Siogopi kushare mume, naogopa HIV

Siogopi kushare mume, naogopa HIV

na ukicheka na nyani utavuna mabua. khaaa! mme kitu kingine Suprise hebu kuwa serious bana.

Usemalo Husninyo ni kweli kabisa, hata mimi nilikuwa nikielezwa kuhusu mume wangu nilikuwa nakataa, siku niliposhikwa mkono kupelekwa nikakuta na mtoto keshazaliwa, ikabidi nifanye mateka ya mtoto, aliporudi home kumkuta , alitokwa na jasho mpk miguuni, So uambiwalo Suprise na wengine changanya na akili zako chukua hatua, wanaume si ndigu zetu na wala hawana huruma na sisi.
 
wazima wote,

Lets share true story. Kwa jina naitwa suprise, mama wa mtoto mmoja na mke ndani ya ndoa yenye miaka 2. Hivi karibuni, kiherehere cha kusoma sms za mume wangu zimenifanya nigundue ana mahusiano nje just kwa mtiririko wa simu na message wanazotumiana.

The usually meet na huwa wanapongezana kwa raha wanazopeana. Kilichonisukuma kuomba msaada hapa ni how to handle the situation coz sina hofu hata kidogo kushare hilo penzi najua ipo siku atachoka atarudi . Sasa katika hii waiting period nifanye nini maana nna hofu na kuletewa virusi n am nt sure kama anakumbuka kutumia kinga.

Nawaza nimwambie live kua najua yupo na mtu fulani na nimuombe atumie kinga. Pili nawaza nikae kimya ila nimuwekee pakiti za condom kadhaa kila atokapo asubuhi hop ataelewa nataka ajilinde. Au tatu niamue kutoshiriki nae kabisaaaaaaa hadi atakapoamua kusitisha ya nje tukapime tena au tutumie condom mke na mume.

Serias am comfused naomba ushauri

Mpendwa Surprise.....miaka miwili ya ndoa kama ni mwaka ndio kwanza mwezi wa pili........ingawa sijakuelewa huko nilipo bold ila nakushauri tu uongee nae achague aendelee na huyo anayesifiana naye kwa mapenzi motomto kwenye sms au wewe.......ukiendelea kunyamaza atamuoa huyo na wewe utakua mke wa pili badala ya wa kwanza.........otherwise kama bado huoni shida basi utakua na huyo jamaa kwa sababu ya kitu Fulani.....last name yake au pesa.......inaonyesha pia huyo jamaa sio mtamu ndio maana roho haikuumi pia........unaonyesha bado mdogo sana.....usicheze na future yako.
 
Ampigie simu mke mwenza amwambie kwamba yeye bi mkubwa Ana ukimwi ajihadhari, kwa hiyo bwana atafukuzwa

Hahahahahahaaaaaa!!! Usinichekeshe , maana hilo liliwahi kutokea mwananyamala, bimkubwa alisikia mumewe ana small house, basi akajikusanya mpk kwa huyo small house, akamkuta na kumwambia ajitayarishe kunywa dozi maana yeye na mumewe wameathirika, basi ile small house, ikamwambia bi mkubwa amsubiri kidogo akaingia ndani alipotoka akatoka na kadi ya klinic ya ukimwi akampa akamwambia kuwa yeye alianza kunywa dozi tangu mwaka 2009, na ungonjwa walionao yeye ndiye kamuambikiza mumewe. Loh!! Bimkubwa alipiga yoweeee !!! na kuanguka chini, akaokotwa na kukimbizwa mwananyamala hosp, ikashindikana kuamka, akafa, na mpk sasa small house ndiyo mke anayetawala pale home.
Kwa hiyo unaweza ukamtishia akakupa majibu mabaya ya kukufanya ukafa gafla bila kupanga. KWA UPANDE WANGU SISHAURI.
 
