Siri 5 Mauaji Msikitini

Siri 5 Mauaji Msikitini

Mimi nimesoma maelezo ya hao global lililofact ni kuwa watu wameuawa msikitini ila hizo sababu waluzoainisha global nahisi zina mushkeli huwezi kuua waislam ili ukawatetee waislam!
Na hapo ndio ile hoja ya hawa maluuni kuwa si waislam inapopata mashiko!
 
siku zote sijawahi amini ktk Uislamu
Kama ambavyo waislam hawa amini ktk ukristo ama dini nyingine yoyote na kama ambavyo kutoamin kwetu hakupunguzi ama kuongeza chochote ktk dini yako ndivo kuto amini kwako hakutupungizii wala kutuongezea chochote ktk dini yetu kwa hiyo kua tu na amani ndugu hamna anayekuhitaji uamini uislamu
 
Huwa najiuliza waarabu ndo wangekuwa super power wa Dunia hii mfano kama Marekani, France, Uk, German, Russia, China, Japan nk. Wangeruhusu imani nyingine kweli nje ya uislam?
 
Huwa najiuliza waarabu ndo wangekuwa super power wa Dunia hii mfano kama Marekani, France, Uk, German, Russia, China, Japan nk. Wangeruhusu imani nyingine kweli nje ya uislam?
palikua na wayahud na wakristo wakat wa mtume katika dola ya kiislam,pana wakristo iran ya leo,misri..waislam wa tanganyika walimpokea na kumlea julius nyerere mkatoliki swafi,dhana yako tu ya uadui inakusumbua
 
palikua na wayahud na wakristo wakat wa mtume katika dola ya kiislam,pana wakristo iran ya leo,misri..waislam wa tanganyika walimpokea na kumlea julius nyerere mkatoliki swafi,dhana yako tu ya uadui inakusumbua
ina maana kila mtu anayeingia uislamu basi anawaona wengine kama adui???? au anaonewa au anasingiziwa???maana kauli hizi za eti chuki zimezidi,au ukiwa Mwislamu maana yake ni kuwa Mlalamikaji wa kuchukiwa na kuonewa???wake-up Bwana.
 
Nikweli,ila kwa wakati tulionao wa matukio ya kigaidi na mengineo,sio mbaya ikapitishwa sheria au zuio ya kuzuia mazoezi ktk nyumba za ibada, kwa mpenda mazoezi gym mbona zipo nyingi tu, wasizuie watu kufanya mazoezi, mazoezi kiafya ni muhimu, si wengine kupita week bila kuingia gym kupiga skwati na kulift weight akili na mwili haikai sawa,,
gym si wanalipia ? kama huna hela je ?
 
Kukataza watu kufanya mazoezi ni kukiuka sheria. A lot of evils out there polisi washughulikie kwanza kabla ya kuanza na mambo ambayo hayavunji sheia
Bora mchinjane wenyewe huko Misikitini.
Wahishaneni kwenda kula mabikra
 
Hili kundi lililoua watu wakisali sidhani hata kama wanaujua uislamu vizuri, kwahiyo wao walitaka wenzao wasisali ili waenda tu kushinda Polisi mpaka wenzao watolewe?

Kwa uislamu salaa inaweza kuachwa na mtoto mdogo,Mwenye matatizo ya akili,mwanamke anapokua kwenye siku zake (coz mwili unakua sio msafi) huwezi kuacha kusali kisa wenzenu wamefungwa!!

Unapofika wakati wa salaa ni lazima kusali, hata kama utakua unazama baharini ila unapofika muda wa salaa utasali japo kifikra bila vitendo kama vile kusujudu n.k na Mungu anakukubalia tu salaa yako,huwezi kuua wenzako eti kisa wanasali,

Wanajuaje hapo kwenye sala zao pengine hao waliowaua pia walikua wanamuomba Mungu awasaidie wenzao ili watoke jela kwa amani? Tusihukumu uislamu wote kwa vitendo vya vikundi fulani tuu,

Amani ni kitu cha thamani sana na ikipotea ni ngumu sana kuirudisha,tudumishe amani na tuungane wote kulaani hicho kitendo cha watu walio uawa bila hatia,

Mungu azilaze mahala pema peponi roho za marehemu wote...Amin
umeandika vizuri saana mkuu
 
Huwa najiuliza waarabu ndo wangekuwa super power wa Dunia hii mfano kama Marekani, France, Uk, German, Russia, China, Japan nk. Wangeruhusu imani nyingine kweli nje ya uislam?
Kwani hapo waliohusika ni waarabu ? mbona waarabu wapo wakristo , unawakumbuka tareq Aziz wa irak, boutros boutros ghaly(katibu mkuu wa zamani wa UNO)
 
Duh! Mbona inatisha sana!
Mtume Muhammad (SAW) anasema; "Siku za mwisho umma wangu utagawanyika katika makundi 73.Makundi 72 yatakwenda MOTONI,na kundi MOJA litakwenda PEPONI."
Anasema tena; "Jihadharini na walinganiaji walio katika MILANGO YA JAHANNAM."
Kwa hadithi hizi mbili,akina IS,Boko Haram,Al-Shabaab,Janjaweed na wengine wote duniani wenye kufanana na USHETANI wa magenge haya, HAWATAMBULIWI NA UISLAMU.Hadithi hizi zinawagusa moja kwa moja.
Mwenyezi Mungu ndio kaweka wazi kabisa kitakachowakuta kwa dhuluma kubwa wanayofanya.Anasema; "Mwenye kuua muumini kwa makusudi bila ya haki,malipo yake ni JAHANNAM.Na gadhabu za Mwenyezi Mungu na laana ziko juu yake,na ameandaliwa adhabu kubwa." (Quran; 4:93)
Kuhusu kuvaa Suruali fupi au kanzu fupi lengo ni kwamba,unapovaa kanzu ndefu, Kanzu ndefu huanza kuburuza na kuchuka uchafu na hasa najisi kama vile mikojo barabarani au uchafu wa aina nyingine kote huko njiani utakapo pita, na hata Suruali ndefu ni hivyo hiyo,

so,kwa matokeo hayo ya kuvaa Kanzu/Suruali ndefu sana,ndio unajikuta unaingia kwenye Nyumba ya Ibada au unasali huku ukiwa umevaa nguo chafu na hasa "najisi"

Bila shaka nafikiri utanielewa kama hujajikoki kubishana tu!

