Sioi Sumari achaguliwa na CCM kumrithi baba yake Arumeru Mashariki!

Nilipata taarifa kuwa wazee wa kimila wa kabila ya marehemu Sumari walimlaani huyu kijana kwa kukimbilia kwenye kurithi kiti alichokiacha baba yake kabla hata ya arobaini,hii ni kweli au ni majungu.Na kama ni kweli si anaweza kosa support ya hawa wazee wa mji?

Kwangu mimi kuchaguliwa kwa huyu mtoto wa Sumari ni njia nyeupe kwa CDM kulitwaa hili jimbo kiulaini tena hata bila nguvu,itakuwa ni kama kumsukuma mlevi vile.
 
Ukijumlisha kura za maoni ya CCM 2010 na kura za mwaka huu 2012 ni dalili mbaya sana kwa CCM.
Kutoka kura 16,087 za CCM 2010 mpaka kura 1,033 mwaka 2012! Kura 15,054 zimeenda wapi?
(16087 - 1033 =15,054) CCM...!!!???
 
CCM bana hii system ya Baba na Mwana ndio inayokimaliza Chama
Makamba na January
Kikwete na Ridhiwani
Sumari na Siori
 
Tusubiri vikao vya uteuzi wa jina la mgombea atakayeingia katika kinyang'anyiro kukwaana na upande wa pili (CHADEMA) maana nilisikia kuwa CUF hawapeleki mgombea wao.
 
Sumari 361
Sarakikya 259
Elilehema Kaaya 205
Elishilia Kaaya 176

Anthony Musami 22 na
Ndg Urio 11

Utawala wa kifalme wa mbio za kupokezana vijiti kupokezana kama Korea vile vile.
Mambo ya uroho wa madaraka CCM hata watu wa familia moja wanashindwa kuachiana nafasi. Hizo kura za akina Kaaya ukijumlisha zilitosha kumwibua mmoja kuwa mshindi, mapato ya kugombania nafasi wameishia kugawana kura na hakuna mshindi.

Kwa kweli kijana anastahili pongezi kwa kushinda kura za maoni. Lakini kushinda kura za maoni ni suala moja na kupitishwa na NEC ni suala lingine. Historia inaonyesha kuwa si wote walioshinda kura za maoni walipitishwa na NEC, hebu tujikumbushe ya H. Bashe (Nzega), F. Mwakalebela (Iringa Mjin)...

But with strategic personel behind him, nadhani kupitishwa na NEC itakuwa rahisi. Binafsi nitafurahi kama mchuano huu wa ARUMERU utakuwa ni kati ya vijana wawili.
 
Bila kuzungusha maneno sioi ndo mbunge wa Arumeru hutaki mwaga vumbi .
 
Hivi mbona Watanzania tumekuwa watu wa jabu kiasi hiki? Mtu unasema Sioi ndio mbunge wakati hata ujasikia sera zake, kweli hii forum imeingiliwa siku hizi.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari TBC saa tano usiku huu, Mkutano Mkuu wa CCM Arumeru umemchagua mtoto wa Mar Sumari kumrithi baba yake Ubunge.

Ikumbukwe kuwa rushwa ilitembea katika mchakato huo. Kazi kwenu wana CCM!

inamaana TBC wameweza kuwa wazi kusema rushwa ilitawala kwenye uteuzi huo, kweli hapa kuna ukweli na uhakika.
 
Utawala wa kifalme kivip nyie si amechaguliwa kwa kura? Agrrrrrr, waacheni wameru wachague watu wao sio mnawachagulia kama vp amieni kule mkapige kura!
 
Kupeana vp wakati kura unaziona hapo juu ?

Mi nawashangaa sana hawa watu, na hii itawa cost sana cDM wasipojipanga vizuri wakitegemea maneno ya key board, wataachwa solemba kama igunga vile wabaki kuuma meno!
 
Sioi sumary,ridhiwani Kikwete,January makamba,victor kawawa,Zainabu kawawa,Hussein mwinyi,aman karume,William malechela,munde tambwe,beno malisa,na kadhalika

msije kushangaa 2020 mwanaasha kugombea urais. atakuwa mgombea wa kwanza mwanamke kupitia ccm kugombea uraisi. hahahahahaaaaa
 
huyu dogo bana yaani kwa kuwa babake alikuwa mbunge basi yeye anadhani anaweza kuwa mbunge...mawazo ya hovyo hovyo sana haya

Aliekwaambia anadhani nani? Wapiga kura ndo wanjua kama anaweza kua mbunge au la!
 
Nape Nnauye,A.malima,Fred Lowassa,

wamepigiwa kura na matokeo ndo hayo
lowenya,freeman, kiwelu,raya, uhuru ,raila odinga, bush,karume sio dhambi kuongoza kama unauwezo wa kufanya hivyo,sasa kama baba,mjomba,shemeji,alikuwa kiongozi mimi nisigombee?, hata kwenye sanaa tumeona hivyo,kina abeid ayew,iglesious,kalala junior,damin marley,etc jaribu kufikiri kwa kina na si upinzani tu
 
Back
Top Bottom