Sina amani ya moyo na maisha ya mjini

Sina amani ya moyo na maisha ya mjini

Kuwa makini usije tatua tatizo refu kwa njia fupi....mara nyingi Huwa inatabia ya kujirudia zaidi ya awali
Sizani kama nikiwa mbali na hii jamii takutwa na hiyo hali tena.

Maana hii ni mara ya pili nakumbuka mara ya kwanza ilinitokea nikiwa jeshini nilitamani nitoroke jeshi nizamie vijiji vya ndani vya kule nachingwea niwe naishi kule...

Ila nikakaa sawa nikajaribu kuongea na mama mzazi kuhusu hii hali alistuka sana.

Kuna mda huwa naonea wivu watu waliotangulia an naona haya maisha ni bora kupumzika an kuwa kaburini utakua mbali na haya ya dunia.

Huwa nawaza mbali sana mpaka sasa naona nimefikia point ya mwisho ni kwenda kijinini tu nikaishi huko.

Japo mama mzazi hakubaliani na hii hali ila mimi naona kabisa siwezi kabisa mama anasema niende alipo yeye huko nje ila napo hakupo sawa maana nitabaki kwenye circle ya familia.

Yaani nipo dillema huwa natamani nianze upya kabisa niwe mimi kama mimi
 
Ahahahha ngoma ni kwa sababu ya bardi watu wanapigana miti kila leo
Hapana sio baridi, mbona arusha kuna baridi na maambukizi yako chini compared na njombe( nyanda za juu kusini)? Shida watu wa kule hawana elimu kuhusu STDs, tabia zao n.k, picha linaanza sijawahi kukataliwa na demu yoyote mpaka naondoka njombe
 
We jamaa ebu naomba nipe info kwa uzuri mbna umeongea seriously sana hivo et ebu naomba nielekeze vzr mkuu
Kijijini jau wewe komaa mjini tu ndio kuna maisha, kijijini kuna shida nyingi sidhani kama utaweza kuzivumilia, KILIMO hili neno lisikiege tu usiombe ukutane nalo utajuta na utapakumbuka dar mzee
 
Wakuu salam alykum
Ndugu katika imani niseme ukweli tu.
Sio kama nina hali ngumu ya maisha laaah ila tu kiukweli sina.amani na maisha ya mjini.

Napachukia sana sna sana sana
Natamani nikaishi vijijini huko mbali kabisa.

Mi kazi yangu ikawa ni kulima, kufuga na kufanya kazi za kijijini.

Napenda sana niwe karibu zaidi na nature, tofauti na maisha ya huku mjini kelele, joto na ugomvi kila siku.

Napenda maisha ya kukaa mbali na ndgu jamaa na marafiki nataka niwe na mtandao mdogo sana wa marafiki tena sio marafiki ni kama majirani tu.

Napenda maisha yangu yote nimalizie huko.

Napenda niishi kama babu zetu ambao walikua wanakaa vijijini huko ndani ndani ndio kitu napenda.

Je nafanyaje ili niweze kufanikisha jambo langu....

Nitafurahi sana pia akipatikana mtu ambaye ana wiwa kushirikiana na mimi katika hili.. au atakae nipa wazo Bora la mimi nafikaje huko.

Asanteni 🙏🙏🙏🙏🙏
#twendezetukijijini Jumlisha
Chukua 500,000 Mpe Madrid Win Keshokutwa!, Stimu yote ya kukaa mjini itakata!
 
We jamaa ebu naomba nipe info kwa uzuri mbna umeongea seriously sana hivo et ebu naomba nielekeze vzr mkuu
mzee nilikulia dsm(kigogo round about) mwaka fulan nikasema nimepachoka town kama wewe, nikaingia mkoa kilichofuata mzee mpaka jeans, raba nilikuwa najiuliza mara ya mwisho kununua ilikuwa lini, nilipakumbuka dar mzee....ila kama unakiweza KILIMO cha mkono nenda mzee, nisikutishe bure
 
Ni wazo zuri, ila huko kijijini utakuwa na mtandao au ndo unajitenga na civilaization kabisa? Mi napenda mixcha ya tradition na modernity
 
Ni wazo zuri, ila huko kijijini utakuwa na mtandao au ndo unajitenga na civilaization kabisa? Mi napenda mixcha ya tradition na modernity
Ndo huko huko kwenye traditional life maana kwa hapa dasalama uwezi pata
 
Raha sana sana sana kuna sehemu tanga ndani ndani mpaka nasemaga sizani kama kuna watu wanazeeka kule.

Nashangaa wanaotoka vijijini kuja mjini for what reason...

Watu hawajui tu how nature is beautiful na ndio maana watu wakubwa unakuta wanaenda kutalii ndani ndani huko...

Sasa just imagine sehemu ambayo watu wanaenda kutalii na kupunguza stress wewe yale ndo maisha yako
Tanga Maeneo ya wapi mkuu
 
Back
Top Bottom