Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 69

“Umeweza kukaa mwenyewe!!” alibwatuka, uso wake ulionesha kunishangaa kwa kitendo cha kuniona nimeketi kitandani.

Nilibaki na utulivu wangu, sikujihangaisha kujibu maneno ya miss bantu huyo.
Alinisogelea uso wake ukisawijika kwa furaha kubwa. Alichota uji kwa kijiko kwenye lile bakuli na kuninywesha.
“Kunywa baba huu uji utakusaidia” alisema.

Kwa kweli yule mwanamke alinionyesha mapenzi makubwa mno. Nilikunywa ule uji kwa pupa, dakika chache badaye bakuli likabakia tupu. Mwanamke akabaki akiniangalia usoni kwa huruma.
“Hivi unaitwa nani wewe?” hatimaye nilimuliza.

Badala ya kujibu, binti akaninishika kichwa changu na kukivutia kwenye kifua chake. Akanikumbatia huku akibubujikwa na machozi. Kitendo hicho kikaniongezea maswali utitiri.

“Jina lako nani jama?” nilimuliza tena.
“Kweli umenisahau mume wangu?”
Shit!

Kumbe niliwahi kuwa na mke maishani? Nilimuoa nani, Lawalawa? Hapana. Lawalawa alikuwa mpenzi wangu tu, tulipendana kwa muda mfupi, mwarabu koko yule akaniacha na kwenda kuolewa na mwarabu mwenziye wa huko nchini Yemen sasa vipi tena na huyu miss tabasamu aniite mimi ni mume wake? Ni kimeo gani hiki Yarabi? nilijiuliza kimoyomoyo.

Nilijitoa kwenye kifua chake na kumwangalia. Nilimtizama sura yake kwa muda, nikaiingiza sura hiyo katika ubongo wangu, kidogo ni kama niliwahi kuiona mahala fulani hivi lakini bado sikumbuki ni wapi.
“Wewe ni nani lakini?” nilimuliza tena.

“Mimi ni Pili. Pili mkeo uliyezaa naye mtoto mmoja akafariki kwa saratani ya damu.”

Ewaa!!.
Sasa kila kitu kilifunguka. Kumbukumbu ya mke wangu Pili ikanifungukia ubongoni kama nuru ya jua la asubuhi lichomozavyo tokea mlimani.

N ikamkumbaka vema mwanamke huyo. “Pili!!” nilimwita.
Alinitikia kwa kichwa akanikumbatia tena kwa nguvu.

“Nilipatwa na nini mimi?” nikamuliza swali jingine.
“Ulirogwa mume wangu, walikuroga wenzio?” alisema.

“Wenzangu! Wenzangu gani?”
“Wacheza mpira wenzako, mapaka shume wale.”Pili alinieleza huku akiwatusi tena wachezaji wa mpira.

Maneno yale pia yakawa yanafungua kumbukumbu zingine zilizokuwa zimejifunga funga ndani ya kichwa changu. Angalau sasa nikawa najiwa na vipande vya kumbukumbu ya maisha ya nyuma.
 
Sehemu ya 70

“Nimelala hapa kwa muda gani?” nikazidi kumsaili pili kwa maswali.
“Tangu tulipokukamata huko mtaani na kukuleta hapa, ulilala kitandani leo inaweza kuwa ni siku ya tano ama nne kama sijakosea.”alinijibu.

“Mlinikamta mtaani!! Kivipi hapo? Yanii mtaani nilikuwa nafanya nini?”
“Ajibu tulia....”

“Nijibu wewe.” nilimkemea, uso wangu ulionekana kutaka jibu la swali langu.
“Ulikuwa umerukwa na akili mume wangu,” Pili alinipasulia.

Nilikiona kile chumba kinayumbayumba. Nikahisi nataka kuanguka, pili akawahi akanikumbatia. Zilikuwa ni taarifa nzito zilizourarua moyo wangu. kwa kweli siwezi kusahau siku hiyo. Niliumia sana nafsini.
“Mungu wangu!!” nilimaka.

“Kwa nini mimi... kwa nini sasa? Yani mimi niwe kichaa! Iweje nifanyiwe hivyo?” nilizidi kuongea mambo yasiyoeleweka sawasawa, taarifa za ugonjwa huo zilinishitua mno.

“Unataka kuniambia nilikuwa natemba uchi mtaani?” niliuliza swali ambalo kwa pili nadhani aliliona la kipumbavu, alitulia kidogo, kisha akaanza kunisimulia mambo mengi mno.

Alianzia kunieleza tangu siku nilipomtelekeza hospitali ya Bugando akiwa na mtoto wetu ambaye alikuwa mahututi, mimi nikatimkia mjinin Tabora kuvinjari maisha na mwarabu koko wangu Lawalawa.

“Pamoja na kwamba siku zile ulinikimbia ukaniacha na mwanao, peke yetu, hadi Mungu naye aliponinyang’anya mwanetu, siku hiyo ulikuwa umeondoka na moyo wangu Ajibu, ” alisema huku machozi yakimlenga. Akatoa kitambaa na kupangusa macho yake.

Mwanamke huyo alikuwa na mapenzi ya dhati mno dhidi yangu, bahati mbaya tu binti wa watu aliangukia kwa mpumbavu mimi, nisiyejua thamani ya upendo. Pili akaendelea kunisimulia:

Hata siku zilipotoka taarifa katika vyombo vya habari kuwa umerukwa na akili, watu waliokuwa wanajua mambo uliyonifanyia walishangalia, lakini mimi....alisema huku donge zito likiwa limemkaba kooni. Akaendelea.

“Niliweka nadhiri ya kuwa nawe bega kwa bega japokuwa nilitambua hukuwahi kunipenda maishani.” Alisema. Akapangusa machozi Akaendelea kunieleza.

“Ajibu. Ndugu zako wote, wakiwemo wazazi wako, hawakuwa radhi na wewe tangu siku zile uliponiitelekeza mimi na marehemu mwanangu...”
 
Sehemu ya 71

Alishindwa kuendelea kueleza, alibubujikwa na machozi, ukimya ukapita, mrembo akaendelea kulia, akapangusa macho kwa leso kisha baada ya kujituliza akaendelea kusimulia.

“Nilisafiri hadi Dar es salama, nikakusaka mtaani. Wiki mbili mfululizo, wiki ya tatu nikakupata kwenye majalala ya mitaani ukifukua chakula kama kunguru. Ulikuwa uchi wa mnyama wewe.
Nimepata tabu kubwa hadi kukufikisha hapa Kigoma.

Ajibu nimepitia misukosuko mikubwa maishani, kama ujuavyo mimi sina kazi wala fedha za kukutibia hospitalini za kisasa, ilitokea kama bahati tu nilimpata msamaria mwema akanishauri nikulete hapa. Ndugu na jamaa wananiuliza vipi nikupe msaada mwanaume usiyekuwa na haya usoni.

Mara kwa mara wamekuwa wakiniuliza nina sababu gani ya kukupa msaada mtu usiye na mapenzi na damu yako mwenyewe. Lakini masikio yangu niweka pamba.”

Maneno ya Pili yalinichoma moyoni, niliendelea kukiona chumba kile kikiyumba yumba kwa kasi zaidi. Ukimya mrefu ukapita baina yetu.
Nilikuwa mwanaume niliyemfanyia ushenzi wa kila aina mtoto wa watu.

Ajabu binti aligeuka na kuwa mithili ya malaika wa ukombozi dhidi ya mpumbavu mimi. Alinilipa wema dhidi ya ufedhuli niliomfanyia huko nyuma Katikati ya ukimya, mara mlango wa chumba ulisukumwa. Akaingia mama wa makamo, alikuwa amevaa hijabu.

“Bibi huyo!” Pili alimlaki, ile huzuni yake iliyeyuka ghafla na kuwa tabasamu lile lile adhimu. “Hatimaye mgonjwa ameamka!” yule mama naye alisema. “Ameamka, yanii sikutegemea kabisa jamani.” “Umempa uji?
 
