Sipendi kuitwa wa "Mkoani".

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,713
12,063
Utasikia naenda au nahamia 'mkoani' ivi ni wapi huko?! Hii dharau inatokana na nini?
Dar sio mkoa?
Kama ishu ni jiji, mbona hata mkiwa mnaenda Tanga, Mwanza na Arusha mnasema mkoani?!
Hii dharau huwa siipendi kabisa. Ntakuja ua mtu.
 
Mie sipendi hasa wakazi wa Lindi Mtwara, Ruvuma huwa hawataki kutaja mkoa anaotoka utasikia natokea kusini huko. Hiyo sentensi imefanya hata watu wengi saas wanatumia utasikia watu wa kusini, kweli nachukia sana huo usemi, kwa nini usitaje mkoa rasmi au wilaya unajumuisha tuu eti kusini kwa nini?
 
na mie wa mashariki....loh
ila ni kutojiamini, kwa nini usiseme natokea songea?
 
Utasikia naenda au nahamia 'mkoani' ivi ni wapi huko?! Hii dharau inatokana na nini?
Dar sio mkoa?
Kama ishu ni jiji, mbona hata mkiwa mnaenda Tanga, Mwanza na Arusha mnasema mkoani?!
Hii dharau huwa siipendi kabisa. Ntakuja ua mtu.
weye ntu ya bara
 
Kuna wengine wakiwa wanaenda dar utaskia "NAENDA TOWN"

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: awp
What's in a name? Shakespeare aliuliza, hivi waridi lenye harufu nzuri likiitwa jina lingine litaacha kuwa waridi lenye harufu nzuri?

Wamarekani walivyokuwa wanajadiliana jina gani wamwite mkuu wa nchi yao, walipata matatizo sana.

Wengine wakataka kumwita Jaji Mkuu, wengine wakataka kumuita mtukufu, wengine wakataka kumuita mfalme etc.

Mwisho wakafikia makubaliano ya shingo upande kutumia jina la "President" kama jina la muda wakati wanatafuta jina la kudumu (by the way Bunge la House of Representative halijalipitisha jina hili permanently mpaka leo).

Mpaka wakati huo hakuna nchi duniani iliyokuwa inamuita mkuu wa nchi yake "President". Na Wamarekani walihofia kwamba ni jina lisilo na mvuto wala nguvu kiasi cha kumnyima kiongozi wao uwezo wa kushawishi.

Lakini kutokana na nguvu na ushawishi wa Wamarekani, tukaona nchi zote zenye mfumo wa uongozi unaofanana na wa Marekani hata kidogo tu zinaanza kuita mkuu wa nchi "President".

Habari hii inatufundisha nini?

Kama hupendi kuitwa wa Mkoa, fanyia kazi sababu zinazokufanya ujisikie vibaya kuitwa wa mkoa.

Mkoa ukiwa na maendeleo ya kutosha utaona sifa kuitwa wa mkoa. Msahau kwao mtumwa.
 
KWI KWI KWI! dar ndio haswaaaaaaa tanzania, hata zanzibar ni mkoa! yaani dar ni mambo yote, lolest! msinipige tu humu jamani! taratibu,
 
  • Thanks
Reactions: awp
Ulitaka uitwe mzawa??wa mkoa wa mkoa tu.mbona mkiwa unakuja dsm mnasema naenda 'town'

Haaa Nilienda Mkoa flani hivi sasa nikataka kupakiza magunia ya mchele na maarage sasa yule konda akaniambia hii gario inaenda town nikawa sijamuelewa kumbe town ndio dsm,wkt huku ukisema unaenda town means unaingia city center.....
 
kha! lakini hata tulio jijini mwanza huwa tunaiita mikoa kama tabora,shy,mara,kagera mikoa. . utasikia mtu asema hivi magari ya mkoani yashafika stendi? which means mikoa tajwa hapo juu. . .
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom