Siri 5 Mauaji Msikitini

Siri 5 Mauaji Msikitini

Kuhusu kuvaa Suruali fupi au kanzu fupi lengo ni kwamba,unapovaa kanzu ndefu, Kanzu ndefu huanza kuburuza na kuchuka uchafu na hasa najisi kama vile mikojo barabarani au uchafu wa aina nyingine kote huko njiani utakapo pita, na hata Suruali ndefu ni hivyo hiyo,

so,kwa matokeo hayo ya kuvaa Kanzu/Suruali ndefu sana,ndio unajikuta unaingia kwenye Nyumba ya Ibada au unasali huku ukiwa umevaa nguo chafu na hasa "najisi"

Bila shaka nafikiri utanielewa kama hujajikoki kubishana tu!
Mbona waarabu wenyewe hawakati kanzu zao wala hawavai hivyo vipedo?
 
I'm sorry, nilifikiri Ww ni SHE, nimezoea maneno kama yako yanatoka kwa mdomo wa KE
Watoto wa kiume mliokaa na kinadada mnashida sana, ila kutetea kwako magaidi lazima ufuatiliwe tu.
 
Mimi nimesoma maelezo ya hao global lililofact ni kuwa watu wameuawa msikitini ila hizo sababu waluzoainisha global nahisi zina mushkeli huwezi kuua waislam ili ukawatetee waislam!
Na hapo ndio ile hoja ya hawa maluuni kuwa si waislam inapopata mashiko!
Wewe, hao ni wenzao kabisa, eti wamewasaliti, usilete urojo hapa
 
Huwa najiuliza waarabu ndo wangekuwa super power wa Dunia hii mfano kama Marekani, France, Uk, German, Russia, China, Japan nk. Wangeruhusu imani nyingine kweli nje ya uislam?
Waarabu wana roho mbaya sana
 
Kama una jicho la uono na fikra pevu utamaizi kuwa waliouliwa walikuwa Waislamu na walioua Si Waislamu. Watafutie dini ya kuwapa, regardless ya watakachosema hawana uislam na Uislamu hauwatambui.
Hizi ndo quotes za busara
 
Nafikiri ni wakati wa kuangazia makundi yote ya judo.Iwe msikitini ama nje ya hapo.Kama mnauana wenyewe sisi makafiri si mtatumaliza? Majudo ya nini nchini sisi sio wachina.
 
Waarabu wana roho mbaya sana
Wanao uwatu hapa tz ni waarabu wanao katakata maalbino wakiwa hai ni waarabu wanachuna ngozi kule mbozi mbeya ni waarabu walio uwa watu sengerema ni waarabu walichoma moto familia yote hapo dsm ni waarabu walio uwa mwnyekiti wa mtaa mwz ni waarabu wanauwa vikongwe huko kanda ya ziwa ni waarabu?
Kumbuka kila jamii ina watu wahalifu...
Burundi waafrica wanuwana congo, sudan, masumbiji, angola, naigeria,kenya, uganda kila sehemu za africa maiwaji ivi hayakuumi haya mawaji yanayo fanyika africa unaumia na mauwaji ya waarabu tu?
Jadili hoja bila chuki na toa maoni yako nini kifanyike kizuiya haya mauwaji ktk ardhi ya tz africa na dunia yote.
Yawezekana maoni yako yakawa dawa ya kumaliza mauwaji na uhalifu mwngine.
 
Wanao uwatu hapa tz ni waarabu wanao katakata maalbino wakiwa hai ni waarabu wanachuna ngozi kule mbozi mbeya ni waarabu walio uwa watu sengerema ni waarabu walichoma moto familia yote hapo dsm ni waarabu walio uwa mwnyekiti wa mtaa mwz ni waarabu wanauwa vikongwe huko kanda ya ziwa ni waarabu?
Kumbuka kila jamii ina watu wahalifu...
Burundi waafrica wanuwana congo, sudan, masumbiji, angola, naigeria,kenya, uganda kila sehemu za africa maiwaji ivi hayakuumi haya mawaji yanayo fanyika africa unaumia na mauwaji ya waarabu tu?
Jadili hoja bila chuki na toa maoni yako nini kifanyike kizuiya haya mauwaji ktk ardhi ya tz africa na dunia yote.
Yawezekana maoni yako yakawa dawa ya kumaliza mauwaji na uhalifu mwngine.
Hayo maarabu si ndio yana recruit na kuwa brainwash baadhi ya waislam kujiunga IS na kuchinja watu kama kuku.
Waarabu wana roho mbaya sana.
 
Nafikiri wanapenda mazoezi ukilinganisha wala nguruwe
kwahiyo hawa waliokuwa wanasali baada ya kumaliza mazoezi badala ya kwenda kuwatoa wenzao ulitaka wapewe adhabu gani na kaka gaidi????

Maana ni ujinga kupiga mazoezi. unaletewa taarifa wenzako wanaonewa wewe unaendelea kusali.

ACHA KUANDIKA KWA HISIA TUMIA AKILI.
 
kama kuna sheria inakataza kufanya mazoez nyumba ya ibada weka hapa,judo ni kwa ajil ya kujilinda na uonevu(vibaka) na kuweka afya safi
Ndio maana kaka gaidi alivyoingia ndani aliuliza swali moja.

Kwanini mnsali wakati wa mapambano kutafuta haki ya wenzenu.wala hujakosea mkuu na gaidi hakukosea pia.
 
kwahiyo hawa waliokuwa wanasali baada ya kumaliza mazoezi badala ya kwenda kuwatoa wenzao ulitaka wapewe adhabu gani na kaka gaidi????

Maana ni ujinga kupiga mazoezi. unaletewa taarifa wenzako wanaonewa wewe unaendelea kusali.

ACHA KUANDIKA KWA HISIA TUMIA AKILI.
Kwanini unaamini waliotekeleza mauaji hayo ni waislam? Kwani hujawahi kuona jambazi anaua halafu silaha anamshikisha marehemu ku-FAKE ionekane marehemu kajiua? Akili gani uko nayo...

Kwa akili yako hii wauaji mpaka sasa wameshafanikiwa malengo yao coz tension yote imehamia kuwasaka hao the so called Magaidi
 
Hayo maarabu si ndio yana recruit na kuwa brainwash baadhi ya waislam kujiunga IS na kuchinja watu kama kuku.
Waarabu wana roho mbaya sana.
Mkuu jitahidi kunisoma unielewe..
Waarabu wanayao na sisi waafica tunayetu.
Sasa nini tufanye ili sisi waafrica tuondokane na maovu yetu?
Ya waarabu waachie waarabu wenyewe kwanza tuanze na yetu tukimaliza ndio tutaenda kwa waarabu kuwasaidia njia tulizo tumia sisi ili na wao watumie.
 
View attachment 350761 View attachment 350760 View attachment 350763 View attachment 350762 View attachment 350764 View attachment 350765 View attachment 350766

Gaidi.


Na Waandishi Wetu, UWAZI

MANZA: Usiku wa kuamkia Mei 19, mwaka huu ni wa kukumbukwa kwa wakazi wa Ibanda Relini Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana kufuatia watu nane wanaodhaniwa ni magaidi kuvamia Msikiti wa Rahmani na kuua waumini watatu kwa kuwakata mapanga, sasa nyuma ya mauaji hayo kuna siri 5, Uwazi limechimba.

Watu hao walijitambulisha kuwa, wao ni wa kutoka Kundi la Islamic States ‘IS’ huku wakionesha bendera nyeusi yenye maandishi ya Kiarabu.

Ndugu muandishi wa #uwazi,Siri hizi 5 ulizipataje(chanzo chake tafadhali)
Uzi huu una pelekea maudhi ya imani za dini.

Watu wanatukanana sana,Mara wala nguruwe,huku wavaa vipedo aiseee!!
Kwa hiyo huyo kiongozi wa wauaji alikuwa mwanamke na akaingia sehemu ya wanaume ya kusalia?Huo msikiti hakuna wanawake?

NIMEVUTIWA NA HII NARRATIVE STORY.


Mjane

CHANZO CHA MAUAJI

Ilidaiwa kuwa, kundi hilo liliingia msikitini hapo na kuwauliza waumini hao ni kwa nini wanaswali wakati kuna wenzao wamekamatwa na polisi wa jijini Mwanza kwa madai ya ugaidi. Hivyo waumini hao hawakupaswa kuswali bali kwenda kupambana na polisi ili kuwatoa wenzao.

Tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi alishakiri kushikiliwa kwa watu hao wanaodhaniwa kuwa magaidi, lakini akatoa angalizo kwa wote wanaotaka kutumia nguvu kuwatoa watuhumiwa hao.



Polisi eneo la tukio

NI MKAKATI WA MUDA MREFU

Madai ya kundi moja kutangaza mkakati wa kuwatoa wenzao walio gerezani yalianza muda mrefu ambapo mwaka jana, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kaisi Bin Abdullah (mtazame ukurasa wa mbele amevaa ninja) alisambaza video akianika mkakati huo kama njia ya kulipa kisasi kwa wenzao wanaoshikiliwa nchini kote kwa madai ya uhalifu.

Mashuhuda wa tukio hilo.

Katika video hiyo, Kaisi alisikika akisema: Tumeshaungana ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu 17 walikamatwa kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga makosa ya ugaidi. 21 wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine 18 wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine 17 wameuawa Mtwara kwa amri ya …(anamtaja waziri).

“Subira yetu imefika mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa ahadi kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame. Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.”



MKUU WA JESHI LA POLISI ALITIA NENO

Baada ya kunaswa kwa video hiyo, waandishi wa Global Publishers walitia timu kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na kumkabidhi video ambapo alisema:

“Nawashukuru sana kwa kuleta video hii. Huu ndiyo ushirikiano unaotakiwa, nawaomba wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni kosa kuwa nazo na watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.

“Sisi kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya uhalifu kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni kwamba polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa kushirikiana na raia wema.”



UJUMBE WA KUTODHARAULIWA


Kwa mujibu wa chanzo chetu, siri ya kwanza ya mauaji hayo ilitokana na ukatili wa watu hao ambapo walionesha kuwa, endapo wasingemwaga damu, dhamira yao ya kutaka kuwakomboa wenzao polisi isingekuwa na nguvu.

“Wakati wanalazimisha waumini kulala, mmoja alisema; ‘lazima tumwage damu ili watu wajue hatuna utani. Tusipomwaga damu watatudharau hawa,’” alisema mmoja wa walionusurika akiwakariri watu hao huku akiomba hifadhi ya jina lake.



KUITISHA SERIKALI

Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye anasema aliwashuhudia watu wao wakiwa wanaondoka, alimsikia mmoja akisema; ‘serikali si inataka kuambiwa kwa vitendo, hivi ndivyo vitendo sasa. Hakuna kumwabudu Mungu mpaka haki ipatikane.’ (akimaanisha wenzao waachiwe).



WALITOA ONYO


Mmoja wa waumini wa msikiti huo ambaye pia hakupenda kuandikwa jina gazetini, alisema mauaji hayo yalifanywa na watu hao baada ya kuwatumia salamu mapema waumini wasisali lakini walipogundua watu wanasali wakaona wamepuuzwa.

“Tunasikia walituma ujumbe wa onyo tangu awali kwamba waumini wasisali washughulikie kuwatoa wenzao. Sasa walipobaini watu wameingia kuswali wakajikusanya na kuja kufanya mauaji wakiamini ndiyo dawa pekee ya maneno yao kufuatwa.

Naye kiongozi mmoja wa Bakwata Mkoa wa Mwanza ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa, kwa kawaida makundi ya watu wanaotumia mwavuli wa imani ya Kiislam kufanya mauaji, ni ya wale wanaopenda kuabudiwa kwa kile wanachokisema.


KUCHELEWA KUTII AMRI


Hata hivyo, siri nyingine ya tano ya watu hao kuuawa inadaiwa kuwa ni kuchelewa kutii amri. Inadaiwa kuwa, wakati magaidi hao wakiingia na kuamrisha watu kulala, wapo waliochelewa kutii wakitaka kujua kwanza wanaotoa amri hiyo ni akina nani na wana lengo gani!

“Karibia wote waliokatwa mapanga sana walichelewa kutii amri ya kulala. Walitaka kuwaona wale watu ni akina nani. Kwani lilikuwa tukio la kufumba na kufumbua. Na wao walipoona kuna ambao ni wagumu kulala, wakaanza kutembeza majambia mpaka kuua,” alisema muumini mmoja.

WALIBADILI SAUTI

Muumini mwingine wa msikiti huo alisema kuwa, sauti walizotumia watu hao si za asili kwani alimsikia mmoja wao ambaye huenda ni kiongozi, aliwasisitizia wenzake kuhakikisha wanabadili sauti ili wasibainike.

“Zile sauti hazikuwa zao. Naamini wale watu wanatujua na sisi tunawajua, nilimsikia mmoja akisisitiza kuhusu sauti. Alikuwa akisema; ‘sauti sauti, angalieni sauti zenu.”

SIRI YA KUFICHA SURA

“Ndiyo maana walificha sura kwa kuvaa ninja. Mbona majambazi kibao tu wanaingia benki kuiba bila kuficha sura? Wale sura zao si ngeni kwetu ndiyo maana walificha,” alisema muumini huyo.

WATOTO WAWILI WAZUA UTATA

Muumini mwingine aliyenusurika katika tukio hilo yeye anasimulia kwa kirefu tangu alipoingia kwenye mlango wa msikiti huo.

“Ilikua saa 2: 35 usiku nilipongia msikitini na kuwakuta watoto wawili wageni. Mmoja aliketi mbele mwingine nyuma. Kwa kawaida Waislam kuwa hatuulizani na kuwa na wageni wa kawaida, kumbe sivyo. Naamini walikuwa kwenye mpango.

“Baada ya muda nikasikia watu wakiingia na kutuamuru tusigeuke na tulale pale tulipo. Walimuulizia imamu wa msikiti, alipokosekana wakampata msaidizi, wakampiga shoka kichwani na kumcharanga sana huku wengine wakiendelea na mauaji, sisi tulifanikiwa kukimbia,” alisema muumini huyo.

MWINGINE HUYU

“Mimi nilifika msikitini saa 2:40 nikiwa nimechelewa, nikaenda kujipanga mbele. Wakati tunamalizia Rakaa ya mwisho, tukasikia watu wanaingia wakatuambia hapohapo mlipo laleni chini, wakasema wanamtaka imam. Mimi nilijua ni polisi kumbe siyo, wakamchukua Ostadh Feruz wakampiga bapa kwanza, alipopiga kelele wakamkata panga, lakini kumbe vipaza sauti vya msikitini vilikuwa wazi, wakavizima.

“Walizima taa na kuanza kumchinja Ostadhi tukiwa tunaona huku wakisema nyiye badala ya kupigana mnasalisali, mnasali nini kwanza mmetusaliti.

“Kiongozi wa kundi hilo alikuwa mwanamke, akaanza kuamrisha kwa kusema; ‘chinja na huyu.’ Alipofika mtu wa tatu, yule mwanamke akasema; ‘watoto wasichinjwe.’ Baada ya kusema hivyo mimi nikachoropoka na kuanza kupiga kelele, na wao wakaondoka.”

KISA CHA WALIOKAMATWA

Kutokana na eneo la Ibanda Relini kuwa nje kidogo ya Jiji la Mwanza, inadaiwa limekuwa likitumiwa kufanya mafunzo ya kigaidi kwa baadhi ya watu wa eneo hilo ambao walikuwa kwenye Kikundi cha Al Shabaab hivyo, baada ya jeshi la polisi kupata taarifa walifanya msako na kuwakamata watu kadhaa ambao ndiyo chanzo cha magaidi hao kuvamia msikitini na kuwaambia wenzao wasisali.

MKE WA MAREHEMU

Amina Salumu ni mke wa marehemu, Ostadh Feruz Ismail Elias, alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka nyumbani saa 2:15 kwenda msikitini kuswali lakini baada ya muda mfupi alisikia kelele za watu huku kukiwa na milipuko msikitini hapo.

“Lakini polisi walipofika eneo la tukio tayari mume wangu alikuwa ameshafariki dunia. Naiomba Serikali ijitahidi kuwakamata waliohusika na tukio hili ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Amina.

JESHI LA POLISI

Kutokana na tukio hilo kuvuta hisia za wengi ndani na nje ya Jiji la Mwanza, jeshi la polisi mkoani hapa kupitia kwa Kamanda Msangi, limesema waliouawa katika tukio hilo ni Feruzi Isamail Eliasi (27) kabila Muha, Imamu wa msikiti huo na mkazi wa Ibanda Relini, Mbwana Rajab (40) kabila Mbondei na Khamis Mponda (28) dereva wa kiwanda cha samaki na mkazi wa Mkolani.

Aliyejeruhiwa vibaya ni Ismail Abeid (13) mwanafunzi wa Shule ya Kiislam ya Jabari iliyoko Nyansaka, anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, Butimba.

Feruzi Isamail Eliasi (27) na Khamis Mponda (28) walizikwa Mwanza na Mbwana Rajab (40), alizikwa Tanga.

chanzo:
Global Publishers
 
Mbona waarabu wenyewe hawakati kanzu zao wala hawavai hivyo vipedo?
Unaongea usichokijua mkuu,waarabu wenye kuijua dini na kuifuata hawavai kanzu zinazoburula mji mzima kisha hizo hizo Kanzu wakaingia nazo Msikitini kuswali!!

Usiongee kitu usichokijua Mkuu, au pengine kwa vile umeona waarabu wawili watatu hapo mtaani kwako wanavaa kanzu ndefu basi ndio ukahukumu waarabu wote wako hivyo?!
 
Waarabu wana roho mbaya sana
waliotengeneza HIV wana roho nzuri?..waliochinja wahindi wekundu wana roho nzuri?..waliomwaga agent yellow vietnam wana roho nzuri,waliopga atomic japan?chinja aborigin australia?walioendesha vita vya msalaba?vita iraq,afganstan?
 
Back
Top Bottom