Kwa hiyo Mungu wenu huwa ananusa hiyo harufu ya uchafu?
 
Kuna haja ya kuzuia watoto wasiingie misikitini ili wasiuawe
 
Kuna haja ya kuzuia watoto wasiingie misikitini ili wasiuawe
Hilo sio jibu la kuzuiya uhalifu.
Ungesema kuna haja vyombo vya ulinzi kuimarisha ulinzi ktk sehemu zote za nchi.
Na zaidi wananchi kusaidia vyombo vya usalama ktk kufichuwa wahalifu.
Siamini kama misikitini tu ndio kunako fanyika mauwaji ukiangalia takwimu utaona sehemu nyingi za nchi kunatokea uhalifu ikiwemo mauwaji.
Na nivyema tunapo jadili mambo ya msingi yanayo husu mustakabali wa taifa na wananchi wake tuepuke mihemuko ya udini na ukabila.
Nchi hii ni wtz sio ya waislam wala wakiristo wala usidhani kama waislam wakiuwana wasio kuwa waislam watasalimika.
Unataka kuniambia tuhamishe watoto sengerema au hapo alipo uwawa mwenyekiti wa mtaa napo tuhamishe watoto?
Mm nadhani tuishauri serikali iongeze nguvu mashuleni watoto wasomeshwe elimi ya dini kwani hakuna dini inayo ruhusu uhalifu wa aina yeyote ile ili tuwe na misingi madhubuti ya maadili.
 
Hii habari ina harufu ya uongo kila pahali. Something fishy is going on in Tanzania sio ugaidi.
 
Huwa najiuliza waarabu ndo wangekuwa super power wa Dunia hii mfano kama Marekani, France, Uk, German, Russia, China, Japan nk. Wangeruhusu imani nyingine kweli nje ya uislam?
Mkuu ivi hujui kama kuna waarabu wakiristo?
Rejea kanisa la anglikana znz lilijengwa mwaka gani na ujenzi huo ulibarkiwa na utawala gani na waanglikana hao walipewa kiwanja cha kujenga kanisa hilo na utawala gani?
Ukishajua hilo itajuwa kama waarabu na waislam hawana chuki na wasio waislam.
Nenda oman nenda UAE 100% ni waarabu waislam lakini kaone makanisa na wakiristo wanavyo abudu kwa amani na utulivu.
Ondoa shaka yako ktk uislam hatuhimizwi kuwauwa au kuwachukia wasio waislam.
Na kiongozi wetu ktk iman mtume muhamad (saw) ametuhimiza kuishi kwa upendo na watu wasio waislam.
Usihukumu jamii nzima kwa uhalifu wa mtu au kikundi.
Mm leo siwezi kuhukumu kama ukiristo au wakiristo wanaruhusiwa kufunga ndoa za jinsia moja.
Lakini kuna wahuni wachache wanao tumia ukiristo kwa upuuzi wao.
Jiepushe na jazba na chuki sio tu kwa waislam hata kwa wasio waislam jifunze kujenga sio kubomowa.
 
Kwani hapo waliohusika ni waarabu ? mbona waarabu wapo wakristo , unawakumbuka tareq Aziz wa irak, boutros boutros ghaly(katibu mkuu wa zamani wa UNO)
Mkuu namaanisha mataifa(nchi) zao ndo zingekuwa super power, wangeruhusu imani nyingine zitamalaki Duniani? Siongelei mtu mmoja mmoja maana hata hayo mataifa super power niliyoyataja yana raia waislam wengi tu kama ambavyo umebainisha waarabu wakristu.
 
Mkuu namaanisha mataifa(nchi) zao ndo zingekuwa super power, wangeruhusu imani nyingine zitamalaki Duniani? Siongelei mtu mmoja mmoja maana hata hayo mataifa super power niliyoyataja yana raia waislam wengi tu kama ambavyo umebainisha waarabu wakristu.
Mkuu nchi nyingi za Kiarabu zina Makanisa na wanaabudu kwa amani kabisa,kwa mfano nenda Dubai ukaone kanisa lilivyo zuri la wakristo na huabudu bila bughudha,

Dini ya Kiislamu haimlazimishi mtu yeyote kua mwislam wala haimkatazi mtu kwa nguvu kuabudu anachokiamini,

Kuna nchi za kiarabu ambapo waarabu kibao ni wakristo, Nchi kama vile, Misri,Lebanon,Palestina,Syria e.t.c na wanaabudu bila kukatazwa na mtu,

Usiongee vitu usivyovijua kwa mihemko tu ya chuki zako binafsi kwa dini fulani.
 
Gazeti la Shigongo bwana, sasa hizo siri tano ndio ziko wapi?, wanageuza geuza maneno tu kuonekana wana kipya kumbe vyote vimeshaelezwa hapo awali
 
Back
Top Bottom