pole sana
matatizo yote haya yanatokana na hofu tuliyonayo katika maisha yetu. mtuanapokuwa na HOFU ni kwamba anakuwa ni kama mtu anyetoroka ukweli badala yakukabiliana nao. wengi tumekuwa na hofu zinazotokana na changamoto mbalimbali ambazo chache nikipata nafasi nitazieleza hapa chini ambazo zimechangia hiyo hofu tulio nayo.
hofu pia inatokana na matokeo mbalimbali yaliyotokea kuanzia kutungwa mimba kwetu mpaka maisha yetu ya sasa japo pia nafasi yetu kwenye familia, inamsukumo mkubwa sana katika hatua hii.
hii utupelelkea kuwa kwenye maeneo makubwa kama manne
- kuwa na rohoya kujilaumu/kuwalaumu wengine
- kuwa na roho ya kuhukumu
- huzuni
- kujikataa/kukataliwa
kwa bahati mbaya nafasi inanibana kwa sasa kuweza kueleza vizuri hayo yanatokea vipi lakini nafikiri kwa wakati mwingine naweza kueleza ila ndio chanzo cha mtu kujawa na hofu na mwisho kufikiria hata kujiua.
pamoja na maelezo mengi yaliyotolewa wachangiaji lakininafikiri twende nini kifanyike ili kuepukana nahali hii:-
- ujue ukweli na ukweli utakuweka huru
wengi wetu hatujui ukweli wa jinsi tulivyo mfano tulizaliwaje hii ni pamoja wazazi wetu walikutana katika mazingira gani wakati sisi tunatungwa mimba. hili linaweza kuwa swali la kijinga lakini lina maumivu kwawengi.pia maisha yetu katika hatua zetu za kukua na zenyewe ni changamoto.
tumekataliwa matokeo yake tumejikataa na mwisho tunaona bora kufa. mfano watu wengi wanaofuga rasta ni watu waliojikataa na mara nyingi wameumizwa na wazazi ,wengi wao wamelelewa na mzazi mmoja na hasa mama na kusababisha maumivu ya kumkosa baba yawaumize.
hivyo kabla ya kujiua tafuta ukweli wako wewe ni nani ikiwemo kujua lipi linakuumiza na kisha hakikisha unalikabiri vilivyo na ushindi upo.
2.jitambue wewe ni nani.
jifanyie SWOT analysis mara kwa mara kwachangomoto zilizopo angaliauwezowako na jinsiya kutatua pale ambapo unafikiri hauwezi (kuna tofauti kubwakati ya mtu anaye sema siwezi, nitafanyaje, na nifanyaje -usiwe mtu wa siwezi jaribu kutumia uwezo MUNGU aliokupa kufanyamambo magumu kidogo mfano wakati nikiwa naanza maisha mshahara ulikuwa mdogo na haulingani na malengo yangu hivyo nikiwa na shida ya laki natafuta watu watatu mmoja namwazima hamsini, mwingine 30,000 na mwinginie 20,000)
3.jipokee/jikubali
kuna mhubiri mmoja yuko arusha au moshi yeye ni mlemavu wa miguu, anaitwa supa. mwanzo aliiona udhaifu wake kama mapungufu, lakini alivyo uchukulia kama changamoto akajiuliza kwani miguu kazi yake nini? si kufika sehemu? sasa wapi mimi nilitaka kufika nikashidwa?
hivyo jikubali naudhaifuwako ili uweze kupambana na changamoto zako.
4. jisamehe
jisamehe na kila lililotokea amini limebeba kusudi la MUNGU juu yako hivyo huhitaji kwa kujutia kwakukata tamaa. binadamu ameumbwa kwa kutazama mbele hivyo jisamehe kubali kuanza upya kwa mtazamo chanyawenye mafanikio kwako na kwajamii kwa ujumla ukimpendeza MUNGU.
Yapo mengi ila kwa leoachatuishie hapa vinginevyo nipm twende kwenye specific case