kiukweli nampenda na sitamani kutoka ila kiukweli pia hainiumizi hata kidogo nnachohofia ni hilo gonjwa tu, ila nahisi nikiongea nae he might change lakini slowly so lengo langu wakati anarudi kwenye mstari arudi ila virusi , so atanielewa nikimwambia tutumie condom as his wife ma dr,

ni ngumu kwa mwanaume kukubali kutumia condom ilihali wewe ni mke wake wa ndoa sio rahisi ukimlazimisha ndio kwanza utampa tiketi ya kwenda nje wewe ongea nae taratibu mueleze kuhusu madhara ya mtandao wa mapenzi
 
Take your time,kwanza nenda kajue status yako,then endelea na uchunguzi wa kina collect more evidence,then mueleze A-Z,mpe side effect za kuacha watoto yatima ,he will respond positively
 
Mkekuu ni hivi;
ukiangalia michango ya ;ke; inaonyesha wivu na hasira kali;
na kujiona kana kwamba they are more safe kuliko hao wenzao
.

Laiti wangejua kuwa hata huko pembeni ;me; wanapata huduma zote
kama wanazozipata huko kwao, wangejitahidi kuongeza mapenzi kwa
hao waume zao kuliko kupanic na kusema sana;

................. najua watanitupia mawe ngoja nikae kando kidogo.


zamu yako imefika funguka sasa mkuu.
 
Huna sababu mama. Hawa wanawake wanaokushauri hapa hawajui tu kuwa waume zao wana wanawake nje. Waume wao wako smart kiasi cha wao kutokujua. Na hawa wanaume wanaojifanya kukuonea huruma ni wanafiki wengi wao kwa kuwa hakuna mwanaume nayemjua mimi mwenye mwanamke mmoja.

Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja, İ tell you me.

Alichokosea mmeo ni uzembe mpaka umejua. Mmeo ni mzembe sana.


Unajifanya umesahau au? .............ina maana hujui kila mtu hapa JF ni msafi including me!!!!!!!!!!!!!!
 
Na hizo ngono wanafanya mda gan? Usione so sema nae kuhusu kutumia kondomu anapokuwa na kimada! Atajistukia na kuacha!
 
acha uchoyo wewe acha na wenzio wapigwe kagera technology....
 
Am sorry to say kuna watu humu ni wapinga ndoa kwa maslahi yao binafsi either ni vimada au ni vidumu....

Mimi huu uzi nilisha utilia mashaka...hakuna mwanamke mwenye akili timamu tena mke halali anaweza sema maneno alosema huyu dada.

Mshindwe na mlegee...mutuwache na ndoa zetu hacha na muache kutuchokonoa...

Ameanzisha huu uzi ili kuwavunja moyo watu walio kwenye ndoa na kuwatisha wale wanaotaka kuolewa...

sijuhi kwa nini hawaanzishi nyuzi zinazowahusu.

 
He babu!ndoa kitu kingine na uhai kitu kingine..sitojiweka kiroho juu kwa starehe za mwengine!

Unapoingia kwenye ndoa ujue ndo ushaipa kondom byebye. Mmeo akuvalie kondom??? Over my dead body!!! Utapigwa nyama kwa nyama utake usitake.

İngia kwenye ndoa utaniambia mwenyewe.
 
Unajifanya umesahau au? .............ina maana hujui kila mtu hapa JF ni msafi including me!!!!!!!!!!!!!!

Hahahah sijasahau, ni huu uzee tu. Hebu nikumbushe bathi nawee.
 
Am sorry to say kuna watu humu ni wapinga ndoa kwa maslahi yao binafsi either ni vimada au ni vidumu....

Mimi huu uzi nilisha utilia mashaka...hakuna mwanamke mwenye akili timamu tena mke halali anaweza sema maneno alosema huyu dada.

Mshindwe na mlegee...mutuwache na ndoa zetu hacha na muache kutuchokonoa...

Ameanzisha huu uzi ili kuwavunja moyo watu walio kwenye ndoa na kuwatisha wale wanaotaka kuolewa...

sijuhi kwa nini hawaanzishi nyuzi zinazowahusu.

sijui kwa nini nimecheka nliposoma coment yako ila upo sahihi kabisaaaaa watuwache na ndoa zetu ebooooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom