Sina amani ya moyo na maisha ya mjini

Sina amani ya moyo na maisha ya mjini

KAKA WAISLAMU TUNAAMINI KWENYE KADAR KAKA SASA KAMA UNAOGOPA USWAHILI WA WATU WA KULE UTAISHI WAPI SASA, OKTOBA 29 WATU WAMEULIWA HOVYO, BILA HATIA KWA HIYO WEWE HATA USIPO ENDA MAFIA UKAENDA ARUSHA VIJIJINI KAMA MTU ATATAKA KUKUDHURU ATA KUDHURU TU MKUU,

KULE PAKO SALAMA SANA, HAMNA KUFATILIANA LABDA WE UENDE KUFANYA MAMBO YAKO ILA KAMA UKITAKA KWENDA KUTULIA ZAKO MAHALA BILA KUBUGUDHI WATU, AMANI TU MBONA
Mkuu nafurahi sana kwa elimi yako..
Ila sasa mkuu tunaishi kwa taadhari pia.

Mafia naweza kwenda ila suala la kuvuka maji nalo ni changamoto nikisema nimeenda basi nimeenda mazima kule habari za kuja na kuindoka itakua NOOO..

Bi mkubwa ana mpango wa kurudi mafia pia
 
Simple sana
Japo vijiji vya sasa vimeeendelea kuna mdaa asili inapotea ila maisha ya kijiji raha sana hakuna foleni hakuna kelele za ovyo Kuna upendo
kuna vijj vingne afadhal hata huku mujini, mfano unaweza pelekwa kwa mtendaji wa kijij kisa jogoo (kuku namaanisha) wako kamgegeda mtetea wa jiran.
 
kuna vijj vingne afadhal hata huku mujini, mfano unaweza pelekwa kwa mtendaji wa kijij kisa jogoo (kuku namaanisha) wako kamgegeda mtetea wa jiran.
Ebu kuwa seriously 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Vijiji vya moshi hivo au...
 
Ndgu life la mjini silielewi mkuu kweli sielewi mkuu najikuta naingia kwenye msongo wa mawazo wakati life ni very short na bado unakua unawaza waza tu..

Kiukweli ndgu natamani life hata la kuwa mbali na simu au mitandao kabisa an mi nipate access ya kuishi kijijini huko no 5G but peace 💯

Mkuu sijui nisemeje
Mkuu kwa haya maelezo wenda una changamoto ya afya ya akili,ukiwa serious unaweza kupata msaada na ukapona kabisa.
 
Mkuu mbeya sehemu gani..
Tukuyu
Kiwira
Chunya ...nk

Oky nipo tayari naomba tuongee zaidi...
Hapana sio huko kote ,mimi nakupeleka kwa watu wanaitwa wamalila ,nakupeleka kwa watu wanaolima kahawa ,viazi vya chips, maharagwe ,mahindi na paleto

Huku si rahisi kwa kila afikaye mbeya kupajua maana ni pembezoni mwa mbeya jiji yaani unaingia mbalzi alafu unakutana na rough road mpaka ninaposema na hao watu wote mjini yao ni mbalizi kwa maana mazao yote tajwa hapo juu isipokuwa kahawa yananunulika hapa mbalizi sehemu moja almaarufu kwa kalinga mastoo

Ila kahawa unaamua wewe uuze ikiwa shambani au uibangue na kuuza iliyobanguliwa kwa wateja wanaokuja mashambani au unahitaji uibangue uwauzie viwanda vya ushirika almaarufu CPU

Huku kuna sehemu kama nane ila zote zinakaliwa na watu wanaoitwa wamalilq ,huku kuna baridi sehemu nne na sehemu nne zingine hazina baridi ila ni moderate .

Huku fursa nyingi bado zipo kwasababu wenzetu walichelewa kidogo kufika shule ,ila wanaye icon wao anaitwa Barack mpenja ni hapo mechi yoyote anayotangaza huyu bwana ukifungua banda haukosi wateja .

Ila ukifika huku usipende sana kumzungumzia mkuu wa majeshi mstaafu MBOMA ,kwanini usimmxungumzie ?
Ni kwasababu ilikuwa ni icon yao ila wao wanadai haikuwakumbuka kuwaingiza jeshini ila ikaupendelea sana upande wa ukweni kwa akina Chonka bojo iwe .😀

Hivyo nihitimishe na Mboma ni mmalila wa huko .

Je unajua kuwa pale stereo temeke asilimia sabini na tano mazao yake haswa maharagwe na viazi vinatoka umalila ? Umestuka ennhe?

Ndiyo mimi ni mzaliwa wa hapo mjini kati kule kwa bwana kichwa duara alipowafukuza machinga wasikae njiani wapishe wacongo wafanye biashara kwa amani ,sijitambulishi unijue ila najaribu kukuambia kuwa kati ya gari Mia zinazofika huko umalila kubeba mzigo ni gari mbili tu ambqzo dereva au tingo hatonijua sasa ukiwauliza mzigo unaenda wapi ni hapo wananipa jibu la ninalokuambia kuhusu stereo temeke .

Huwezi kulima bwana mdogo wewe maana unawaza mishangazi sana basi usijipe presha huku wenzio hawashiki jembe watoto wa mjini kama mimi na wwe ila mkulima shida zake haziishagi hivyo wenzio wanawapa hela kuanzia elfu kumi mpaka milioni kadha wa kadha ili kahawa ikishavunwa wenzio wanapewa kahawa ila kwa faida ya mara mbili .,Unastuka enhe?

Ndivyo ilivyo kaka na wengi wametoboa lakini wenzako wananunua mahindi na maharagwe mashambani na kuleta mbalizi elfu tano kwa gunia kumi si haba kaka

Unajiuliza je wakinidhulumu itakuwaje ,oyaa umetoka mjini wewe ni mjanja shika ukaribu na wenye majina yao kwenye biashara ambao kijiji kizima kinasema yule anamiliki bunduki ni hapo mavuno leo ,jioni mdaiwa anabisha hodi mwenyewe kuleta mazao yko

Unajiuliza sasa kama sitaki hivyo huku wenzio hawana cha B O T wala T R A wanagawa hela za riba kama njugu maana biashara zipo na watu hela wanashika ila siri kuu ukaribu na wenye kuogopeka toka awali ..

Oya mimi napaita kijijini ila kwa waliozaliwa sumbawanga kirando tarafa ya mtakuja wananishangaa kwa kuwa mimi inaonekana sivijui vijiji kwasbabu huku ni mwendo wa dakika hamsini mpaka lisaa upo zako mjini unakula mshangazi pale mapacha lounge songwe au mbalzi kwa dada Netsha au ofisini kwangu wanakopaita kwa RPC wa mtaa mbalzi

Mdogo wangu naandika natetemeka mikono mwenzio mimi ni mnywaji na mlevi wa bia ila sasa nipo kwenye mfungo hivyo napata shida sana mida ya iftari ikikaribia ,haya nakurleza maana ukifika huku usiseme wewe muislamu sema wewe mkiristo ili upate ushirikiano wa biashara kaka ,huku wote wanaamini waislamu wana majini hivyo mwenzio nikiwa huko sivai kanzu wala sipokei simu na kusema salamu ya kiarabu ni bwana asifiwe tu ,katika mfungo ni siri yangu tu .

Naiona shauku yako kutaka kujua mimi naishi huko na nilifuata nini ?
Pole kwa hiyo shauku mimi siishi huko ila maisha yamewahi na yanaendela kunipeleka huko iwe asubuhi au jioni kwasbabu nahisi ninachokitaka kipo huko .

Wenzio kule mbuzi na kuku sio habari za kufungulia uzi kujisifia hapa mara sasa nimeanza kufuga ,kule wanayo mifugo na inapt8kana kwa bei nafuu kikubwa uwakaribie wenyeeji ila uwe na eneo lako la kuwafugia maana maneo mengi ni kilimo .

Center zipo na ni kali tu huku kila bia unayokunywa hapo samaki samaki na huku utaipata tu ,unajiuliza kibipi wakati hawajasoma ,kaka asikudanganye mtu hela ndiyo kila kitu wenzio huku mtu kununua gari akalipaki uwani mwaka mzima lengo wamu9ne na gari ni suala la kawaida sasa itakuwa kununua hivi vinywaji vya milioni ?

Eti mtu anaanzisha uzi kusema watu wanatumiq hela kwa kufuru kisa mtu mmoja kufunga bar ?

Huku kiangazi hizo sio habari kwasisi watumishi ndiyo sehemu ya pombe za bure kikubwa usilewe ukajisahau wakakushusha heshima asubuhi .

Kwasasa nimechoka kaka ,wqcha nifuturu nikishiba tutajibizana vyema .

Karibu kijijini ,kukimbia mji sio ujinga ila kuzikimbiza ndoto zako ,niko njiani kurudi nyumbani Kesh ni sikukuu ya akina mama

Wabillah taufiq
 
Aiseee pole sana, tuweni makini na maneno tunayotumia! Global crime kama hizi sio za kuletea mizaha kabisa! Anything can happen..
Nina experience ya hili jambo
Humu humu Jamiiforums nilikuwa naulizia jambo fulani tena ni haki ya msingi kabisa, nikapewa muongozo na wadau humu.

Siku naenda ile ofisi ya Umma utadhani ndio Nilikuwa nasubiriwa nijae kwenye zone yao 😀😀😀

Lakini pamoja na lile tukio nimepata taarifa muhimu sana.

Watu humu wapo wapo tu lakini usalama wetu sio guarantee kabisa
 
Nina experience ya hili jambo
Humu humu Jamiiforums nilikuwa naulizia jambo fulani tena ni haki ya msingi kabisa, nikapewa muongozo na wadau humu.

Siku naenda ile ofisi ya Umma utadhani ndio Nilikuwa nasubiriwa nijae kwenye zone yao 😀😀😀

Lakini pamoja na lile tukio nimepata taarifa muhimu sana.

Watu humu wapo wapo tu lakini usalama wetu sio guarantee kabisa
Uko sahihi ni kweli kabisa na nimependa kwa maana kila siku tunalalamika sana Tanzania haijali ila kuna mambo nyeti kama haya wanafuatilia kimyakimya!
 
Na je utakaa eneo lina fursa zipi , ajira za kueleweka , huduma muhimu au unakaa ilimradi umekaa😅😅
 
Wakuu salam alykum
Ndugu katika imani niseme ukweli tu.
Sio kama nina hali ngumu ya maisha laaah ila tu kiukweli sina.amani na maisha ya mjini.

Napachukia sana sna sana sana
Natamani nikaishi vijijini huko mbali kabisa.

Mi kazi yangu ikawa ni kulima, kufuga na kufanya kazi za kijijini.

Napenda sana niwe karibu zaidi na nature, tofauti na maisha ya huku mjini kelele, joto na ugomvi kila siku.

Napenda maisha ya kukaa mbali na ndgu jamaa na marafiki nataka niwe na mtandao mdogo sana wa marafiki tena sio marafiki ni kama majirani tu.

Napenda maisha yangu yote nimalizie huko.

Napenda niishi kama babu zetu ambao walikua wanakaa vijijini huko ndani ndani ndio kitu napenda.

Je nafanyaje ili niweze kufanikisha jambo langu....

Nitafurahi sana pia akipatikana mtu ambaye ana wiwa kushirikiana na mimi katika hili.. au atakae nipa wazo Bora la mimi nafikaje huko.

Asanteni 🙏🙏🙏🙏🙏
#twendezetukijijini Jumlisha
That's life

Hayo ni maisha mazuri sana kuliko mengine yote
 
Mkuu nafurahi sana kwa elimi yako..
Ila sasa mkuu tunaishi kwa taadhari pia.

Mafia naweza kwenda ila suala la kuvuka maji nalo ni changamoto nikisema nimeenda basi nimeenda mazima kule habari za kuja na kuindoka itakua NOOO..

Bi mkubwa ana mpango wa kurudi mafia pia
Basi subiri ye atangilieko kwanza AKISHA setlle WALAU MWAKA mmoja NENDA kapacheki ALAFU utajiongeza ila KULE AMANI, HATA matukio ya OKTOBA 29 hayakufika huko
 
Wakuu salam alykum
Ndugu katika imani niseme ukweli tu.
Sio kama nina hali ngumu ya maisha laaah ila tu kiukweli sina.amani na maisha ya mjini.

Napachukia sana sna sana sana
Natamani nikaishi vijijini huko mbali kabisa.

Mi kazi yangu ikawa ni kulima, kufuga na kufanya kazi za kijijini.

Napenda sana niwe karibu zaidi na nature, tofauti na maisha ya huku mjini kelele, joto na ugomvi kila siku.

Napenda maisha ya kukaa mbali na ndgu jamaa na marafiki nataka niwe na mtandao mdogo sana wa marafiki tena sio marafiki ni kama majirani tu.

Napenda maisha yangu yote nimalizie huko.

Napenda niishi kama babu zetu ambao walikua wanakaa vijijini huko ndani ndani ndio kitu napenda.

Je nafanyaje ili niweze kufanikisha jambo langu....

Nitafurahi sana pia akipatikana mtu ambaye ana wiwa kushirikiana na mimi katika hili.. au atakae nipa wazo Bora la mimi nafikaje huko.

Asanteni 🙏🙏🙏🙏🙏
#twendezetukijijini Jumlisha
Mchawi pesa tu ndugu. Kama umeshasettle vizuri financially (sio hela nyingi kwa account ila mfumo wa hela uliposimama vizuri)

Ukifikia hapo, wala usimuulize mtu yeyote, tafuta Kijiji chochote Tz chenye uhakikq wa maji na barabara, ikiwezekana karibu na mito isiyokauka, ukimudu tafuta heka zako 5 (hata nusu heka) hata nusu heka weka Kibanda chako classic (sio mambo mengi ila modern) Anza Maisha upya hapo.

Yaani ni kwamba, Ukihisi uko poa kiuchumi huna haja ya kuomba ushauri. Chomokq tu! Usiwaze chochote, sijui shule watoto, sijui baa, sijui nini na nini, nyanyuka tu.
 
Moja ya Siri ya Kijiji Bora, ni pale kile utakachokuta migomba inamea vizuri sambamba na minazi. Kijiji Cha namna hiyo hawajawahi kutwa na njaa, kwa mazao mengi sana yatakuwa yanamea hapo, uchumi wa eneo hilo huwa umesettle sana.
 
Umepatia mkuu, moshi, arusha ni shda mtu anaenda kwa mtendaj anasema mm sitaki kukanyaga sehemu moja na fulani, wakat wanashare uchochoro.
Daaaah aiseee huko hatareeee basi...
Sasa sehemu kama hizo mimi sitoboi kabisa mi staki kabisa... 🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom