Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 65

Nusu saa badaye, nilikuwa ndani ya ofisi ya daktari, alikuwa ni mwanamke mmoja wa makamo. Alionekana alikuwa na muda mrefu kwenye taalumu ya uganga.
“Tatizo nini?” aliniuliza. “Kifua kinauma.”
Nilipomjibu akaandika kwenye kitabu chake. Akaniuliza tena:

“Kinaumaje?”
“Ni kama kinawaka moto ndani kwa ndani.”
“Unamawazo?” alizidi kuniuliza. Nikatafakari kidogo swali lake kisha na mimi nikamuuliza.

“Kuna binadamu asiye na mawazo dokta?”
“Nina maanisha unamsongo wa mawazo kwenye maisha yako, hasa kwa siku za hivi karibuni?”

“Hapana.” Nilimjibu. Akaniuliza tena:
“Unafanya kazi gani?”
“Mimi ni mchezaji wa mpira.”
“Tatizo limeanza lini?”
“Usiku wa kuamkia leo.”
Akaendelea kuandika majibu yangu kwenye tabu lake la kumbukumbu.
“Kuna dawa nitakupa, zisipokusaidia rudi tena hapa. Sawa?”

“Sawa dokta.”
Aliniandikia tembe za vidonge fulani vitatu vya aina tofuati. Siwezi kabisa kusahau majina ya zile dawa. Tembe moja ilikuwa inaitwa Ampidox , nyingine inatwa Predistone pamoja na Panadol.

Nazikumbuka vizuri kabisa.
Tuliondoka na kurudi nyumbani tayari kwa kuanza dozi ya dawa hizo. Hali yangu ilikuwa bado ni tete, kila wakati nilikuwa nahisi maumivu makali na kifua kikitaka kulipuka kwa joto kali.

Tulipowasili, Cholo aliniacha sebuleni nipumzike, kisha yeye akaondoka na kwenda kuripoti klabuni. Nilichukua chupa ya maji safi na kumeza tembe hizo.

Ilikuwa ni kama baada ya dakika 20 baada ya kutumia vidonge hivyo... Nilipatwa na muamivu makali nashindwa hata kuyaelezea mfano wake.

Ndani ya mwili wangu kulikuwa ni kama vile kuna uji wa plastiki umemwagwa kwenye mifupa yangu. Nilikuwa nalia kama mtoto mdogo. Jasho lilikuwa linanichuruzika kama maji mwilini mwangu. Dunia ilikuwa inazunguka kwa kasi kama panga boi.

Ndani ya muda mchache nilipoteza fahamu, pumzi nazo zilikuwa zinakata kama utambi wa mwisho kwenye mshumaa unaovyoishilizia. Sasa dalili ya malaika mtoa roho ilikuwa waziwazi mbele yangu. Katika hali hiyo, nikawa nahisi kama kuna kundi la watu wameingia mule ndani kisha wamenizinguka.

Wakati fahamu zinanipotea kabisa, nikawa nahisi kama lile kundi la watu linaniangalia namna ninavyozama kwenye wingu la giza nene,
Hii hatari
 
hongera Shunie sie wacheza mpira tunajifunza kitu hapa
 
Sehemu ya 66

“Kwisha habari yake....” hiyo ndio sauti ya mwisho kunipitia kwenye ufahamu wangu uliokuwa ukingoni kabisa.
Baada ya hapo sikujua tena kilichoendelea. ****

SIKUJUA fahamu zilinirudia baada ya muda gani au baada ya siku ngapi kwani kichwani mwangu nilikuwa nikipitiwa na taswira nyingi za ajabu ambapo zilifuatiwa na vipindi virefu vya giza na utupu mrefu akilini.

Miongoni mwa yale yaliyopita ni tukio la kukimbizwa na yule ngo’mbe mwenye pembe ndefu na kupamiwa katika eneo la kifuani.

Jambo jingine lililopita akilini mwanguni ni la mchumba wangu Lawalawa. Kumbukumbu ya nyakati nzuri kwenye penzi letu zilikuwa zikinitesa akilini. Mwanamke huyo ambaye kwa sasa alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine, hakufutika.

Kuna wakati maumivu makali yaliutesa moyo wangu hasa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa. Niliishi maisha ya tabu sana katika siku za ukubwa wangu. Kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa. sikumfahamu yeyote katika eneo nililokuwa nikiishi.

Nilikuwa Sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu. Kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu. Sikutamani kufa kwa sababu sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa kwa wakati huo.

Kwa kweli yalikuwa maisha ambayo sikuwahi kufikiri kama ningeishi. Ajibu Maganga, mchezaji machachari wa klabu ya Mzizima Fc ya jijini Dar es salam, nilikuwa kichaa!.

Mwendawazimu niliyerukwa na akili. Mwehu aokotaye makopo mtaani.
MAISHA yangu yalikuwa yamebadilika kama mchezo fulani hivi wa kijinga jinga. Niliishi nikiwa binadamu niliyerukwa na akili kwa muda mrefu mno.

Kuna methali ya kiswahili inasema: Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Naam! msemo huo pia uliyasadifu maisha niliyoishi.

Ilifika siku dunia ikafunguka. Nuru ikaniangazia. Nikawa kiumbe niliyezaliwa upya kwa mara ya pili. ***** MASIKIO
yangu yalikuwa katika mkanganyiko dhidi ya nzi waliokuwa wakicheza gwaride katika masikio yangu na kusababisha misisimko yenye karaha mbaya sana.
 
Sehemu ya 67

Hali ile iliniondolea utulivu kabisa. Nilijaribu kutikisa kichwa changu lakini wapi! Kichwa kilikuwa kizito ajabu!
Hata nilipojaribu kuinua mkono wangu ili niwaswage wale wadudu, nilihisi mikono yangu ikizuiliwa kutenda agizo langu.
Nilifumbua macho kivivu.

Macho yangu yakakutana na sura ya mwanadada aliyekuwa ameniinamia huku akitabasamu ilihali kwa mbali nikisikia muziki wa heart break hotel wa Elvis Presley.

“Nimekufa na mungu ameniingiza peponi,”niliongea kwa sauti ya chini. Wakati huo wale nzi sikuwasikia tena sikioni.

Tabasamu zuri la msichana lililoacha mashavu yenye vishimo katikati ya mashavu yake lilisafisha ukungu wa taswira ya picha niliyoiona. “Peponi kuna wadada wazuri hivi. Loh!” nilinong’ona tena.

“Halafu kumbe kwa Mungu huwa kuna miziki ya Elvis Presley?” nilijiuliza kwa sauti iliyo kwaruza na macho yaliyo legea huku nikiendelea kumtizama yule mdada mwenye tabasamu la kukata na shoka.

Mrembo alizidi kunipa zawadi ya tabasamu lake tamu, kabla ya tabasamu hilo kupanda cheo na kuwa kicheko kidogo kilicho acha kinywa chake wazi na kunifanya nizidi kupata faraja isiyo fafanulika.

"Hapa ni Buzabazeba Kigoma, siyo mbinguni Ajibu," alisema huku akinitizama kwa macho ya upendo na huruma. Ukimya mfupi ukapita baina yetu.

Nikabakia namwangalia huku yeye akionekana kulengwa lengwa na machozi, akashindwa kabisa kustahimili kutazamana nami usoni. Akayatupa macho yake kando na mara machozi yakambubujika mashavuni mwake.
 
Sehemu ya 68

Kwa nini unalia sasa?” nilimuuliza huku nikijilazimisha kunyanyua mkono na kumgeuza ili aniangalie. “Silii ni furaha tu kwa kuwa umeamka leo,” alisema huku machozi yakiendela kumbubujika.

“Ngoja nikakuandalie uji.” Mdada mwenye tabasamu la kukata na shoka aliniambia, na muda huo huo aliondoka ndani ya chumba nilichokuwa nimelala.
Nilinyanyuka kwa tabu pale kitandani na kuketi kitako. Viungo vyote vya mwili vilikuwa vimechoka, nadhani ni kutokana na kulala muda mrefu.

Nikawa najiuliza. Nilipatwa na kitu gani maishani? Kwa nini sina kumbukumbu ya mambo mengi maishani? Yani kichwa changu kilikuwa kinajiwa na taswira ya mambo mawili tu. Ng’ombe aliyenichoma na pembe kifuani, sambamba na taswira ya mpenzi wangu Lawalawa.

Sasa na huyu binti anayefurahia kuamka kwangu ni nani? Na huku Bezabazeba Kigoma nafanya nini? Nilijiuliza. Kila kitu kwenye maisha yangu ilikuwa ni kitendawili kisicho na majibu.
Nilizungusha macho mule ndani, nikajiona nimo kwenye chumba ambacho kwa harakaharaka nilibaini nilikuwa kwa mganga wa kienyeji.

Kwenye kona moja ya chumba kile kulikuwa na vyungu vyeusi sambamba na tunguli lukuki zilizotapakaa chini.wakati kwenye ukuta ambao ulikuwa umepakwa chokaa muda mrefu kiasi cha kutoa taswira isiyovutia kulikuwa na ngozi ya mnyama pori sambamba na kioo cha kujiangalizia. Nipo kwa mganga nafanya nini? Naumwa nini? Kwa nini kwa mganga wa kienyeji?

Niliendelea kujiuliza. Hata hivyo nikaona nitaendelea kujichosha kwa maswali ambayo sitapata majibu. Nafsi yangu ikakiri kwamba kuna namna fulani nilikuwa nimepoteza kumbukumbu katika maisha yangu na kwa kuwa nimerudiwa na fahamu sina budi kuwa na subira.

Nilitaka kusimama chini ya kitanda ikiwezekana nitoke nje hata hivyo nikajikuta nakosa kabisa nguvu ya kuteremka pale kitandani.na ndani ya dakika hiyo hiyo nikawa nahisi njaa kali mno.

Nilibakia nimejituliza kitandani nikingoja uji kutoka kwa dada mwenye tabasamu liwezalo kukusahaulisha madeni kadha wa kadha unayodaiwa.

Muda mfupi baadaye, mlango wa chumba ulisukumwa, yule binti aliyejaliwa wowo zuri na tabasamu la kipeke dhdi ya mamilioni ya wanawake katika dunia alirudi mule chumbani akiwa na bakuli la uji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom