Hakuna kazi ngumu kama kuacha kazi, achilia mbali wewe uliyepo kwenye well-paying job, hata anayepata 150k kwa mwezi bado anaona shida kuacha kazi, so it's very understandable.
Kazi inakupa security, ona hata familia inakushangaa unaachaje kazi wakati wao wanaona kazi yako inawasaidia hata wao.
Lakini hili ni lako na mumeo, wengine ni observers na washauri tu. Kama wawili mnaamua mnaweza kuishi bila ajira rasmi, mnaweza kujilipia health insurance kupitia biashara zenu, mnaweza kuendesha maisha yenu na vipato visiathiri maisha yenu, elimu za watoto na maendeleo mengine, unaacha tu.
Changamoto ya biashara, nyingi hazina long lifespan, yaani sisi waafrika hatuwezi kuweka mazingira mazuri ya kuendesha biashara kwa miaka 50 ijayo.