Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 75

“Ajibu, hebu achana na mawazo ya visasi.”

“Pili, hebu ona maisha yangu sasa yalivyo haribika. Kwa nini alinitendea jambo baya kama lile? Lengo lake lilikuwa ni lipi hasa?”

“Ajibu nimesema achana naye, Mungu ndiye mlipaji wa kila jambo?” “Kwa hiyo unataka nikae kizembe tu kusubiri mungu anilipie?”

“Muachie Mungu mume wangu, usipende kujikita kwenye shari zisizo za msingi na walimwengu” mke wangu alilalama. Hakupenda hata kidogo kuona mume wake naingia kwenye matatizo ya aina yoyote.

Sikumjibu, nililiweka kiporo chambo hilo. “Jambo la pili mke wangu,” nilisema huku nikiwamwangalia usoni. Nikaendelea. “Hatuwezi kuendelea kuishi na wazee hawa siku zote. Tunafanya nini mama?”
Mke wangu Pili, alinyamaza kidogo, akanisogelea na kulaza kichwa chake kifuani mwangu, kwa sauti yake ya upole naye akaniuliza:

“Hutaki tena kucheza mpira?”
“Hapana. Sihitaji, kuna msemo unasema, jitihada za mja haziwezi kushinda kudra za mwenyezi Mungu, nadhani hapa ni mwisho wangu wa mchezo wa soka. Mungu alinikadiria maisha yangu ya soka yaishie vile”

“Nimefurhi kusikia hivyo Ajibu. Na kama unatambua kudra za mwenyezi Mungu basi achana na visasi, sawa mume wangu?”

Sikumjibu. Akaendelea kuongea. “Lakini kuhusu jambo uliloniuliza nilikwisha liwaza tangu siku ya kwanza nilipofika hapa Kigoma, njia ni moja tu ya kuanzisha maisha yetu upya.”

“Ipi hiyo?” niliuliza kwa kiherehere.
“Kufanya biashara ya dagaa, kuzinunua dagaa za Kigoma hapa na kuzipeleka mjini Dar, hii inalipa sana na mtaji wake si mkubwa.”

“Una akili sana we mwanamke,” nilisema kwa furaha. Nikamkumbatia na kummiminia mabusu motomoto.

Siku chache badaye, mpango wangu namke wangu Pili, tuliwashirikisha mzee Mo na mkewe, nao bila choyo walitupa baraka zote.
“Lakini tungehitaji msaada wenu zaidi?” niliwaambi.

“Kama upi baba?” Bibi Mo aliuliza.
“Msaada wa kifedha, tunahitaji kama laki mbili na nusu tu.”
“Hilo mmepata. Kuna jingine?”
“Hakuna wazee.”

Kwa kweli, tulitokea kushibana nao mno. walituchukulia kama wanawe wa kuwazaa, hasa kwa kuwa binti yao wa pekee, ambaye alikwisha fariki miaka mingi akiwachia mjuuku aitwaye Mohammed ama Mo.
 
Sehemu ya 75

Baada ya kupata kiasi cha fedha tulichotaka, mimi na mke wangu, Pili, tulikwenda hadi Bangwe, ufukweni mwa ziwa Tanganyika. Tukalangua dagaa. Siku mbili zilizofuata nilipanda treni kupeleka mzigo ule Dar mke wangu akibakia Kigoma.

Kwa kweli biashara ile ilikuwa nzuri tu, na ilitupatia kiasi cha fedha cha kutosha kabisa. Mara nyingi mke wangu alikuwa akininunulia dagaa Kigoma Kisha mimi nazisubiria Dar, nikishazipokea naziuza katika masoko mbalimbali hapa jijini Dar.
Kwa kuwa mimi na mke wangu kwa kiasi kikubwa tulikuwa tumetengwa na ndugu na jamaa kutokana na historia tuliyopitia maishani. Tulilazimika kuishi mjini Kigoma.

Tulihama nyumbani kwa mzee Mo kule ujiji Buzebazeba japokuwa wao hawakupenda kabisa kitendo kile, tulipanga chumba maeneo ya Mwanga mtaa wa kwa Ndaje.

Na katika nyakati zote hakuna mtu aliyejali wala kuuliza habari zangu, timu ya Mzizima na wachezaji wake mashuuri akiwemo Felix Kisu ambaye alikwisha pona majereha ya kuvunjika na kurudi uwanjani. Alikuwa tishia mno nyakati hizo.

Ajibu maganga yule mcheza soka wa klabu ya mzizima hakuongelewa popote. Cholo naye, yule jamaa yangu wa Zanzibar sikujua habari zake kabisa.
 
Sehemu ya 76

Maisha yaliendelea kati yangu na mke wangu Pili kwa furaha tu. Pili wangu alinenepa na kupendeza.

Wakati hali hiyo inatokea kwakwe. Bado siri ya kutokuwa na upendo kwakwe iliendelea kubaki kuwa siri yangu moyoni, Lawalawa aliendelea kunivuruga mno nafsini.

Niliishi na pili kwa kuwa tu, alikuwa ni mfadhili aliyeokoa maisha yangu, ni kwa sababu tu yeye alinipenda, na ni kwa sababu tu nilimwonea huruma, lakini sikuwa nampenda kabisa. Moyo wangu ulikuwa wa baridi mno kwakwe.

Siku moja nikiwa kwenye biashara zangu jijini Dar nikamkumbuka yule mganga wa Unguja, ambaye Cholo alinipeleka kwenda kuwaroga wachezaji wenzangu. Jamaa alikuwa kiboko sana yule.

Nilimkumbuka mganga huyo baada ya siku hiyo kumfikiria sana kipenzi changu Lawalawa. Bado nilikuwa sijamalizana na mwanamke yule chotara.

Wazo lililokuwa linatekenya fikra zangu ni kumwendea mganga yule ili aweze kumvuta kichawi Lawalawa ambaye alikuwa ameolewa huko nchini Yemen na mwanaume wa kirabu.

Penzi zito lililokuwa linachemka polepole moyoni mwangu liliuzidi nguvu utashi wangu. Ni muda mrefu ulikuwa umepita, sikujua kama Lawalawa alikuwa bado yupo Yemen ama alikwisha rejea Tanzania, sikujua kama bado yupo ndoani ama kaachika. Sikujua.

Mchana wa siku ya Jumanne nilipanda boti ya kwenda Zanzibar kwa malengo mawili. Kwanza kumvuta lawalawa mikononi mwangu. Lakini pili kulipiza kisasi dhidi ya mtesi wangu. Felix Kisu
Saa tisa alasiri tulitia nanga bandari ya Unguja. Kwa kuwa nilikwisha wahi kufika Zanzibar nikiwa na rafiki yangu Cholo haikuwa kazi kufika kwa mgaga.

Nilitembea nikipita mjini Malindi, Mji Mkongwe kisha Darajani. Nikapanda daladala ya Kiembe Samaki. Muda mfupi badaye niliwasili nyumbani kwa Sheikh Majeed Mapaka.

Nilimkuta sheikh huyo akiwa nje ya nyumba yake anasikiliza redio. Aliponiona akanilaki kwa ukarimu.
 
Kiruuuu [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Nachukia kwa watu wanaowashobokea watu ambao hata hawajuani analazimisha kukujua hata kumjua simjui
Hahah...

Hadi hapa wewe hufanani na Pili labda kidogo unafanana Tatu...

Ila hii stori iko kwenye level fulani hivi, nyota ya kyepe yai na mirinda nyeusi ya baridiiiii
 
Hahah...

Hadi hapa wewe hufanani na Pili labda kidogo unafanana Tatu...

Ila hii stori iko kwenye level fulani hivi, nyota ya kyepe yai na mirinda nyeusi ya baridiiiii
Hahahahaha we mzee bwana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom