulingoni hadi afikie hatua ya kutumia meno badala ya ngumi nadhani hakuna mtu angeamini ama kusikiliza. Lakini hilo lilimtokea mbabe Tyson pale alipozidiwa kwa kila namna na Evander Holyfield na alipoona anapata umbuko la karne aliamua kutumia meno kwa kudhani angeondoa aibu kumbe ndiyo alizidi kuaibika.

CCM wamefikia pabaya kiasi cha kushindwa kupanga mambo mapya na ya maana zaidi ya kuaibika kwa matukio wanayopanga wenyewe na kuishia kuambulia matokeo hasi. Kama waliamini Arusha ndiyo wangemaliza kila kitu sasa hivi ile damu iliyomwagika inaanza kuwarudi na siku sio nyingi wataanza kuumbuana wenyewe.
 
Move ya hii ya kichina itagoma kama zile nyingine

move ya 1--kwamba cdm ina plan ugaidi-ft mwigulu (haina mauzo sokoni na imeshadoda)

move ya2-- wanatengeneza bomu kuua wananchi ili kusingizia cdm--ft same actors (hili move lilidoda siku hiyo hiyo lilipozinduliwa)

move ya 3---wanaleta kesi ya tindikali ili kuwashitaki viongozi wa juu---(move limedoda tayari hata kabla ya kutoka kwenye production)

move ya 4... coming lakini litadoda kabla ya production

move ya 5.....grrrrrrrrrrrrry (ccm wanaangukia pua na wananchi wameshawashtukia)
 
Asante mkuu,

Hata mimi nilishastuka toka jana baada ya kusikia Kileo amepelekwa kusikojulikana. Mapambano yanapofikia hatua kali mara nyingi upande unaoelemewa hujaribu kutumia mbinu chafu, hii ikiwa mojawapo. Tuendelee kuhabarishana, lakini ninaamini hata wafanye nini, ukombozi wa Mtanzania umekaribia!

Waingereza wanausemi ya kuwa 'It gets the darkest just before sunrise!'

Nimekugongea Like !
 
Hivi ccm hawapo tena watu wanaofikiri kwa kutumia vichwa tena,

Yaani move kama hizi wanajichoresha live kwa kila mtu kwamba wanatafuta jinsi ya kujificha kwenye uovu waliofanya Arusha

Wangekuwa wajanja wangepanga hii move baadae kidogo ili watu wasiunganishe na hii ya Arusha.
Swala la kuiunganisha na issue ya Arusha ni ushahidi tosha wa ushiriki wa ccm kwenye maovu kwenye taifa hili

Nashauri Dr. Slaa na Mbowe waombe Hifadhi ubalozi wa Rwanda kwa muda na waeleze wazi umma,

Nashauri pia viongozi wote wachadema ambao wanatishiwa maisha na hawa wezi wa taifa, wajisalimishe kwenye balozi za nje na kutangazia umma mbinu hizi mbovu,

Ccm ni janga la sio tu la taifa, bali ni janga la ustawi wa mtanzania.

Mkuu Mbona sikuelewi Vizuri.Rwanda si Wanatuponda kwa Ushauri tuliowapa?Sasa Dr.Slaa akiomba hifadhi kwenye Ubalozi wao si ndio Watazidi kutukebehi?
 
Mkuu Mbona sikuelewi Vizuri.Rwanda si Wanatuponda kwa Ushauri tuliowapa?Sasa Dr.Slaa akiomba hifadhi kwenye Ubalozi wao si ndio Watazidi kutukebehi?

Afadhali kuomba hifadhi kwenye ubalozi ambao hawana close friendship na Tanzania hasa with president, watakuwa hawayumbishwi nyuma ya pazia.
We angalia Asange alikoenda kuomba hifadhi, na hata huyu jamaa aliyelikisha program mpya naye anaelekea huko huko Ecuador kupitia Urusi (ambayo haifungamani na marekani)
 
jaribio la kubambikiza ugaidi limeshindikana sasa wanarudi kwenye uhaini. Roho ikitaka kutoka ni tabu sana
 
UWT wanaripoti kwa CDM

"To know the enemy is half the victory"
 
Afadhali kuomba hifadhi kwenye ubalozi ambao hawana close friendship na Tanzania hasa with president, watakuwa hawayumbishwi nyuma ya pazia.
We angalia Asange alikoenda kuomba hifadhi, na hata huyu jamaa aliyelikisha program mpya naye anaelekea huko huko Ecuador kupitia Urusi (ambayo haifungamani na marekani)

Nimekuelewa Mkuu.Tanzania ndipo tunapoelekea.Wanamapinduzi Wengi waliishi Uhamishoni.Ni mambo ya kawaida sana kama unapambana na Serikali inayotumia Mkono wa Chuma,kwa hiyo CDM watafakari na kuufanyia kazi Ushauri uliowapa.
 
Uoga ni ugonjwa mbaya sana ndo wanachoonesha chama tawala hapa.wanaogopa sana chadema.hamuwapunguzii chochote.sema nitafurahi kama na waliowaua watu wa chadema igunga na arumeru na arusha,moro nao wakamatwe.hamna taaluma ya kipuuzi na ya kipambe kama polisi na tiss nchini tanzania..mwanangu sitamshauri kujiunga na mfumo huu wa usalama wa kujidhalilisha.
Mifano tunayo ya polisi kufanya upuuzi kama chagonja alivyotoa kuhusu mwangosi kabla picha hazijawekwa mitandaoni,na baadhi ya polisi kufanya mda mfupi kabla ya kustaafu
 
Washaurini viongozi wenu mpaka sasa watakumbukwa wachache kwa ubora na ufanisi,mtakufa na mtaacha watoto ambao hawatowakumbuka kwa kingine bali uonevu na wizi
 
Uoga ni ugonjwa mbaya sana ndo wanachoonesha chama tawala hapa.wanaogopa sana chadema.hamuwapunguzii chochote.sema nitafurahi kama na waliowaua watu wa chadema igunga na arumeru na arusha,moro nao wakamatwe.hamna taaluma ya kipuuzi na ya kipambe kama polisi na tiss nchini tanzania..mwanangu sitamshauri kujiunga na mfumo huu wa usalama wa kujidhalilisha.
Mifano tunayo ya polisi kufanya upuuzi kama chagonja alivyotoa kuhusu mwangosi kabla picha hazijawekwa mitandaoni,na baadhi ya polisi kufanya mda mfupi kabla ya kustaafu

Maneno aliyoyazungumza Mwigulu kabla ya tukio la mlipuko, kama uchunguzi ulikuwa objective angetakiwa awe mtu wa kwanza kukamatwa,

Matunda ya vijana wa Mwema aliowatuma kuchunguza bomu, wakaishia kwenda kuchunguza vitu vya miaka mitatu ambavyo wao wao ndio walifanya
 
jaribio la kubambikiza ugaidi limeshindikana sasa wanarudi kwenye uhaini. Roho ikitaka kutoka ni tabu sana

Hata Juma Duni Haji (et al) wa CUF aliwahi kubambikiziwa hii Kesi na CCM-Zanzibar Enzi za Komandoo Salmin Amour.Mungu alivyo wa Miujiza hivi sasa Komandoo ni Kipofu na anahudumiwa Macho yake na Juma Duni Haji kama waziri wa Afya.
 
Katika mazingira ya kushangaza sana jana Mwanasheria mkuu Werema aliongelea kuhusu watu 200 walioficha fedha Uswiss.Huko nyuma aliwahi kuulizwa na kukataa kusema lolote, jana kaja na habari nzuri kabisa eti tume imefikia mahali pazuri!!

Hizi ni jitihada za kuondoa umma katika tukio la Arusha ambalo linaiandama serikali ya CCM kikamilifu.
Wameshindwa kumshtaki Mbowe kwa ''obstruction of justice'' maana kama ana mkanda anapaswa kuufikisha katika vyombo vya sheria.

Ninasikitika sana kuwa badala ya kutafuta chanzo cha tatizo(kama ni tofauti na dhamira zao) wao wanatafuta kufuta ukweli juu ya damu za watu.

Kama haya yasemwayo ni kweli basi kitu kinachoitwa ''crisis management ndani ya usalama wa taifa hakipo''
Na jinsi wanavyopindisha mambo ndivyo ''kitanzi'' cha Arusha kinavyowabana.

Ningewashauri waachane na hili la Igunga kwanza kwasababu kwa mtu mwenye kutumia akili na logic, Igunga inakioleza moto. Ni rahisi sana kuunganisha dots na itarudi kule kule Arusha.

Ikirudi Arusha itaunganika na Olisaiti kwasababu yote ni mabomu ya China. Itaendelea kurudi nyuma kwa akina Ulimboka, Mwangosi(RIP) n.k.

Hivi hawajajifunza kutoka sinema ya Kova ilivyokwama hata kabla ya kuingizwa katika jumba la sinema?
 
atutakubali kiraisi kiivo kupelekeshwa na magamba.
 
Serikali imepewa licence to kill na mataifa ambayo wanashirikiana kutuibia ikiwemo marekani ndo maana there is no coverage kabisa kuhusu matukio yanayotokea na uonevu wa kisiasa
 
Back
Top Bottom