Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,168
- Thread starter
- #121
Sehemu ya 59
Nilipanda basi hadi Tabora mjini, kwa kuwa nilikuwa nimefika mapema. Nikachukua tax iliyonipeleka hadi mtaa wa Airport, nyumbani kwao Lawalawa.
Niliteremka garini nikaikabili nyumba hiyo. Siku zote nilikuwa na hofu ya kufika nyumbani kwao na mwanamke huyo.
Ila kwa kuwa nilikuwa nimekwisha amua kujilipua kwa ajili yake, sikuogopa chochote kumfuta mwanamke kwao.
Niligonga geti, muda mfupi badaye akatokeza mwanamume mmoja ambaye alionekana ni kama mfanyakazi wa ndani ya nyumba ile ya kifahari. “Habari yako, unasemaje?” mtu huyo aliniuliza bila kusubiri niitikie salamu yake.
“Naitwa Ajibu Maganga, nashida na Lawalawa.”
“Lawalawa!” “Ndio.”
“Kwani huna tarifa?”
“Sina, kuna nini kwani?”
“Baada ya ndoa yake, alisafiri kwenda kwa mumewe huko Uarabuni. Yemen.” Jamaa alisema.
Nilihisi nguvu zinaniishia miguuni, jasho likanichuruzika maungoni mwangu.
“Unasema kweli?” “Sina sababu ya kukudanganya,” jamaa alinieleza, uso wake ulionesha wazi wazi ukweli wa kile alichokuwa akizungumza. Macho yaliniiva, akili ilinizunguka.
Jamaa akaniuliza tena:
“Kwani wewe unatokea wapi?”
Sikupoteza muda wa kumjibu swali lake, niliondoka nikimwacha mwanaume huyo akinishanga.
Nilitembea huku nikihisi kifua chote kikichemka, nilijiona kama ninaye kaangwa kwenye sufuria la mafuta. Kuthibitishwa juu ya kuolewa kwa mwanamke yule ilikuwa ni zaidi ya maumivu moyoni.
Nilichukua tax nikamtaka dereva anipeleke hoteli yoyote nzuri. Dakika 20 badaye nilikuwa Ristalemi hoteli, baada ya malipo ya chumba, nilingia ndani, huko nilijifungia na kulia kama mtoto mdogo. Nililia penzi la Lawalawa, mwanamke huyo niliyemweka moyoni, nikamuhifadhi sehemu muhimu ndani ya moyo wangu.
Eti naye alikuwa amenipa pigo takatifu.
Niliitelekeza familia yangu hosipitali ya Bungando, mwanangu akafariki dunia kwa kukosa matibabu, nikamwacha mwanamke aliyenipenda kwa dhati. Yote kwa ajili ya Lawalawa.
Sasa naye alikuwa amenigeuka, amekimbilia kwa mwanaume mwingine. Halafu mpumbavu mimi nabaki nalia chumbani kama hayawani. Hapana haiwezekani. Siwezi kuwa bwege kwa kiwango hiki.