Sehemu ya 72

“Tayari amekunywa.”
“Ulitia na ile dawa niliyokwambia.”
“Ndio, Nilichanganyia” Pili alijibu huku akiningalia kwa mashaka.
“Haya mume wako yupo nje analo jambo anataka kuongea na wewe.” Mama yule alimwambia Pili.

Moyo wangu ukapiga kite. Nikajiuliza: Inamaana kumbe huyu mke wangu wa zamani, Pili. tayari alikwisha olewa na mwanaume mwingine?

Shit.
Ama ndiye yule msamaria aliyenieleza kwamba alimpa msaada wa matibabu yangu?

WAKATI najiuliza mambo yote hayo, tayari Pili mke wangu, alikwisha simama na kutoka nje kwenda kuonana na huyo anayesemwa ni mumewe.
Ndani nilibakia na yule mama wa makamo ambaye Mke wangu, Pili, alikuwa akimwita bibi.

“Inamaana Pili alikwisha aolewa na bwana mwingine?” nilimuliza yule mama.
Badala ya kujibiwa, yule mama aliangua kicheko, alicheka hadi machozi yakamtoka. Nilibaki kimya nikimwangalia Bi mkubwa huyo anavyo nicheka kama punguani. “Unasema nini...kwamba mkeo amenini vile...” aliongea halafu akanicheka tena.

Kicheko chake kilipokwisha akaniambia:
“Pili hajaolewa baba yangu...Huyo ninayesema ni mumewe ni babu yake, ambaye ndiye anayekutibia tangu umefika hapa, yeye hupenda kumwita mjukuu wake, Pili, mkewe.”

Eboo!! Kweli mama alikuwa na haki ya kunicheka. Angalau maneno yake yalinifurahisha hata mimi, nilitoa pumzi nyingi kwa mkupuo, nikahisi kitu fulani kimeniachia mwilini mwangu.
 
Sehemu ya 73

Kwa kweli pamoja na kwamba sikuwahi kumpenda mke wangu Pili, maishani mwangu, ila sikupenda kabisa mwanamke huyo awe na mwanaume mwingine katika nyakati kama zile.

Nakiri wazi mpumbavu mimi sikuwa na chembe yoyote ya mapenzi kwakwe, ila pamoja na hilo nilikuwa bado sijamalizana naye.

Kwa fikra za kihayawani nilizokuwa nazo, niliamini siku moja isiyokuwa na jina, ningeachana na msichana huyo kiroho safi, yanii bila yeye au mimi kuwa na maumivu yoyote. “Nilidhani ameolewa,” niliongea tena mbele ya yule mama. Alikuwa akiniangalia kwa uso wa tabasamu.

“Pili hawezi kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako baba yangu.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Binti anakupenda mno, wanawake wenye moyo wake, wamebakia wachache sana kwenye huu ulimwengu wa leo,” alisema.
Ukimya mfupi ulipita baina yetu. Kisha nikamuliza.

“Na wewe ni nani hapa?”
“Ni mke mwenziye na Pili.” Jibu lake likanifanya niendelea kumfahamu vizuri, huyo mama.

Alikuwa ni mwanamke aliyependa sana masikhara. “Alaa!. Kwa hiyo babu kizee aliyemwita mke wangu ndiye mumeo?” Wote tulicheka.

Kwa kweli ukarimu wa mama huyo ulinipa nguvu na tumaini jipya pale kitandani nilipokuwa nimeketi.

Niliendelea kumtambua yule mama, alikuwa akijiulikana kwa jina maarufu kama bibi Mo, yeye na mumewe, ambaye naye alikuwa akiitwa babu Mo. Ufupisho wa jina la mjukuu wao aliyekuwa akitwa Mohammedi au Mo.

Muda mfupi baaada ya utani na dhihaka kati yangu na bibi Mo. Mke wangu Pili, aliyeitiwa huko nje na babu Mo, mzee mwenye umri kati ya miaka 60 ama 65 waliingia ndani ya chumba kile. “Mgonjwa umeamka?” Babu Mo akiwa kwenye uso wa ukarimu, alinihoji huku akisogea karibu na kitanda changu. Alikuwa mzee mwenye mvi nyingi kichwani.

“Jamaa alikuwa kwenye shinikizo kubwa la nafsi,”bibi Mo aliongea kwa kiherehere.
“Kwa nini?” mke wangu Pili pamoja na babu Mo wakauliza kwa shauku. “Ni baada ya kuja kumwita Pili, kuwa anaitwa na mumewe. Alidhani mkewe alikwisha olewa miaka mingi yeye akiwa kwenye nusu kaputi kitandani,” mama yule wa makamo alisema:

Watu wote mule ndani wakanicheka.
Mzee Mo alishika kiganja cha mkono wangu na kuningalia kwa makini. Halafu akaniambia:
 
Sehemu ya 74


“Utapona babu. Ulikuja ukiwa vibaya sana.”

“Ilikuwaje babu?”
“Nilikukuta na bibi hapa...” aliongea huku akigeuka kumwangalia Pili, akaendelea.
“Bibi hapa, alikuwa akihangaika na wewe kwenye mahopistali ya serikali huko Dar es salam huku wewe ukiwa zezeta uliyeshindikana.

Siku niliyokuoneni pale Muhimbili, nilipokutizama tu nikaona unaye mdudu mbaya sana kichwani mwako.

Hili lilinipa kibali cha kutaka kukusaidia kabisa, nisingeweza kuacha kutoa msaada kwa mtu ambaye naona naweza kumsaidia, nilikuchukueni wewe na mkeo huko Dar na kukuleta hapa Kigoma kwa matibabu.”

“Mungu wangu! Ndivyo ilivyokuwa?” “Ndio...Ehh...Yeah,” watu wote mule ndani waliitikia kwa pamoja huku wakinikodolea macho.

Nilikuwa nina sababu zaidi ya elfu moja kumshukuru mzee Mo na mkewe bibi Mo, bila kumsahau mke wangu Pili.
Nilitibiwa nikiwa kitandani kwa mzee Mo kwa kipindi kirefu tu. Wakati wote mzee yule alinieleza kuwa amejitolea kunisaidia kwa nguvu na uwezo wake wote hadi nitakapopona na kurudi kwenye shughuli zangu, kulipa wema ule itabakia kuwa juu yangu.

“Sina cha kukulipa mzee wangu, hata kama nitakupa magari yote ya kifahari nyumba na noti, bado havilingani na wema wako mzee.” Siku moja baada ya kuwa nimeimarika kiafya nilimweleza mzee Mo. Nilikuwa nimepona kabisa baada ya kutumia dawa za miti shamba kwa muda mrefu sana.

“Mimi ni mganga wa kienyeji, kazi hii mara nyingi naifanya kwa wito, wadudu wangu walio kichwani wananiagiza kufanya hivyo,” Mzee Mo, alinijibu. Aliposema wadudu alimanisha maluhani ama majini aliyokuwa nayo kichwani mwake.

Kwa kuwa nyakati zote za matibabu hatukuwa na kitu chochote cha kufanya, Mimi na mke wangu, Pili, tuliendelea kuishi kwa wazee wale wawili, Ujiji mtaa wa Buzebazeba.

Na katika kipindi chote hicho, mke wangu Pili alikuwa akinionesha mapenzi motomoto.

“Mke wangu.” Usiku mmoja kitandani, nilimwita mke wangu Pili.
“Abee, mume wangu.”
“Nimepona sasa...” nilimwambia, nikaendelea.

“Tunahitaji kuanza upya maisha, sijajua naanzia wapi mke wangu. Kitendo cha kutupiwa jini na Felix Kisu, kinanifanya nione bado ninalo deni kwakwe, siwezi kumwacha hivi hivi.”
 
kweli wanawake akina PILI wako wachache dunia hii
 
Asante sana shunie. Majukumu yamenibana nimezorota kidogo kufatilia hadithi. Hadithi nzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom